HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MASAUNI ATANGAZA MAJINA YA WATUHUMIWA 16 WA MAUAJI YANAYOENDELEA KIBITI, MKURANGA NA IKWIRIRI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto),alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha baadhi ya picha za watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP),Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI ENG. NGONYANI AKAGUA UJENZI WA BARABARA MBANDE-KONGWA KM 11.71

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
 Sehemu ya barabara ya Mbande - Kongwa yenye urefu wa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara  nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Salome Kabunda (kushoto), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (wa pili kushoto), pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakikagua barabara ya Hogoro - Kongwa KM 14.57 kwa kiwango cha changarawe wilayani humo, mkoani Dodoma.

Serikali imesisitiza nia yake ya kuhakikisha ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa yenye urefu wa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami unakamilika kwa wakati.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema hayo mkoani Dodoma, mara baada ya kukagua sehemu ya mradi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa yenye urefu wa KM 49.14 ambao ujenzi wake unaendelea na kumuagiza Kaimu Meneja Wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Salome Kabunda kusimamia mradi huo kikamilifu.
"Tutahakikisha fedha za mradi huu zinapatikana kwa wakati ili mradi ukamilike  mapema ikiwa ni mkakati wa kuifungua wilaya hii na kuhuisha fursa za kimaendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa", amesema Eng. Ngonyani.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa za uwezekezaji katika maeneo hayo ikiwemo kurahisisha huduma za usafirishaji wa mazao kwa Wilaya hizo mkoani humo.
Naye, Kaimu Meneja wa TANROADS, mkoa wa Dodoma Eng. Kabunda, amemhakikishia Naibu Waziri kuwa watamsimamia Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kwa karibu ili ubora wa barabara hiyo uendane na thamani ya fedha.
Aidha, Eng. Kabunda amewataka wananchi wa Wilaya ya Kongwa kushirikiana na mkarandarasi ili kuwezesha ujenzi huo kwenda kwa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi ameishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwani utachochea maendeleo wilayani humo.
Takribani shilingi Bilioni 7.5 zinatarajiwa kutumika katika sehemu ya kwanza ya mradi huo wa Mbande-Kongwa ambapo KM 5 zitajengwa na zinatarajiwa kumalizika ndani ya miezi nane.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

NAIBU WAZIRI MH. LUHAGA MPINA AFANYA UKAGUZI KATIKA MAENEO YA BOKO BUNJU TEGETA NA KEKO MWANGA.

 Mtaro wa maji Machafu uliokuwa ukilalamikiwa na wakazi wa keko mwanga katika mtaa wa Mafuta.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina (Katikati)  akimsikiliza katibu wake Bw. Daniel Sagata (kulia) alipokuwa akizungumza kuhusu sehemu ya ukuta wa kiwanda cha red sea uliobomolewa kupisha maji ya mvua, wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa katika ziara yake alipotembelea katika eneo la keko mwanga mtaa wa Mafuta kushoto ni Bw. Salea Haffif mwakilishi wa kiwanda cha Red Sea.
 Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina akimsikiliza katibu wake Bw. Daniel Sagata  kulia alipokuwa akimuonyesha tuta lililojengwa na kiwanda cha saruji cha Wazo cha Tegeta Jijini Dar es Salaam, Tuta ambalo  lilijengwa baada ya kujengwa mtaro wa kupitisha maji ya mvua yaliyokuwa yakisababisha kero ya mafuriko kwa wakazi wa maeneo jirani yaliyotaka na makorongo yaliyochimbwa na kiwanda hicho kwa lengo la kutafuta maligafi za kutengeneza saruji, kero hiyo inasemekana kupungua baada ya Naibu Waziri Mpina kuwahai kufanya ziara kiwandani hapo na kutoa maagizo.
 Sehemu ndogo ya korongo inayomwaga maji ya mvua na kuingia katika mfereji uliojengwa na kiwanda cha wazo.
Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Kiongea na vijana katika eneo la Bunju A Usalama, kuhusu Karavati (halipo pichani) ambalo lilikuwa ni moja ya kero ya kuchangia mafuriko katika eneo hilo hasa katika vipindi vya mvua kutokana na uchafu wa mazingira uliopelekea karavati hilo kuziba. Naibu Waziri Mpina ametembelea eneo hilo leo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa  magizo aliyotoa kwa sekta husika wakati wa ziara yake aliyowahi kuifanya katikamaeneo hayo.

MASAUNI AZINDUA MPANGO WA KUWASAIDIA WAKIMBIZI NA NCHI ZINAZOHIFADHI WAKIMBIZI, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke. 
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi  Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo.
 Sehemu ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini  pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

NAIBU WAZIRI NGONYANI AKAGUA UJENZI DARAJA LA KELEMA

 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akikagua hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari.
 Mkandarasi wa Kampuni ya Chicco, Li Jianzheng, akimounesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), namna ya usukwaji nondo katika Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 wakati alipokagua daraja hilo mkoani Dodoma leo.
 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu ujenzi wa Daraja la Msui lenye urefu wa mita 45 lililopo katika barabara hiyo, mkoani Dodoma, leo.
 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela – Bonga Km 88.8 Eng. Kini Kuyonza akimuonesha taarifa ya mradi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Manyara, leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akikagua zege lililowekwa katika barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 eneo la Mlima Kolo uliopo wilaya ya Kondoa, wakati alipokagua ujenzi wake, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Kini Kuyonza

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Akizungumza leo mkoani Dodoma, mara baada ya kukagua daraja hilo lililopo katika barabara ya Mayamaya-Mela KM 99.35, Naibu Waziri Ngonyani  amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo na  barabara za maingilio katika daraja hilo kutarahisisha  huduma ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani ya  Manyara na Arusha.
"Daraja hili na barabara zake ni kiungo muhimu kati ya mkoa huu na mikoa  ya Manyara na Arusha  na pia inaunganisha  nchi ya Tanzania, (Cape Town) South Afrika hadi (Cairo) Misri, hivyo kurahisisha huduma za  usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka hapa kuelekea maeneo mengine", amesema Eng.Ngonyani.
Aidha, Naibu Waziri ameitaka kampuni ya ujenzi ya Chico kuhakikisha inamaliza daraja hilo ifikapo mwezi wa Kumi mwaka huu kama ilivyoandikwa kwenye mkataba ili wananchi kuweza kulitumia.
Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Eng. Leornado Licari, amesema kuwa kwa sasa mradi umefika asilimia 87 ambapo hivi karibuni wanatarajia kuweka lami.
"Nakuhakikishia kumaliza mradi huu kwa wakati kwani kazi zilizobaki kwa sasa hivi ni chache, kwa hiyo hadi kufikia mwezi Septemba tutakuwa tumeshakamilisha kazi zote", amesisitiza Mhandisi Mshauri Licari.
Naibu Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kikazi ya siku moja katika mikoa ya Dodoma na Manyara ambapo pamoja na ukaguzi wa daraja hilo pia amekagua madaraja mengine matatu likiwemo la Msui, Kingali na Mela pamoja na ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga KM 88.8.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


KLINIKI YA AFYA YA AKILI KUTOLEWA KUPITIA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA NCHINI- DK.KIGWANGALLA

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni mjini Dodoma.

Kliniki ya Afya ya Akili kutolewa kupitia Hospitali zote za Rufaa nchini- Dk.Kigwangalla Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla amekutana na viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni Dodoma. 
Viongozi hao walikaribishwa na Wabunge wawakilishi wa Watu wenye changamoto mbali mbali za ulemavu nchini, Mhe. Amina Mollel (Mb.) na Mhe. Stella Ikupa (Mb.). Katika kikao hicho Dkt. Kigwangalla ameweza kujadiliana nao mambo mbalimbali viongozi hao wa TUSPO ikiwemo uanzishwaji wa Kliniki ya Afya ya Akili kupitia Hospitali zote za Rufaa za Mkoa hapa nchini. 

“Nimekutana na Viongozi wa TUSPO ambao wanashughulika na masuala ya Afya ya Akili. Tulijadili mambo mengi na niliwaelezea mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwenye eneo hili, ikiwemo Uanzishwaji wa Kliniki za Afya ya Akili kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mkoa nchini nzima. Lakini pia Uanzishwaji wa Rehabilitation Centers kwenye kila kanda na usambazaji wa Madaktari bingwa wa Afya ya Akili na wataalamu wote wanaohitajika kutoa huduma hizi kwenye Hospitali na vituo hivi” 

Ameeleza Dkt. Kigwangalla. Aidha, ameongeza kuwa, amewaahidi uongozi huo wa TUSPO, kuwa atafuatilia juu ya hatua ambayo mchakato wa kukamilisha muundo wa kisheria (legal framework) ulipofikia na sababu za kukwama kwake toka sheria ya afya ya akili ilipotungwa mwaka 2008. “Serikali ya awamu ya tano ni sikivu kwa wananchi wake bila kubagua. 

Nina aahidi kulifuatilia sualala uanzishwaji wa Baraza la Afya ya Akili, kwani tayari sheria ilishatungwa muda mrefu. Na kwamba ni kwa nini Baraza la Afya ya akili halijaanzishwa toka sheria itungwe mpaka leo na kwa nini mpaka leo hakujawa na kanuni za Afya ya akili kuelekeza juu ya mambo mbalimbali” alieleza Dkt. Kigwangalla ambapo amewaahidi kuwapa taarifa ya utekelezaji wa masuala hayo kwenye Bunge la Mwezi November 2017.

Kuhusu Magonjwa ya Akili: Magonjwa ya akili ni magonjwa ambayo yanaathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda, na hivyo kuwa na tabia au mwenendo uliotofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi, na nyanja nyingine za kijamii. 

Tabia hizo zinatokana na ugonjwa wa akili kuathiri ufanisi na shughuli za mtu husika (mgonjwa) au huathiri jamii nzima inayomzunguka endapo mgonjwa huyo hatopatiwa matibabu stahiki na kwa wakati muafaka. Kwa Tanzania imeeelezwa kuwa baadhi ya wagonjwa wengi wa akili hawafiki katika vituo vya kutolea huduma za afya na badala yake kuishia kwenye tiba za jadi au kutelekezwa na kunyanyapaliwa huku takwimu za zinaonyesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu takriban milioni 45 na kutokana na taarifa ya afya ya akili kwa mwaka 2014/15 inaonyesha kuwa idadi ya watu 817,532 wanaugua magonjwa mbalimbali ya akili nchini, hii ni karibu asilimia 2 ya watanzania wote.

 Pia idadi hii ni ongezeko la wagonjwa 367,532 ukilinganisha na takwimu za mwaka 2013/14 walikuwa ni 450,000. Kati ya wagonjwa wote wa akili kwa mwaka 2014/15 wanawake ni ni 332,000 na wanaume ni 485,532. Mkoa wa Dar-Es-Salaam unaongoza kwa kuwa n awagonjwa wengi nchini ukifuatiwa na mkoa wa Dodoma na mkoa wa mwisho ni Lindi. Idadi hiyo ya wagonjwa ni wale walioweza kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma ya afya hapa nchini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla (mwenye koti nyeusi kulia) akifanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni mjini Dodoma.

MASAUNI AFUNGUA GEREZA LA WANAWAKE MPWAPWA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akishirikiana na Viongozi wengine kufungua Gereza  la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa  kushirikiana na wafungwa.Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa, mkoani Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mheshimiwa George Lubeleje , akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa,  akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,Mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kulia), akiongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa (kulia) kuelekea katika eneo lilipo  Gereza la Wanawake Mpwapwa, lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana  na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Wananchi wa Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni  askari magereza kwa kushirikiana  na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu, MOHA
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Benki ya Exim inatarajia kujenga nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana na changamoto za makazi ya askari  wa jeshi hilo hapanchini.
Akizungumzia changamoto za Makazi ya askari wa Jeshi la  Magereza Nchini, wakati wa uzinduzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alisema Serikali inatambua changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari iko katika mazungumzo na benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.
“Nawaomba  askari wetu nchi nzima  wawe na subira  Serikali inatambua na  inashughulikia changamoto ya makazi ya  askari na tayari tuko katika mazungumzo na wadau ikiwemo benki ya Exim kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 9500, lengo ni kukidhi kiu ya makazi ya askari na familia zao,” alisema Masauni.
Awali akitoa maelezo ya ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa alisema ujenzi wa Gereza hilo umefanywa na wataalamu ambao ni askari Magereza kwa  kushirikiana na wafungwa kama sehemu ya utekelezaji wa  amri ya Mh. Rais Dk. John Magufuli ya kutaka wafungwa watumike katika kazi za uzalishaji ikiwemo kilimo,ujenzi na ufundi mbalimbali.
Ujenzi wa Gereza hilo umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia  kuhifadhi wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la Kongwa mkoani Dodoma pamoja na kuepuka usumbufu wa  ndugu wa wafungwa kusafiri mpaka wilayani Kongwa kwenda kuwaona ndugu zao.

“HALI YA DAWA NCHINI IMEIMARIKA”-MHE.KIGWANGALLA

  Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya upatikanaji wa Dawa nchini imeimarika na kufikia asilimia 83.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Khamis Kigwagalla alipokuwa akijibu Hoja mbalimbali za Wabunge leo Mjini Dodoma.

“Moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma nchini”Alisema Mhe.Kigwangalla.

Amesema kuwa katika kutekeleza azma hii Serikali ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi kufikia bilioni 251,500,000,000 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Aidha hadi kufikia Mwezi April 2017 Jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma kupata mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba na Vitendanishi.

Kufuatia Ongezeko ilo la fedha kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeimarika sana.

“Hadi kufikia tarehe 15 Januari 2017,Mkoa wa Kagera pekee umepokea kiasi cha bilioni 4,150,767,216 kupitia fungu 52 kwa ajili ya kununulia dawa,vifaa,vifaa tiba na vitendanishi.”Aliongeza Mhe.Kingwangalla.