HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

WAZIRI MWAKYEMBE AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI NAHODHA WA SERENGETI BOYS

NAPE AIPONGEZA SERENGETI BOYS KWA KUFUZU FAINALI ZA AFCON GABON 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye




SERENGETI BOYS YAFUZU AFCON U-17

Tanzania imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-17 zitakazofanyika Gabon mwaka huu.
Serengeti Boys ilifuzu baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Congo iliyomchezesha mchezaji aliyezidi umri.
Tanzania itaingia Kundi B ikichukua nafasi ya Congo kundi hilo lina timu za Niger, mabingwa watetezi Mali na Angola.
Timu nne zinazofanikiwa kuingia katika nusu fainali zitafuzu moja kwa moja Kombe la Dunia la Fifa U17 litalofanyika India baadaye mwaka huu.
Waziri wa Michezo, Nape Nnauye aliandika kwenye akaunti yake ya twiter kuipongeza Serengeti Boys kwa kufikia hatua hiyo.
“Mungu Mkubwa! Tumefuzu kwenye fainali za Afrika chini ya umri wa miaka 17. Nia, uwezo na sababu za kuchukua kombe hili tunazo. Hongera TZ” aliandika Nape.

SERENGETI BOYS YAENDELEA KUJIFUA KWA KASI KABLA YA KUWAKABILI WENYEJI WAO VIJANA WA CONGO KESHO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


CONGO TUTAWAZIKA HAPA... Ndivyo anavyoonekana kusema Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo. Uwanja huo ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Congo, Jumapili Oktoba 2, 2016.
Huyo ndiye Muhsin Malima Makame au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kuonyesha uwezo wake uwanjani pindi anapoingia kipindi cha pili kuokoa jahazi. Akikosa kufunga huwa ni kama bahati mbaya.

Kiungo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Kelvin Nashon ‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Beki wa kushoto wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Nickson Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Libero wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ally Msengi (Kulia) akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah akipigia hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili
Baadhi ya vigogo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, kutoka kushoto ni Dk. Gilbert Gilbert Kigadye, Mratibu wa timu, Pelegrinus Rutayuga na Dk. Sheicky Mngazija wakifuatilia mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Kipa Na. 1 wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.

SERENGETI BOYS WAJIFUA JIJINI BRAZZAVILLE TAYARI KWA MTANANGE WA MARUDIANO NA CONGO JUMAPILI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakijifua kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville. 
 Kocha wa Makipa wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Muharami Mohammed maarufu kwa jina la Shilton (wa pili kushoto) akiwanoa vijana wake, Kelvin Kayego (kushoto), Ramadhani Kabwili (wa tatu kushoto) na Samwel Brazio kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.


 Purukushani langoni ambako Dickson Job akiwa hewani akikoa hatari langoni kwake.
 Shughuli ilikuwa kati ya Kelvin Nashot Naftal (kushoto) na Zuberi Rashid Ada.
Madaktari wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Dk. Sheicky Mngazija (kushoto) na Gilbert Kigadye wakifuatilia kwa karibu mazoezi ya timu kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo. Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.  Picha zote na Alfred Lucas wa TFF.

SERENGETI BOYS WATUA CONGO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda walikopiga kambi kabla ya kuwavaa vijana wenzao wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Massamba Sebat, Brazzaville. Timu hiyo imefikia Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini hapa. Kikosi hicho kimetua salama salmin kujindaa kuifumua Congo Jumapili. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Wakiingia Hotelini.
Makocha wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Muharami Mohammed Sultan maarufu kama Shilton (kushoto) anayewanoa makipa, Kocha Mkuu Bakari Nyundo Shime au Mchawi Mweusi na Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini Brazzaville, Congo.

Kipa Na. 1 wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili akionyesha furaja ya kuwa fiti mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya, tayari kabisa kuwavaa vijana wenzao wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Massamba Sebat, Brazzaville. Timu hiyo imefikia Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini hapa. Kikosi hicho kimetua salama salmin kujindaa kuifumua Congo Jumapili. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Kutoa kushoto, Kibwana Shomari, Yohana Mkomola na Rashid Ada wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maya Maya mara baada ya kutua leo wakitokea Kigali nchini Rwanda walikopiga kambi kabla ya kuwavaa vijana wenzao wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Massamba Sebat, Brazzaville. Timu hiyo imefikia Hoteli ya Michael’s iliyopo Barabara ya Nelson Mandela jijini hapa. Kikosi hicho kimetua salama salmin kujindaa kuifumua Congo Jumapili.

SERENGETI BOYS KUWEKA KAMBI NJE NCHI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Baada ya kuifunga Congo-Brazzaville mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya vijana, Serengeti inatarajiwa kuondoka Alhamis wiki hii kwenda kupiga kambi nje ya nchi.

Hata hivyo, taratibu zinapangwa kuhakikisha kwamba timu hiyo inakwenda kupiga kambi kwenye nchi tulivu inayolingana hali ya hewa na Congo Brazzaville kadhalika chakula pamoja na mazingira.
Tanzania na Congo Brazzavile, zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na timu itakayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa fainali hizo.
Katika mchezo uliofanyika Septemba 18, Serengeti Boys ilipata mabao yake kupitia Yohana Mkomola na Abdi Makamba wakati yale ya Congo yalifungwa na Langa-Lesse Percy na Makouana Beni ambao mashabiki wa soka walikuwa wakiwalalamikia kuwa ni “wakubwa.”
Ili ifuzu kwa fainali zitakazofanyika mwakani huko Antananarivo, Madagascar katika fainali zitakazoanzia Aprili, 2017, Serengeti Boys inatakiwa ibaki na matokeo yake ya sasa na ihakikishe inapata ushindi na kama sare basi wapate bao kufuta faida ya bao la ugenini ambalo Congo Brazzaville walikuwa wanasheherekea baada ya mchezo.

WAZIRI NAPE KUTOA LAKI TANO KWA KILA GOLI LA SERENGETI BOYS

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo Pichani) kuhusu mchezo kati ya Serengeti Boys na Congo-Brazaville utakaofanyika Septemba 18 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Picha na May Simba WHUSM

Na Lorietha Laurence-WHUSM.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa shilingi laki tano kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Serengeti Boys katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Taifa dhidi ya Congo-Brazzaville.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mhe.Nape amesema milango ipo wazi kwa wadau wengine wa michezo kujitolea katika kuiwezesha timu na hivyo kufanya vizuri katika mechi hii ambayo ni muhimu sana kushinda ili kufuzu kwa fainali hizo.

“Hii timu ni yetu sote hivyo inahitajika tuimiliki, tuepe nguvu, tuiombee ili iweze kufanya vizuri na hatimaye kufuzu kuingia fainali kwa kuitoa timu ya Congo-Brazzaville” alisema Mhe. Nape.


Aidha aliongeza kuwa kesho asubuhi atakutana na wachezaji wa timu hiyo ili kuwapa maneno ya faraja kabla ya kuanza kwa mechi na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa motisha wachezaji kwa kuwashangilia na kuwatia moyo.

Mbali na hayo Waziri Nape alitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya kadi za kieletroniki zilizozinduliwa hivi karibuni kwa kueleza kuwa kadi hizo bado hazijaanza kutumika rasmi ili zitaanza kutumiwa katika mchezo baina ya Wabunge wa Simba na Yanga pamoja na Bongo Fleva.

Timu ya Serengeti Boys inaundwa na vijana wa Kitanzania wenye umri chini ya miaka 17 ambapo katika mchezo wa kesho watahitaji ushindi na baadaye kufanya mechi ya marudiano mnamo Oktoba 2 mwaka huu nchini Congo-Brazzaville.