HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

KITUO CHA AFYA HIMO JIMBO LA VUNJO CHAPATA VIFAA TIBA VYA MILIONI 74


Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

SERIKALI imeendelea kuboresha huduma za afya katika jimbo la Vunjo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo imetoa vifaa tiba katika kituo cha Afya cha Himo vyenye dhamani ya milioni 74 pamoja na gari la kubebea wagonjwa.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Charles Kimea alisema kuwa, kutolewa kwa vifaa hivyo vitasaidia kituo hicho cha afya kutoa huduma bora kwa wananchi kwani kipo katikati ya Jimbo hilo ambapo wananchi wa kata nyingi hutegemea huduma hapo.

“Tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hata mimi nilikuwa na wasiwasi hata nilipomuomba kukipandisha hadhi kuwa kituo cha Afya haikuwa na majengo ya Wodi , maabara jengo la mama na mtoto pamoja na mochwari lakini kwa sasa serikali imeanza kuboresha kwa kuleta vifaa tiba” alisema Dkt. Kimei.

Mbunge huyo alisema kuwa, katika kampeni za mwaka 2020 walifika kituo hapo na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwine Mollel na kumweleza shida na adha zilizokuwa zikiwakumba wananchi ambapo kitua hicho kilikuwa hakituo huduma masaa 24 na kuomba kipandishwe hadhi.

Alisem kuwa, katika jimbo la Vunjo baada ya sense ya watu 2022 ilionyesha kuwa katika jimbo hilo kulingana na idadi ya watu kila kata ilistaili kuwa na kituo cha afya ambapo tatizo lilionekana zipo kata hazina maeneo ya kujengewa vituo vya afya hivyo kwa sasa wamelenga kuboresha kati zenye maeneo kwa kujenga vituo vya afya.

Aliongeza kuwa, baada ya kupata vifaa tiba hivyo kituo hicho cha Afya ktalazimika kuongezewa wataalam wa afya ambao watatumia vifaa hivyo kutolea huduma za afya.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi katika kituo hicho, Dkt. Sudi Mohamed alisema kuwa, wamepokea vifaa tiba ambavyo ni drip stendi, mashuka 60, magodoro 15, vifanda vya wagonjwa na vifaa vingine ambapo alisema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha huduma kwa wananchi .




WABUNGE WA VITI MAALUMU CCM MKOA WA DAR, WAFANYA ZIARA KUHAMASISHA WANACHAMA NA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA

Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, akizungumza na Viongozi na Wanachama wa UWT (CCM) wakati wa ziara ya wabunge hao katika Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuhamasisha wanachama juu ya uchaguzi wa Jumuiya hiyo na Uhai wa Chama. Mkutano huo ulifanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa Ndugumbi uliopo Magomeni Barafu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum CCM, Ikupa Alex. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO) 
Baadhi ya Wanachama wa CCM Kina mama wakifurahia moja ya kauli ya mgeni rasmi.
Wanachama wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Masunga, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuhutubia.
Wanachama wa CCM wakifurahi na kucheza na mgeni rasmi
Wanachama wa CCM wakifurahi na kucheza na mgeni rasmi
Wanachama wa CCM wakifurahi na kucheza na mgeni rasmi
Ilikuwa ni furaha kwenda mbele.
Wanachama wakishangilia
Mgeni rsmi Angela Kairuki akiagana na wanachama waliokuwepo ukumbini humo baada ya kumaliza mkutano huo.
Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, akizungumza jambo na mmoja wa wanachama aliyekuwa akimueleza baadhi ya Kero za mtaani kwake baada ya kumaliza kuwahutubia Viongozi na Wanachama wa UWT (CCM) wakati wa ziara ya wabunge hao katika Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuhamasisha wanachama juu ya uchaguzi wa Jumuiya hiyo na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa Ndugumbi uliopo Magomeni Barafu jijini Dar es Salaam.
Mgeni rsmi Angela Kairuki akiagana na wanachama waliokuwepo ukumbini humo baada ya kumaliza mkutano huo.

PICHA: YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA BARAZA KUU LA CHADEMA

 MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendelea CHADEMA, Freeman Mbowe akifungua mkutano huo uliofanyika Mkoani Dodoma Mei 27,2017.
 Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Vincent Mashinji akizungumza
 Meza kuu
 Mwenyekiti wa CHADEM, Freeman Mbowe akisoma taarifa za chama. 
Picha zote na Mroki Mroki.
 Wajumbe wa Baraza Kuu wakiwa katika Mkutano huo mjini Dodoma
 Wimbo wa Taifa uliimbwa
 Dua ilifanyika kabla ya kuanza mkutano huo.
 Wajumbe wakiwa mkutanoni
 Wajumbe ambao ni Wabunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Dodoma, Dk Immaculate Sware (kushoto) na Devotha Minja wa Morogoro.

Wajumbe wakifuatilia mkutano huo.

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA RODRICK MPOGOLO AMALIZA KWA KISHINDO ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA JIMBO LA UBUNGO NA KIBAMBA

Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzimuni, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali (kulia) akicheza muziki na Katibu Mwenezi wa Kinondoni, Mwinyimku Sangaraza, wakifurahia hotuba ya Naibu Katibu MKuu Bara baada ya kuwahutubia katika Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, jana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, katika Ukumbi wa CCM Manzese, wakati wa ziara yake ya kuimarisha Chama kwa kuzungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo hilo la Ubungo jijini Dar esSalaam , jana. 
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, akizungumza kutoa tathmini ya usalama wa kisiasa katika Wilaya yake mbele ya mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, aliyekuwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama katika Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, jana. 
Msanii ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa Kata ya Makurumla, Shukuru Mbundi, akitoa burudani ya kuimba mbele ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara wakati wa mkutano wa kuimarisha Chama katika Jimbo la Ubungo jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa, Mabalozi na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar Es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiwatambulisha Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa na Mabalozi wa Kata ya Manzese na kuwapa majukumu baada ya kuzungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar Es Salaam.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi (kushoto) akisebeneka na baadhi ya wanachama wa CCM Kata ya Manzese wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara , Rodrick Mpogolo, jana. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo la Kibamba, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Hoja Kata ya Salanga, jijini Dar es Salaam, jana.
Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Salanga Jimbo la Kibamba, wakiwa bize kutunza kumbukumbu ya elimu iliyokuwa ikitolewa kwao na Naibu Katibu Mkuu jana.
Baadhi ya wanachama wa CCM Kata ya Salanga wakisimama na kuimba kumpongeza Naibu Katibu Mkuu wakati wa ziara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Salanga, Euzedius Chilipwei, wakati akiwa katika ziarayake ya kuimarisha Chama Jimbo la KIbamba jana.
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akijumuika na viongozi na wanachama wa CCM kufurahi kwa pamoja kucheza muziki baada ya kumaliza kuwahutubia katika ziara yake ya kuimarisha Chama kwenye Jimbo la Kibamba Kata ya Salanga jana.

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akijumuika na viongozi na wanachama wa CCM kufurahi kwa pamoja kucheza muziki baada ya kumaliza kuwahutubia katika ziara yake ya kuimarisha Chama kwenye Jimbo la Kibamba Kata ya Salanga jana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzimuni, 
ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali (kulia) akicheza muziki na Katibu Mwenezi wa Kinondoni, Mwinyimku Sangaraza, wakifurahia hotuba ya Naibu Katibu MKuu Bara baada ya kuwahutubia katika Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, jana.

Naibu Katibu akiondoka ukumbini
Akiagana na baadhi ya viongozi