HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Ripoti ya Jonas Mkude Kutoka hospitali ya Muhimbili

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude anaendelea vizuri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako amefanyiwa vipimo na kupata matibabu kwa ujumla.

Mkude alikuwa kati ya watu sita waliopata ajali iliyotokea leo na shabiki mmoja wa Simba, Shose Fidelis amepoteza maisha.

Ajali hiyo ilitokea siku moja tu baada ya Mkude kuingoza Simba kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Kiungo huyo alifikishwa Muhimbili kwa matibabu zaidi ili kupata uhakika.

Lakini hali yake inaonekana kuimarika na imeelezwa jana alikuwa akilalama sana maumivu lakini sasa ana nafuu.

“Anaendelea vizuri, labda tuangalie kidogo kujua zaidi,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba.

MO aitaka Simba kumrudishia fedha zake, adai wamekiuka makubaliano ya Mkataba

Mdau mkubwa wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ ameiandikia klabu hiyo barua (demand note) ya kuitaka kumlipa fedha zote za mishahara alizokuwa akiwalipa wachezaji tangu mwaka jana kiasi cha shilingi bilioni 1.4 baada ya kubaini kuwa klabu hiyo imeingia mkataba na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.

Hayo yamejiri siku moja baada ya Simba kutiliana saini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa. Uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa timu, Evans Aveva, ulisaini mkataba huo wa miaka mitano na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.

MO amewaandikia Simba ‘demand note’ kwa kuwa wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe fedha kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.

Klabu hiyo ya Simba imeanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.

Barua ya Bodi ya Ligi kuhusu sakata la alama tatu kati ya Kagera Sugar na Simba SC.

Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewajibu rasmi Simba SC juu ya sakata lao la kupokwa pointi tatu za mezani walizopewa baada ya rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar wakidai kumcheza mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano.

Kwa mujibu wa barua kutoka katika Bodi ya Ligi zimesema kuwa Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano wakati akicheza mchezo dhidi ya Simba uliofanyikia uwanja wa Kaitaba, Bukoba Aprili 2 mwaka huu.

"TFF ambayo ndiyo yenye dhamana ya usimamizi wa mpira nchini na ambayo ndiyo iliyokaimu madaraka kwa TPLB kuendesha ligi kuu iliitisha kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ilichunguza kwa undani sakata hili na baada ya uchunguzi wao ambao walihoji watu mbalimbali, walituandikia kutujulisha kuwa wamebaini mchezaji Mohamed Fakhi anayelalamikiwa na Simba hakuwa na kadi 3 siku ya mchezo wa Kagera Sugara dhidi ya Simba hivyo alikuwa halali kucheza mchezo huo". Ilisema barua hiyo

Mzamiru Yassin alamba Tuzo

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, leo wamemtangaza kiungo wao Mzamiru Yassin kuwa ndiye mshindi wa Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Machi mwaka 2017, ikiwa ni mara yake ya pili kutwaa tuzo hiyo ndani ya klabu.

Kiungo huyo Tuzo yake ya kwanza alishinda mwezi Oktoba mwaka 2016 kwa kupigiwa kura na mashabiki kutokana na jitihada na kujituma kwa timu yake pindi wanapokuwa dimbani na hatimaye kuipa ushindi.

Ikumbukwe, mchakato wa kumpata mchezaji bora wa mwezi hupatikana kwa mashabiki wa Simba kuanza kupendekeza jina la mchezaji wanaomtaka kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na mwishowe huanza kupigiwa kura.

Kwa upande mwingine, leo timu ya Simba SC itashuka dimbani kuvaana na Wanalambalamba (Azam FC) katika kutafuta tiketi ya kuingia Fainali michuano ya Kombe la Shirikisho FA, utakaochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kauli ya Jerry Muro baada ya Haji Manara wa Simba kufungiwa na TFF

Muda mfupi baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya nidhamu ya TFF kutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kwa utovu wa nidhamu na kukutwa na makosa matatu.
Afisa habari wa zamani wa Yanga ambaye nae alifungiwa mwaka mmoja Jerry Muro ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika “Mtuache sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa hilo haswa kwenye mpira nadhani yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara“

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka pamoja na faini ya Tsh Milioni 9.

Kamati ya nidhamu ya TFF imetoa adhabu hiyo licha ya Haji Manara kushindwa kufika kwa madai ya kupata dharura lakini anayo nafasi ya kukata rufaa.

Simba Yaitandika Mabao 2 Yanga Uwanja wa Taifa Leo

Mashabiki wa soka wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo kushuhudia pambano la Simba na Yanga. Simba imeshinda 2-1. (Picha na Francis Dande).
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (kulia), akishangilia bao la kufutia machozi alililoifungia timu yake dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzia Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Haruna Niyonzima. Simba ilishinda 2-1. 
Askari wakiwa katika doria uwanja wa Taifa.

 Mashabiki wa Simba.
 Mashabiki wa Simba.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisalimiana na Simon Msuva.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akisalimiana na Simon Msuva.

 Mashabiki wa Simba.
 Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akimtoka beki wa Simba, Novat Lufunga.
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akimtoka beki wa Simba, Novat Lufunga.
 Mashabiki wa Simba.
Mfungaji wa bao la kwanza la Simba, Laudit Mavugo (11), akiwa amembeba Said Ndemla.


Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, akimtoka beki wa Simba, Novat Lufunga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 2-1. 
Shabiki wa Yanga akipata huduma ya kwanza baada ya kupoteza fahamu.
Beki wa Simba, Janvier Bukungu akitoa uwanjani baada ya kupewa kadi nyekundu.
Klabu ya Yanga ilianza vyema mchezo ndani ya dakika za mwanzo kabisa na kupelekea mchezaji Obrey Chirwa mwenye jezi namba 7 mgongoni kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane na mchezaji wa Simba Novat Lufunga na kupelekea Yanga kupata penati ndani ya ya dakika 4 za mchezo na kupigwa vyema na mchezaji Simon Msuva wa Yanga.

Yanga iliendelea kuongoza kwa bao hilo la kwanza huku wakiwa na moto wa kutafuta goli la pili, katika dakika ya 23 Yanga walipata kona ya kwanza ambayo ilipigwa na mchezaji Haruna Niyonzima lakini kipa wa Simba aliweza kuicheza vyema na kuondoa hatari ya Yanga kupata goli la pili ndani ya dakika za mwanzo mwanzo.

Kocha wa Simba Omug alipoona kikosi chake hakina mwenendo mzuri ndani ya dakika 27 alimtoa Luizio na kumuingiza Said Ndemla ambapo hapo kidogo mchezo kwa upande wa Simba ulibadilika na kuanza kufanya mashambulizi, huku wakijaribu

Ndani ya dakika 32 Goli kipa wa Yanga Deogratius Munishi alidaka mpira na kukaa nao kwa muda na kupeleka faulo ambayo ilipigwa na Said Ndemla wa Simba lakini Ndemla alikosa na kupoteza nafasi ya kusawazisha goli la kwanza.

Yanga iliendelea kufanya vyema na kujaribu mara kadhaa katika lango la Simba bila mafanikio, ndani ya dakika 43 Simba ilibahatika kupata faulo nyingine tena ambayo ilipigwa na mchezaji Ajib lakini mpira huo ulikwenda nje.

Mchezo uliendelea kwa kasi na mashambulio kwa timu zote mbili, na ilipofika dakika ya 47 mchezaji wa Yanga Thabani Kamusoko alitoka nje baada ya kupata majeraha na kuingia Said Juma Makapu.

Mpaka muda wa mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao moja dhidi ya Simba huku ikiwa imetawala mchezo kwa asilimia 51 na Simba ikitawala mchezo kwa asilimia 41.

Baada ya kurudi kwa kipindi cha pili timu zote mbili zilikuwa na hamasa ya mchezo na ushindi hamasa hizo zilipelekea mchezaji wa Yanga, Endrew Vicenti alipata kadi ya njano ndani ya dakika 56 mchezaji wa Simba alipigwa kadi nyekundu na kutoka nje ya uwanja na kuwaacha Simba wakiwa pungufu uwanjani.

Katika kipindi cha pili baada ya kuingia mchezaji Kichuya Simba ilibadilika na kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kuonyesha uwezo katika kucheza mpira jambo lililopelekea mchezaji Mavugo wa Simba ndani ya dakika 66 kupata goli la kwanza kwa Simba na kuweza kusawazisha na kuwa bao moja kwa moja.

Mpka dakika ya themanini ya mchezo Simba kupitia kwa mchezaji wake Shiza Ramadhan Kichuya aliiandikia Simba goli la pili dhidi ya Yanga huku timu hiyo ikiwa pungufu uwanjani.

Mpaka mpira umekwisha Simba 2-1 Yanga (Mavugo 66, Kichuya 81 : Msuva 5)

PICHA: VIONGOZI MBALIMBALI WA KISIASA WASHUHUDIA MECHI YA SIMBA NA YANGA

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga.(Picha na Francis Dande)
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 
Freeman Mbowe akiwapungia mashabiki wa soka. 
Mbowe.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto), akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga.  
 Lowassa akishuhudia pambano la Simba na Yanga. 
 Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya akizungumza na Edward Lowassa.
 Viongozi wakiwa wamesimama kuamboleza kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Yanga na timu ya taifa, Godfrey Bonny.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na msanii wa filamu, Wema Sepetu, wakati wakiingia Uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la Simba na Yanga.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na msanii wa filamu, Wema Sepetu, wakati wakiingia Uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, akiwasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 

Mapinduzi Cup Fainali leo nani kuibuka kidedea kati ya Simba au Azam FC?

Fainali za 11 za michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup zinatarajiwa kupigwa leo kwenye dimba la Amaan Visiwani Zanzibar kwa kuzikutanisha timu za Simba na Azam zote za Dar es Salaam.


Mchezo huo unaotarajiwa kuanza Saa 2:15 usiku wa leo, utakuwa ni wa pili kuzikutanisha timu hizo katika fainali ya michuano hiyo.
Awali zilikutana katika fainali ya mwaka 2012 na Azam FC ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutwaa taji lake la kwanza kati ya mawili ya Kombe la Mapinduzi, linguine likija mwaka 2013 baada ya kuifunga Tusker katika fainali.
Simba ndiyo mabingwa mara nyingi wa taji hilo, mara tatu baada ya kulitwaa katika miaka ya 2008 ikiifunga Mtibwa Sugar katika fainali, 2011 ikiwafunga mahasimu, Yanga na 2015 wakiwafunga Mtibwa Sugar.
Kocha wa Simba Joseph Omog, amepania kulitwaa taji hilo, kwa lengo la kuondoa ukame wa makombe ambayo umeikumba klabu hiyo kwa misimu minne iliyopita pasipo kubeba ubingwa wowote
Azam mara zote ilizoingia fainali ilitwaa taji hilo, wakati Simba mwaka 2012 na 2014 ilicheza mechi ya mwisho na kufungwa na kukosa Kombe hilo.
Kuelekea mchezo wa leo, kila timu iko vizuri baada ya rekodi nzuri katika mechi zilizopita, Simba wakiwatoa wapinzani wa jadi, Yanga kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 kwenye Nusu Fainali na Azam wakiitoa Taifa Jang’ombe kwa bao 1-0.
Timu zote ziliongoza makundi yao, Simba A lilikuwa na timu tano kwa pointi zake 10 na Azam B lililokuwa na timu nne kwa pointi zake saba.