HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

LEO KATIKA HISTORIA: HUYU NDIYE MWALIMU NYERERE TUNAYEMUENZI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake

Na Deogratius Temba
WAKATI taifa linaadhimisha miaka 18 ya kifo cha mwasisi wa taifa, na rais wa kwanza wa Tanzania, kizazi kinahitaji kujua huyo alikuwa mtu gani na aalianzia wapi.

Katika makala hii, tutaangalia sehemu tu ya historia ya mwalimu, nia ni kuitaka kumuezi na kujikumbusha kama huyu tunayemuenzi leo alikuwa mtu gani na jinsi alivyoishi.

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 , katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara. Alikuwa moja kati ya watoto 26 wa Mzee Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Kutokana na ujasiri na nia ya kuwa mwelewa wa kila kitu ya Nyerere, Mapadre wa Kanisa katoliki wakaona akili yake na nia yake nzuri ya kutaika kujifunza wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala nchini Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.akiwa katika Chuo cha Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia akaamua kujihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora na kuanza kufundisha katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria (St.Mary´s), Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma Shahada ya Uzamili ya historia na uchumi, kwa hatua hiyo Mwalimu alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.

Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam, (siku hizi Pugu Sekondari). Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.

Uwezo wa mwalimu uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Aliamua kujiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru.

Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Mkutano wa Baraza la udhamini (Trusteeship council) ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na Desemba 9, 1961  na Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.


Hayati Mwalimu Nyerere mnamo Februari 5, 1977, aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake.

Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipong'atuka na kumwachia nafasi rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi.

Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa makini na mfuatiliaji huku akionya katika mambo kadhaa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Baada ya kustaafu kazi ya ukuu wanchi, Nyerere alikaa muda mwingi kijijini kwake alikozaliwa Butiama akilima shamba lake la mahindi. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake inayojulikana kama “Mwalimu Nyerere Foundation, mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Mwishoni mwa maisha yake Mwalimu aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama

Mwalimu alianza kujisikia vibaya mwezi Augost mwaka 1999, akaanza kupata matibabu ya kila mara baadaye alihamishiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.

Oktoba 14, 1999 aliaga dunia katika hospitali hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu ( leukemia).

Mafanikio na kasoro
Kitendo kikubwa ambacho hakisahahuliki ambacho Mwalimu alikifanya na dunia inakumbuka ni kuchanganya ardhi za Zanzibar na Tanganyika ambapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulizaliwa rasmi na hadi leo upo.

Kujenga umoja wa kitaifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vitani dhidi Nduli Idi Amin Dada wa Uganda.

Watu walimuita mwalimu kuwa ni mwanamapinduzi wa afrika, kiongoiz wa bara nzima kutokana na nia zake za kutaka kila Mwafrika kuwa huru na kuwa na amani.

Mwalimu pia alifanikiwa kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za kusini ya Afrika kama; Zimbabwe {ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo)

Kutofanikiwa kwake
Kitu ambacho kilimuumiza mwalimu na kumfanya akose raha mara nyingi ni juu ya kutofanikiwa kwa nia yake ysa kuanzisha siasa za Kijamaa. Siasa zake za ujamaa zilishindwa baada ya mwaka 1976.

Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa na kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais baada ya uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani kwa Mwinyi aliyetawala kwa siasa za uchumi wa soko huria.

Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere alitamka katika tafrija ya kumwaga juu ya siasa yake kiuchumi “Nimefeli. Tukubali hivyo.”

Alikosolewa pia
Kutokana na hali hiyo na kufikia yeye kukubali kushindwa Mwalimu Nyerere analaumiwa kwa siasa zake za kiujamaa kuwa zilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania, Pamoja na kwamba hata leo kuna makundi ya watanzania kwa mtazamo wao yanazitamani siasa hizo.

Pia kuna makundi ya waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya uislamu na upendeleo wa elimu na madaraka kwa wakristo.

Kutangazwa mwenye Heri
Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, mchakato wa kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu ulianza mwaka 2005, na tayari kanisa hilo kwa kibali rasmi kutoka Roma makao ya Baba Mtakatifu, limeshamtangaza kuwa mwenyeheri.

Kuwa mwenyeheri ni hatua ya kwanza ya kuingia utakatifu. Wakristo wakatoliki wameanzisha sala maalumu na kufanya maombi kwa nia ya maombezi yake ili aweze kutangazwa kuwa mtakatifu.

Ibada ya kwanza ilifanyika katika kanisa kuu la Jimbo la Musoma, na kuongozwa na aliyekuwa askofu wa Jimbo hilo marehemu askofu Justine Samba.

Alikuwa mwanamichezo
Licha ya Kuwa mwalimu na mwanasiasa hususani kiongozi mkuu wan chi, pia Nyerere alikuwa mwanamichezo, aliazznisha mchezo wa Bao, akiwa Butiama alicheza bao nyumbgani kwake na majirani zake, wakati mwingine alipotembelewa na wafuasi wake wa kisiasa alikuwa akishiriki nao kucheza bao.

Kutokana na maisha yake aliyoyaishi ambayo yalijaa uvumilivu, unyenyekevu na uadilifu bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini hasa kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.

Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.

Taifa linamkumbuka kwa hayo na mengi ambayo aliyafanya, ameacha machapisho mengi ambayo pia yamekuwa hazina ya maarifa kwa watanzania.

ZITAMBUE DALILI KUMI NA TANO (15) ZA MAPENZI KUNYAUKA

Wapenzi wengi ambao wamefikia hatua ya kuachana wameshindwa katika vipimo vya kitalaamu kuthibitisha ubaya waliokoseana, ambao unaweza kubeba uamuzi huo mzito wa kuvunja ahadi zao za kimapenzi na hata ndoa.
Kwa mujibu wa watalaam wa masuala ya ndoa na mapenzi inaelezwa kwamba wapenzi wanaoachana huwa hawana sababu za msingi, hii inatokana na ukweli kwamba wanaoachana hawafahamu kiini kilichowatenganisha katika makubaliano muhimu na ya kwanza kabisa ulimwengu ya watu kufikia hatua ya kupeana utu wao.
Inasemwa hivyo kwa sababu ukilinganisha matatizo yanayotenganisha watu hayabebi hoja zinazokubalika na wapenzi wote. Kwa mfano kama wapenzi watasema wameachana kwa sababu wamefunaniana na wakadhani hiyo ni sababu wanakuwa wanaudanganya zaidi umma kwa maana kuna wanaofumaniana, wanaodhalilishana, wanaotukanana, wasioheshimiana kabisa, lakini bado wanadumu katika ndoa zao bila kuachana.
Kwa ulinganifu huo, wachunguzi wa mambo ya ndoa wanasema, kuachana si zao linaloota na kukua kwa siku moja, bali ni migogoro isiyoshughulikiwa kwa muda mrefu ambayo huwaachanisha wanandoa taratibu bila wao kujua.
Kwa maana hiyo wanaoachana au watakaoachana wanatakiwa kufahamu kuwa safari yao ya talaka haianzi na kumalizika kwa siku moja, isipokuwa hufikia katika hitimisho baada ya kuwepo katika mwendo kwa muda mrefu, ambapo dalili zake huwa hizi zifuatazo:

1. Ikiwa mmeoana na baadaye mkaanza kuonana ni watu msiohitajiana sana katika maisha. (mapenzi kuchuja).
Kila mtu anafahamu kuwa wakati wa uchumba mapenzi huwa moto moto lakini baada ya kuoana hujitokeza hali ya kuanza kuzoea. Hii inatokana na ukaribu ambao mwanzo haukuwepo au kusitishwa kwa machombezo yaliyokuwa yakiboresha uhusiano. Kwa mfano wapenzi wengi wanapokuwa kwenye uchumba hufanyiana mambo mengi yakiwemo ya kutumiana zawadi na kadi au kutoka pamoja kwa matembezi, lakini wakioana hujikuta hawafanyiani hayo, jambo ambalo huathiri mapenzi yao.
Uchuchuzi unaonyesha kuwa wapenzi walio kwenye uchumba wanapokuwa pamoja hutumia muda mwingi sana kuongea kwa simu, kutumiana meseji, kuzungumza tofauti na mume na mke. Ukitaka kuthibitisha keti barabarani ukiona mwanaume na mwanamke wamo ndani ya gari hawaishi kucheka na kuzungumza wafuatilie utakuta mwisho wa safari yao wanaagana kila mmoja anakwenda kwake (ina maana si mume na mke hao). Ni nadra sana kuwakuta wanaume wakiwa pamoja na familia zao wakifurahi, jambo ambalo hupunguza upendo na kuleta mazoea na hisia za kutohitajiana sana. Hili halifai likiwepo ni ishara kuwa mapenzi yanakaribia kunyauka.

2. Mkiwa hamsameheani na kusahau mnapokoseana. 
Si watu wengi ambao wako tayari kusamehe na kusahau makosa. Wapenzi wa dunia ya leo wakisema nimekusamehe haina maana wamefuta kosa bali huliweka kando na kulikumbushia wakati mwingine. ‘Hili ni kosa la tatu tarehe fulani ulinifanyia hivi, wiki iliyopita na jana ulinijibu hivi hivi sasa leo siwezi kukuvumilia”
Kauli kama hizi hutoka kwenye vivywa wa watu ambao hawako tayari kusamehe, kosa la mwaka juzi litakumbushwa tena na tena na kuzidi kuchochea ugomvi hata uliokuwa mdogo na kuoneka mkubwa kwa sababu tu umehusishwa na makosa yaliyopita. Inashauriwa kuwa uhai wa mapenzi lazima uambatane na kusameheana kama wanadamu na kusahau makosa. Hili lisipofanyika ni rahisi kuua penzi na kuwafanya watu kuachana. Ni vema kila mmoja wetu akajichunguza tabia yake na kuacha kukumbusha makosa yaliyopita.

3. Msipokubali kuwekeana mipaka ya kiutawala.
Kuna suala linatambulishwa sana siku hizi na wanaharakati, linaitwa usawa wa kijinsia, jambo hili limekuwa likichangia sana migogoro ya ndoa hasa baada ya kutumiwa vibaya na wahusika. Hakuna ubishi mila za kiafrika zinaongozwa na mfumo dume, kuubadili mfumo huu kwa haraka kumekuwa kukiharibu uhusiano mwingi wa kimapenzi kutokana na ukweli kwamba ni wanaume wachache sana ambo wako tayari kuishi na wanawake wanaovutana nao kimamlaka.
Hivyo ili kunusuru hili lisiwe kikwazo katika mapenzi tunashauri kila mwanandoa kuheshimu mipaka yake na kujali zaidi utu na si usawa kama inavyotambulishwa (haya ni mawazo yangu). Watu wanaojali utu katika familia watakuwa tayari kuwapa heshima wanaoishi nao kwa kusikiliza mawazo yao na kutokutumia nguvu kuwakandamiza wengine. Ni vema mwanamke akachukua nafasi yake kwa mumewe na mume naye akamuheshimu mke kwa utu wake.

4. Msipozungumzia vikwazo vya maisha.
Matarajio ya watu wengi wanapokuingia katika uhusiano wa kimapenzi huwa ni kupata faraja, ni wachache kati yao hufikiria kukutana na vikwazo vya kimaisha. Tafiti zinaonyesha kuwa wakati mtu anapotafuta mpenzi huamini toka moyoni kuwa akiwa na waridi wake matatizo ya upweke, kukosa msaada wa hili na lile yatakwisha lakini baadaye anakuja kubaini kuwa aliyokusudia kuyapata hayapati tena na hivyo kujuta kwa kauli kama hizi. “Kama ningejua kama mwanaume mwenyewe yuko hivi nisingekubali kuolewa.”
Kauli kama hizi mara nyingi hutokea kwa watu ambao hawazungumzii matatizo na vikwazo wanavyokutana navyo katika mapenzi na kuviondoa. Kama mpenzi wako ana matatizo unasubiri nini kuyatafutia ufumbuzi au kama maisha hayaendi sawa ukimya wa nini kwa mwenza wako, kaeni chini muambizane kuwa mnaupungufu wa fedha na dhiki kadhaa wa kadhaa, ili kama kutatokea kukosa mahitaji muhimu liwe ni jambo linaloeleweka na wote kuwa linatokana na kipato kushuka. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wengi wanapokwama kiuchumi hupunguza matumizi kimya kimya jambo ambalo huwafanya wanawake wengi kubaki wakitumikia zana potofu kuwa huenda wananyimwa baada ya kuwepo kwa nyumba ndogo.

5. Msipokuwa na mipango ya pamoja na uwazi wa matumizi ya pesa.
Nina ushahidi wa kutosha juu ya kuwepo kwa wapenzi hasa wenye kipato kutokuwa wawazi katika mipango yao ya kimaisha na matumizi yao pesa. Natambua baada ya kufanya uchunguzi wangu kuwa pesa za baadhi ya wanawake huwa hazina matumizi ya wazi, badala yake wanaume hubanwa kwa kisingizio kuwa wao ndiyo wana wajibu wa kutunza familia.
Hali hii imekuwa ikileta migogoro mingi sana kwenye familia na kushusha upendo kwa vile upande unaohudumia familia hapa haijalishi mume au mke huwa unajikuta ukikereka kwa kukosa msaada wa upande wa pili na hivyo kuondoa mapenzi ya kweli. Kama hilo halitoshi vijana wengi wa kiume siku hizi wamejikuta wakiahirisha mapenzi yao kwa wasichana baada ya kukosa ushirikiano wa kimapato na matumizi yake.
“Ninashida ya kuonana na wewe mpenzi wangu, vipi nikufuate kazini?” Jibu linakuwa “Hapana niko bize sana leo.” Inawezekana kabisa mtu akawa hayuko bize lakini kwa sababu anaogopa kukamuliwa kipato na yeye mambo yake hayako sawa anaamua kukacha ahadi. Lakini ukiwepo ushirikiano wa kimatumizi husaidia kudumisha mapenzi.
Inashauriwa kwamba kama wapenzi wote wana kazi na wanapokea mishahara ni vema vipato vyao vyote vikatumika katika kutunza na kuendeleza familia. Tabia ya mwanamke kumtegemea mwanamume kimatumizi huku yeye akitumia pesa zake kwa manunuzi ya vipodozi na nguo au kufanyia mambo yake kwa siri haijengi badala yake inanyausha mapenzi kama siyo kuyaua kabisa.

6. Mkiacha kujaliana na kupeana haki katika tendo la ndoa.
Tendo la ndoa ni muhimu kwa wanandoa kwa vile linahusika na hisia za mwili. Matatizo mengi ya usaliti kwa mujibu wa uchunguzi, yanatokana na wapenzi kutotoshelezana wakati wa tendo la ndoa. Kwa kutokutambua madhara au kwa uzembe, wapenzi wengi wamekuwa wakiacha kutimiziana tendo hilo bila kuwepo kwa sababu za msingi. “Mimi nimechoka siwezi kufanya mapenzi.”
Inawezekana kweli mtu akawa kachoka sawa na kauli hiyo lakini sababu hiyo haiwezi kumfanya mwenza akazimaliza hisia zake, isipokuwa kwa kutafuta njia mbadala zikiwepo za usaliti. Sambamba na hilo wapenzi wengi wamenyausha mapenzi yao kwa kutokuwa wabunifu katika uwanja wa sita kwa sita kwa kutokujituma, kutobuni staili mpya, kutochombeza na kutohamasisha kwa chochote na kibaya zaidi kutokuwepo kwa usafi wa miili yao.
Katika kipindi cha maisha yangu ya ushauri wa masuala ya saikolojia, maisha na mapenzi nimekuwa nikikutana na wanaume wengi wanaolalamika kuwa wana upungufu wa nguvu za kiume. Lakini wengi kati ya hao ambao mamia yao nimeshawasaidia walijikuta wakipungukiwa nguvu zao kwa sababu za kisaikolojia zilizochochewa pia na udhaifu wa wenza wao. Kama utakuwa na mtu kwa mfano, ambaye mtakutana naye chumba kile kile, eneo lile lile, staili zile zile, kwa miaka mitano mfululizo bila shaka hali ya kukinaishwa itakuwepo na hivyo mapenzi kunyauka. Katika hili ni vema kujifunza zaidi namna ya kutoshelezana katika tendo la ndoa.

7. Mkibeba fikra binafsi kwa kila mtu kutaka mafanikio yake.
Maisha ya wapenzi wengi yamekuwa yakipoteza maana kiasi cha kufikia kuchuja kutokana na wapenzi wenyewe kuwa na mawazo ya ubinafsi. Utakuta watu wameoana lakini kila mmoja anakabili changamoto za maisha peke yake, hali ambayo humfanya atumie nguvu kubwa kutafuta ushindi wa matatizo yake.
Mantiki ya maisha ya ndoa ni kusaidiana. ‘Mungu alimwambia Adamu kuwa atampatia msaidizi wa kufanana naye ambaye ni mwanamke aliyeitwa Hawa.’ Upo pia msemo usemao ‘Kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi’ Ni wajibu wa wanandoa kuhakikisha kuwa maisha yao yanakuwa ya nyuzi mbili ili yasikatike upesi. Lakini ikiwa kila mtu anajenga nyumba yake, anafanya biashara zake, ana mipango yake binafsi ujue mwisho mbaya wa mapenzi umesogea.

8. Mkiwa watu wa kutoa siri zenu nje.
Upo udanyanyifu mwingi wa kimawazo miongoni mwa wapenzi wengi kiasi cha kudhani kuwa kumwambia rafiki au ‘shoga’ masuala ya ndani ya ndoa ni kutafuta suluhu ya matatizo. Hii si sahihi kwa vile upo ushahidi mkubwa juu ya wapenzi wengi ambao walijikuta katika wakati mgumu baada ya kutoa siri zao nje. Ifahamike kuwa ndoa imara ni ile inayoheshimika katika jamii, na heshima hiyo haiwezi kuwepo kama wanandoa hawatakuwa makini katika kutunza siri za mapenzi yao.
Haipendezi kwa mwanamke/ mwanaume kwenda kijiweni na kuanza kuanika mambo ya ndani kwa mfano. ‘Yaani leo mume wangu hakuacha kitu chochote ndani sijui itakuwaje. ‘Sema wanawake wote lakini si mke wangu, ana kasoro nyingi sana.’
Kauli kama hizi na nyingine ambazo zinatoa nje udhaifu wa maisha yenu hazifai, kwani katika kila ndoa kuna udhaifu mwingi ukiwepo ukimya ina maana wahusika wanaweka udhaifu wao kifuani kwa maslahi ya maisha yao. Na wewe uwe hivyo kwa kutunza siri za mumeo.mkeo.

9. Msipokuwa wawazi katika kuzungumzia upungufu wa kibinadamu mlionao na kusaidiana.
Wapenzi wasomaji wangu, hakuna mwanadamu aliyekamili kwa asilimia mia moja. Ukimuona hodari wa hili ni dhaifu wa lile, kinachotakiwa ni kusaidiana katika kufikia ukamilifu. Faraja inayopatikana katika upungufu wa mwanadamu hasa usiokuwa wa kimaumbile ni kuwepo kwa utatuzi wake. Kuna wapenzi wengi wamefikia kuachana kwa kasoro ndogo ndogo kama za kutojua mapenzi, au hata uchafu wa mwili ambao kama wangekaa na kujadiliana pamoja wangepata ufumbuzi wa tatizo.
Inashauriwa kuwa kunapokuwepo upungufu wowote wa kati ya mwanaume na mwanamke ni wajibu wa wapenzi wenyewe kukaa chini na kuelezana wazi na kushirikiana katika kupata ufumbuzi. Unashindwa nini kuwambia mpenzi wako kuwa hakutoshelezi katika tendo la ndoa, ana harufu mbaya mwilini, mchafu, hajui mapenzi na mambo kama hayo! Kikubwa katika hili ni kujua namna ya kuwasilisha ujumbe, maana kuna wengine hawana lugha nzuri za mawasiliano “Yaani mke wangu unanuka sana mimi nakerwa sana” Ukisema hivi utamfanya mwenzako aone kama unamnyanyapaa. Tumia lugha nyepesi itakayosaidia kumaliza tatizo msikae kimya bila kuzungumzia upungufu wenu mtajikuta mnaachana.

10. Mkiendekeza nguvu katika kutwaa madaraka ndani ya familia.
Kuna baadhi ya familia kila mmoja ni mtemi hakuna diplomasia katika kutatua migogoro. Utakuta mwanamke ni mbogo na mwanaume naye ni simba, basi shughuli inakuwa nzito. Ndoa inakuwa uwanja wa ndodi kila siku kutoana manundo. Hakuna mapenzi ya namna hiyo! Kanuni za mapenzi bora zinakataza wapenzi kutumia nguvu kutwaa madaraka au haki ndani ya familia. Inawezekana kabisa wewe kama mke/ mume uko na haki katika jambo fulani lakini haki hiyo haikupi fursa ya kutumia nguvu nguvu kuipata.
Kinachotakiwa katika mapenzi ni kuheshimiana, kwani katika hali ya kawaida utumiaji wa nguvu katika kudai haki ndani ya familia ni moja kati ya mambo yaliyoshindwa katika historia kuleta maelewano. Kama unadhani naongopa keti chini ujitathmini tangu umeanza kumchunga mumeo/mkeo na kumbana kwa ngumi umepata mafanikio gani, ameacha tabia yake au ndo anazidi? Umwamba haufai kutumika katika maisha ya ndoa kwa mtu yoyote awe mwanaume au mwanamke.

11. Mkiwa watu msioheshimiana mbele za watu na kupenda zaidi kusema kuliko kusikiliza.
Nimeshuhudia wapenzi wengi ambao hawajui umuhimu wa kuheshimiana mbele za watu. Utakuta mwanamke/mwanaume akimwaibisha mwenzake mbele za watu kwa kumfokea, kumwita jina baya, kumtusi, kumtoa kasoro na hata kumdhalilisha. Kitendo hiki ni kibaya na maumivu yake hudumu kwa muda mrefu akilini mwa mtendewa.
Inashauriwa kwamba wapenzi wanapokuwa mbele za watu wachunge ndimi zao na wawe watu wanaopenda zaidi kusikiliza kuliko kunena. Inaelezwa, penye wingi wa maneno hapakosi kuwa na uovu. Kuna wanawake wakianza kuwatusi waume zao mpaka nyumba ya 50 wanasikia au wakati mwingine hutoka nje na kumwaga mitusi kana kwamba wameambiwa watapewa tuzo. Hiyo si heshima na hajawahi mtu kuheshimika kwenye jamii kwa uhodari wa kutukana watu.

12. Msipokuwa tayari kukubali kosa na kujirekebisha.
Dalili nyingine ya mapenzi kunyauka ni kwa wapenzi wenyewe kuwa na tabia ya kutokukubali makosa na kujirekebisha. Utakuta mwanaume/,mwanamke ameshaambiwa mara nyingi na mwenza wake juu ya tabia zake na pengine hata marafiki zake wamemtahadharisha lakini habadiliki, kila siku anarudia makosa yale yale ambayo yanamuumiza mpenzi wake. Huu ni mwenendo mbaya, ubinadamu unamtaka kila mtu kuwa tayari kukiri kosa na kujirekebisa

13. Msipokuwa watu wa kuitafuta furaha pale inapokosekana.
Wakati mwingine harakati za maisha huleta huzuni, kwa mfano, kama wanandoa watafiwa, kuuguza, kufukuzwa kazi, kupoteza mali kwa kuibiwa na matukio kama hayo huondoa furaha. Hapa inashauriliwa kwamba endapo furaha itaondoka kwa sababu yoyote wanandoa wanajukumu la kuitafuta. Hapa namaanisha kutiana moyo na kuwezeshana kusonga mbele wakiamini kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Kuacha huzuni itawale nyumba yenu kwa muda mrefu hupunguza mapenzi.

14. Msipozingatia kuombana msamaha bila kujali nani mwenye kosa.
Kuombana msamaha ni jambo la lazima kabisa katika ndoa, na busara inamtaka mwenza kuwa tayari kuomba masamaha hata kama anaona kabisa hakuna kosa la msingi alilolifanya mbele ya mwenzake. Kung’ang’ania kutaka haki kipindi cha kuzozana ni njia ya kuelekea kukosana zaidi na hatimaye kuachana. “Nakuomba unisamehe mke/mume wangu, najua nimekuudhi.” Baada ya kutoa kauli hiyo na mzozo kupoa mhusika anaweza kufafanua kilichotokea na hapo anaweza kueleweka zaidi kuliko kipindi ambacho mpenzi wake anakuwa na hasira.

15. Msipokuwa tayari kukumbushana wajibu na mwenendo wenu
“Atajijua mwenyewe siku yakimkuta ya kumkuta huko ndo atafahamu” “Mimi nimechoka nimebaki namwangalia tu.” Kubaki unamwangalia mpenzi wako anaharibikiwa si uamuzi wa busara kwani mwisho wa siku kama ni aibu itakufikia na wewe pia. Ukimuona mwenzako anakwenda nje ya mstari wa jamii mrejeshe na kuzidi kumkumbusha kila siku wajibu wake kama baba au mama wa familia, hii inasaidia kumuweka sawa mahali anapokosea.
Mpaka hapa tutakuwa tumefikia tamati ya somo letu, naamini watu wengi wamejifunza vya kutosha. Shukrani za pekee ziwaendee watu wote waliokuwa pamoja nami tangu mwanzo wa somo hili

Zitambue Njia Nne za Kulinogesha Penzi Lako

Kupitia safu hii uipendayo, leo ninakupa njia nne zitakazolifanya penzi lako liendelee kunoga, hata kama litakuwa limeanza kufubaa utaliamsha upya.
Wengi wamekuwa hawaelewi mambo mengi kuhusu uhusiano ndiyo maana huishia kulalamika kwamba wanapenda sana lakini mwisho wa siku huishia kutendwa.
Hakuna mtu ambaye hahitaji faraja, kila aliyekuwa na mpenzi wake anahitaji kuwa na furaha. Hakuna mtu ambaye anaingia kwenye mapenzi ili apate msongo wa mawazo, kila mtu anayediriki kuutoa moyo wake, kitu cha kwanza anachokitarajia ni faraja kisha furaha.
Ipo hivyo! Watu wengi wanakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wakiwa na matumaini kwamba hao waliokuwanao inawezekana watakuwa wapenzi wa maisha yao yote. Pasipo kujua, wakati mwingine kuna makosa hufanyika, mtu hajui afanye nini ili penzi alilonalo kwa mpenzi wake linoge, hajui ni njia zipi zitamfanya kupendwa kila siku.

Leo nitakutajia njia chache ambazo kama utazifanya, nakuhakikishia penzi lenu litashamiri zaidi ya lilivyo hivi sasa.


1. Mpe Uhuru Kwanza
Kila mtu anapenda kuwa huru, kuachwa afanye mambo yake anayoyapenda. Hakuna mtu anayependa kuingiliwa, hasa kwenye masuala ya kutumia simu yake. Kama kweli unahitaji penzi linoge, usitake kuingilia mambo yake hasa katika matumizi ya simu, unachotakiwa ni kumwambia muda ambao hupendi kuona akizungumza na simu na si kwamba kila unapoona simu yake inaita, unaichukua kwa nguvu.
Mapenzi hayapo hivyo, mpe uhuru mwenza wako. Haimaanishi mtu kama hajatulia basi kuchukua simu muda wote inapoita ndiyo kutamfanya kutulia, hapana, bali kwa kufanya hivyo utampa mbinu nyingine ya kuweza kupambana nawe. Unachotakiwa ni kumfanya kuwa huru, usimuingilie.


2. Chukua Muda Wako Kumtoa ‘Out’
Wengi hukosea hapa, huwa hawapendi kwenda matembezi na wapenzi wao. Wengine hujifanya wapo bize, hata ukimwambia Jumamosi nataka tutoke out atakwambia anataka kufanya hili na lile.

Rafiki yangu, kila mtu anahitaji kuwa karibu na mpenzi wake, hakuna anayependa kuwa na mpenzi ambaye muda wote yupo bize tu. Mchukue, nenda naye sehemu. Kutoka mitoko ya mara kwa mara itawafanya muwe karibu zaidi, itawafanya muda wote mzidi kupendana, ila kama utajifanya upo bize, jua kuna mtu ataitumia nafasi hiyo kutoka na umpendaye.



3. Pendelea Kufanya Utani
Hakuna mtu anayempenda mpenzi ambaye yupo siriazi saa ishirini na nne. Pata muda wa kukaa na kutaniana naye. Mchombeze kwa vineno vya utani, mpetipeti, mlaze kitandani na uanze kupiganapigana naye vibao vya kimahaba hata kwa kutumia mito ya kulalia.
Unapokuwa siriazi kila wakati inakuwa ni vigumu mwenzako kulifaidi penzi, pendelea kutabasamu inapobidi kila unapokuwa na mpenzi wako, siyo kila atakachokwambia wewe uso wako umekunja ndita kiasi kwamba ataonekana kukuogopa na kumtafuta mtu mwingine ambaye atahitaji kuliona tabasamu lake, atahitaji kuona akifanyiwa utani wa mahaba nk.


4. Hebu Msifiesifie Basi
Wengi wanaogopa kuwasifia wapenzi wao, hawajui kama kila mtu duniani anapenda kusifiwa. Mpenzi wako anapovaa nguo nzuri zilizomtoa, usikae kimya, mwambie amependeza kwani hilo litamfanya kufurahi sana. Kama utakuwa na mpenzi halafu kila siku humsifii hata akifanya kitu gani, jua kwamba atajisikia vibaya, wakati mwingine atahisi hayupo sawa kwa kuwa tu hujawahi kumsifia.
Unapomsifia mpenzi wako kunamfanya kuongeza umakini katika kuvaa kwake, kununua manukato na hata jinsi atakavyosuka au kunyoa atafanya kwa ubora wa hali ya juu kwa kuwa anajua utamsifia.

WAPALESTINA WAADHIMISHA MIAKA 69 YA NAKBA

 Tarehe 15 ya mwezi huu wa Mei kila mwaka, Wapalestina kote duniani wanaadhimisha kumbukumbu ya kutokea janga(NAKBA) kubwa la kibinadamu la kukaliwa kwa mabavu ardhi yao, huku wenyewe wakifukuzwa na kulazimika kuyaacha makazi yao, kulikofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israeli, ambapo mwaka huu wa 2017 ni maadhimisho ya miaka 69, tangu kutokea kwa janga hilo. Siku hii inajulikana kama siku ya Nakba au siku ya nakama,janga,maafa na msiba mkubwa kwa wananchi wa Palestina wasio na hatia.

Ripoti iliyotolewa na Kamati Kuu ya Kitaifa ya kumbukumbu za Siku ya Nakba imeeleza kuwa, haki ya kurejea wakimbizi wa Kipalestina katika ardhi yao ya asili haipingiki wala haina mbadala. Aidha tarehe 15 Mei kila mwaka, Wapalestina duniani kote hufanya maandamano kukumbuka Siku ya Nakba, ambayo inakumbusha masaibu ya kufukuzwa kwa nguvu kwa maelfu ya Wapalestina kutoka katika ardhi yao ya asili, kulikofanywa na vikosi hivyo  dhalimu vya Wazayuni wa Israeli mwaka 1948. Wazayuni pia walifuta ramani za miji na vijiji zaidi ya 500 vya Wapalestina na kusababisha Wapalestina wanaokadiriwa mamilioni kuwa wakimbizi kwa karne kadhaa kwenye nchi jirani za kiarabu.

SIKU YA NAKBA:
Hivyo basi, Mei 15 kila mwaka Wapalestina duniani kote huadhimisha siku hiyo ya Nakba, inayowakumbusha dhuluma ya kihistoria iliyowapata,ambayo masaibu yake yanaendelea kuwanyima raha hadi leo hii. Waliihama ardhi yao kilazima, ikiwa ni matokeo ya uhalifu wa wanamgambo dhalimu wa Israeli dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina mwaka 1948.
 Kufukuzwa huko kwa Wapalestina toka katika ardhi yao ya asili, kumekuwa kunajulikana kama Al Nakba (Maafa), huku zaidi ya Wapalestina laki nane (800,000) wakiwemo wanaume, wanawake, na watoto, wakilazimishwa kuyahama makazi yao kufuatia tamko la kuundwa kwa Israeli mwaka 1948,litokanalo na kile kilichojulikana kama harakati za kizayuni.
Wapalestina walikimbilia katika maeneo mengine ya Palestina ambayo yalibakia katika udhibiti wa ndugu zao  wa kipalestina na Waarabu au nchi jirani za Kiarabu, huku wakiacha kila kitu zikiwemo mali, biashara, na akiba yao ya vyakula zikiwemo nafaka. Mara baada ya kufukuzwa kwa Wapalestina kutoka katika nchi yao, mfululizo wa sheria za kidhalimu zilipitishwa na serikali ya Israeli, zinazolenga kuzuia wakimbizi wa Kipalestina kutoka na kurudi majumbani mwao. 
Kufukuzwa kwa wapalestina kutoka katika ardhi yao ya asili,haikuwa tu ni dhuluma bali kumelenga pia kuwafutia uwepo wao,hadhi na kuwaondoa kabisa katika historia. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 1948, theluthi mbili ya Wapalestina ilikuwa imefukuzwa kutoka katika nchi yao, kufuatia shambulio la kijeshi la Israeli.
 Hali iliyopelekea kukimbia mauaji yaliyofanywa na wanamgambo wa kiyahudi katika maeneo mbalimbali ya Palestina, kama vile “Deir Yassin” na “Tantura”. Kiuhalisia vikosi hivyo vya kiyahudi vilipunguza idadi ya wapalestina kwa kuteketeza vijiji na miji zaidi ya mia tano (500).
Hivyo, kila mwaka ifikapo siku ya Nakba, Wapalestina hukumbuka na kuomboleza vitendo hivyo vya ugaidi wa Israeli uliotekelezwa dhidi ya Wapalestina wasio na hatia zaidi ya laki nane (800,000). Idadi hiyo kubwa, wengi wao hawakuwa na uwezo wa kujitetea, kwani ni wale waliotokana na familia za wakulima wa kawaida wasio na silaha, ambao walikuwa wamefukuzwa kwa nguvu na kulazimika kuihama ardhi yao ya asili.
 Serikali ya Israeli iliyoingia madarakani hivi karibuni, imepokonya ardhi ya wakimbizi wa kipalestina,bila kuheshimu haki zao au tamaa na matakwa yao ya kurudi nyumbani katika ardhi yao ya asili. Viongozi wa kiyahudi wametamka waziwazi kwamba, kuna haja ya kutumia nguvu za kijeshi ili kuwafukuza Wapalestina wengi vyovyote iwezekanavyo.
Kulikuwepo na mpango mkakati maalumu uliowekwa na wanamgambo wa kiyahudi ujulikanao kama “Haganah Militia’s Plan Dalet”,uliolenga kutekeleza uhalifu huo wa kuwafukuza kwa nguvu wapalestina kutoka katika ardhi yao,kwa mujibu wa kauli ya Waziri Mkuu wa kwanza wa Israeli David Ben Gurion. "Ni lazima kutumia njia mbalimbali zikiwemo ugaidi, mauaji, vitisho, kuwaondoa kwa ngvu na kukata huduma zote za kijamii ili kuwafukuzia mjini Galilaya, ambao ni mji wa mbali wa Kiarabu."
Mahali pengine duniani hali hii huchukuliwa kuwa ni uvamizi wa kutumia silaha, kufuatia kuporwa kwa ardhi ya wapalestina wasio na hatia,kwa kutumia silaha mbalimbali zikiwemo bunduki na mabomu dhidi ya familia  zisizo na silaha.
Kuna wakimbizi wa kipalestina zaidi ya milioni saba (7) katika nchi jirani za Kiarabu na duniani kote hadi kufikia leo hii, ni ukweli usiopingika kwamba ndio idadi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani iliyobaki. Hadhi ya wakimbizi na haki zao mbalimbali ikiwemo haki ya kurudi nyumbani katika ardhi yao ya asili, ni miongoni mwa masuala muhimu katika mzozo unaoendelea kati ya Israeli na Palestina.
Hii ni kwa sababu wakimbizi wote wanafurahia haki ya kutambuliwa taifa lao kimataifa, kwa kurejea katika ardhi yao ya asili ambayo wao walilazimishwa kuihama na kukimbilia nje. Haki hii imekubalika waziwazi kupitia mikataba ya amani ya hivi karibuni katika nchi mbalimbali kama vile Cambodia, Rwanda, Croatia, Bosnia-Herzegovina, Guatemala, Ireland ya Kaskazini, Kosovo, Sierra Leone, Burundi, na Sudan.
Umoja wa Mataifa unatilia mkazo haki hii ya Wapalestina, kupitia Azimio lake namba 194 la mwaka 1948, lakini Israeli kwa kukwepa mkono wa sheria haikukubali kurudi kwa Wapalestina katika ardhi yao ya asili, wakati Mayahudi kutoka mahali popote duniani walipo wanaweza kurudi na kuishi nchini Israeli. Nakba ni maafa makubwa zaidi kuliko uhalifu wa aina yake wa mwaka  1948, ni janga la kihistoria ambalo bado wapalestina wanalichukulia kuwa ni ukweli na uhalisia, si tu kukumbuka tukio hilo ili kuadhimisha kilichotokea miaka 69 iliyopita, bali ni maafa yanayoendelea kuiharibu Palestina na Wapalestina wenyewe hadi leo.
Hivyo basi, siku ya Mei 15 kila mwaka,huwa si tu ya maadhimisho ya miaka 69 au zaidi ya maafa ya Nakba, bali ni mwaka mmoja zaidi wa kudumu kwa ukatili wake. Historia ya maafa ya Nakba haikuwa ni historia tu ya siku na miaka iliyopita, bali ni historia ya sasa tunayoishi nayo.
Nakba imesababisha mamilioni ya wakimbizi wa kipalestina hadi leo kusambaa duniani kote, huku wengi wao wakiwa ni wakimbizi kwa zaidi ya mara mbili au tatu, kutokana na uvamizi wa makazi yao na ardhi yao unaoendelea nchini Palestina. Uvamizi huu wa kidhalimu na uhalifu huu, unaendelea kufanywa na Israeli kinyume na sheria, ukiwemo upanuzi wa mara kwa mara wa makazi haramu ya walowezi,kupora ardhi ya Wapalestina na kuharibu mali na maisha yao.
Hivyo basi,Wapalestina popote duniani, jumuiya ya kimataifa na wale wote wapenda haki na amani duniani, huadhimisha siku hii ya Mei 15, ikiwa sio tu siku ya maombolezo na maadhimisho ya yale yaliyotokea mwaka 1948, bali pia ni siku ya kuungana na wananchi wa Palestina katika kudai uhuru wao, haki zao na kumaliza uvamizi wa kimabavu na kidhalimu katika ardhi yao ya Palestina.

SUMU YA PENZI SEHEMU YA THEMANINI NA NANE(88)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“unataka kufanya nini mke wangu.. hapana tafadhali usifanye hivyo..” alianza kulia mume wangu akitamani kuja kunitoa, lakini Yule kaka alikuwa makini kushikilia bastola yake akimuoneshea mume wangu akAtulia kimya kama ananyolewa.
“Yule mchumba wa jamaa alionekana kulia na kutotaka hata kuangalia nilichokua nikikifanya.
“Basi nikaanza kumchezea aliposimama vizuri nikamuinamia na kuushukilia msumeno wake kwa nyuma na kuuchomeka ili aanze kuranda mbao.
“Sikujali nikamtazama mume wangu akionekana kuumia kiasi cha mwisho, nikawa najiuliza kama yeye alichepuka na kunisaliti mimi, sasa nini kilichomuuma?
Potelea mbali acha nimuadhibu akasimulie kwa mama yake, shangazi yake, hadi kwa babu yake. Lakini kwa muda huo nilitaka kumuonesha kuwa hata mimi siyo mjinga, naweza pia kufanya anachokifanya.
Basi Yule kaka alipomaliza kukojoa, nikajichomoa na kupandisha chupi yangu. Kisha nikabeba vyangu na kuaga.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

MWISHO

SUMU YA PENZI SEHEMU YA THEMANINI NA SABA (87)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kiukweli, nilikuwa nimestaajabu mno, na sasa ndiyo nikagundua kwanini nilikuwa na wasiwasi na mume wa Gululi kurudiana na Gululi harakaharaka vile. 
Ilivyoonesha kuwa alitaka kuwachanganya Gululi na kile kibinti cha chuo, sasa amefumaniwa. Na kwa kuwa nilikuwa mbali sikuweza kwenda cha zaidi nilimshauri tu Gululi cha kufanya.
“Gululi huyo mwanaume amekuelekeza kuwa amemfumania mumeo gesti gani?” nilihoji.
“ndiyo ni palepale kazini kwa mume wangu..” alisema Gululi.
“Gululi naomba ujikaze uende, ukajionee isije kuwa anataka kukufitinisha..” nilisema Gululi akaitikia kuwa anaenda muda huohuo. Akakata simu.
Muda wote nikawa nampigia hakuwa akipokea, nikazidi kuwa na wasiwasi. Baadaye usiku akanipigia simu mwenyewe sasa akionekana amepoa mno kuliko mwanzoni.
“Gululi nini kinachoendelea.!” Nilihoji.
“Mary nimefanya kitu ambacho, sitakijutia maisha yangu yote, najua umefanya kila uwezalo kunisaidia, lakini mwisho wa siku uvumilivu umenishinda nimeamua kutokuwa mjinga tena kwenye mapenzi,” alisema Gululi.
“Gululi niambie umefanya nini?”
Basi akanisimulia mambo ambayo nilipoyasikia tu hata mimi mwenyewe nikabaki mdomo 



UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA ALHAMISI 

VALENTINES'S DAY: ASILI NA HISTORIA YAKE HADI KUSISIMUA ULIMWENGU

Siku ya wapendanao au Valentine's day ina historia ndefu sana. 
Asili ya siku ya wapendanao "Valentine's Day" ni St Valentine, mhubiri wa kikristo aliyekuwa akiishi karibu na mji wa Roma katika karne ya tatu wakati wa utawala wa Claudis II.

Claudis alitaka awe na jeshi kubwa akategemea vijana wangejitolea na kujiunga na jeshi lake. Lakini vijana wengi hawakupenda vita kwakuwa hawakutaka kuziacha familia zao na watoto wao.

Claudis akafikiria akaona hawa vijana kuwakomesha waingie jeshini ni kupiga marufuku watu kuoana.Kuanzia hapo akapiga marufuku watu kuoana akitegemea vijana hawatajali sasa kujiunga na jeshi kwasababu ya familia zao.

Askofu Valentine naye kwa siri akawa anawafungisha ndoa vijana hao kwa siri. Claudius aliposikia habari hizo aliamuru Valentine akamatwe na akahukumiwa adhabu ya kifo cha kunyongwa.

Wakati akiwa jela akisubiri siku yake ya kunyongwa Valentine alikuwa akitembelewa na vijana waliokuwa wakimpelekea maua kuonyesha wako pamoja nae.

Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda kumtembelea ni mtoto wa mkuu wa gereza ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka kwenye selo la Valentine "kupiga naye stori".

Inasemekana kwamba Valentine aliangukia katika mapenzi na binti huyo wa mkuu wa gereza wakati anasubiria kunyongwa.

Inasemekana kwamba muda mchache kabla hajanyongwa Valentine aliomba kalamu na karatasi na kuandika meseji yake ya kuaga akiweka sahihi "From Your Valentine" ( kutoka kwa Valentine wako )

Valentine akanyongwa tarehe 14 februari mwaka 269 AD. Baada ya kunyongwa kwa Valentine, vijana wa Roma walianza kumuiga Valentine na kuwaandikia na kuwatumia wanawake waliowapenda salamu za mapenzi.

Tangia siku hiyo tarehe hiyo ikaanza kuhusishwa urafiki, upendo na mahaba duniani huku ikihusishwa zaidi na mambo ya mapenzi.

Siku hiyo imezidi kuwa maarufu kila miaka inavyoenda huku huku makampuni yakiigeuza siku hiyo kuwa ya biashara zaidi kwa kufanya kila kitu maalumu kwa siku ya wapendanao kionekane kuwa inabidi kiwe chekundu kuanzia kadi za salamu, maua, mpaka nguo wavaazo wapendanao inabidi ziwe nyekundu.

Kuna watu wengi pia ambao hawasherehekei siku hii kwa kuhoji umuhimu wa kuonyesha kumjali umpendaye katika siku moja tu ya mwaka badala ya siku zote 365.

SUMU YA PENZI SEHEMU YA THEMANINI NA SITA(86)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Basi ikawa kama vile Gululi amenitia moyo, japo kuwa mbinu zangu sio za kihivyo lakini zilikuwa zikienda vizuri. Siku hiyo nikamwambia juu avae kitop chini akavaa khanga, ikabidi nimfunge mimi mwenyewe maana yeye alikuwa akizoea kujifunga tumboni kama mtu mzima, wakati wasichana wakisasa wote wanafunga mlegezo. 
Tukaenda na vikapu vyetu kununua mahitaji ya kupika mchana kwa makusudi japokuwa nilijua hatuwezi kukutana na mumewe Gululi lakini nilitaka mtaa mzima ukimuona Gululi ukampe taarifa mumewe kuwa mkewe kawa mcharo.
Basi taratibu tukatembea na kununua vyetu, tukawa tunarudi, kama kawaida vijiwe vya madereva bajaji  wakawa wanazidi kumsumbua Gululi, wengine wakimsifia tu hadharani kuwa amependeza, wengine ni wanawake wa hapo mtaani wakimtazama kwa husuda, tena nikamtaka tujipitishe kwenye vijiwe vya marafiki wa mumewe ili mradi tu maneno yakamfikie mlengwa.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMATANO