HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Rais Magufuli aagiza TCRA kuzifuta kampuni za simu zitakazoshindwa kujiunga na soko la hisa

Rais John Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuyafuta makampuni ya simu yatakayoshindwa kujiunga na Soko la hisa la Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema hayo leo Juni Mosi, wakati akizindua mfumo mpya wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Pia ameziagiza taasisi za Serikali na kampuni binafsi kujiunga na mfumo wa ukusanyaji mapato ili kuiwezesha Serikali kupata kodi bila uonevu kwa upande wowote.
Rais Magufuli amesema dhamira ya Serikali ni kukusanya kodi bila kuwepo kwa malalamiko kutoka upande wowote.
Pia amepiga marufuku wizara na taasisi nyingine za Serikali kuanzisha vituo vya taarifa kwa kuwa vilivyopo ni vingi na wakati huo vinatumia gharama kubwa katika kuanzisha.
“Data Centre kama hii ni mkombozi mwingine wa kupunguza kero mbalimbali, kwa sababu ukijaza vocha yako uko Zanzibar, ukinunulia vocha yako Kigoma au Moshi, hiyo pesa inakuja TRA, hakuna mabishano” amesema
Kadhalika Rais Magufuli amesema anajivunia kuwa na mitandao mingi ya simu ambayo inamsaidia kuwasiliana bila kero wakati wowote.
“Mimi nina mitandao yote ya simu, nina Tigo, Airtel, Vodacom na hata TTCL, mtu akinitafuta huku Airtel,akanikosa ninaweza kuweka Tigo, ili mradi ninatambalika kila mahali,” amesema
Pia amesema, mitandao hiyo ya simu inamsaidia kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea nchini na duniani.
Hata hivyo, Rais amezitaka kampuni za simu kuhakikisha zinalipa kodi ili serikali isikose mapato yake.
Amesema mfumo huo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki una faida yake na hivyo akawaomba watanzania, wawekezaji na wafanyabiashara kukitumia chombo hicho kwa manufaa ya taifa zima.
“Lengo la serikali ni kukusanya mapato. Wenye moyo wa kulipa kodi zao kihalali ni wachache, lakini wapo wasiotaka kulipa kodi na wapo wanaoonewa kwa kubambikiwa kodi. Lakini kwa wale wasiolipa, muarobaini wao ndiyo huu,” amesema
Pia Rais amesema amefurahi baada ya kutembelea kituo cha ukusanyaji taarifa (Data Centre)na kueleza kuwa umuhimu wake ni kukusanya na kulinda taarifa za nchi.
“Nimefurahi kwa sababu haya ni mafanikio makubwa kwa nchi yetu na ninapenda kuwashukuru waliowezesha kufikia mafanikio haya.” amesema

Sugu awaijia juu TCRA baada ya kuzizuia TV za mtandaoni

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi amelaani kitendo cha mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA kuzizuia online TV kuendelea kufanya kazi kama TV za kawaida hadi pale itakapotolewa muongozo na sheria za kuziendesha.

Katazo hilo itaziathiri baadhi ya TV za mtandaoni zenye umaarufu ikiwemo Ayo TV ya Millard Ayo. Akiongea bungeni leo mjini Dodoma, Mbilinyi amedai kuwa uamuzi huo unaliingiza taifa gizani.
“Tunakuwa North Korea kwa spidi ya ajabu sana,” amesema.
“Tunaonekana wa ajabu kwenye international community kwa maamuzi kama haya. Kwasababu wananchi wana haki ya kupata habari kutoka upande wa pili, mfano jana Askofu Gwajima na mfanyabiashara Manji walipata nafasi ya kujibu kwa haraka sana tuhuma dhidi yao zilizotangazwa kwenye TV pendwa za serikali lakini wao wasingeweza kupata nafasi ya live kusingekuwa na online TV wakaweza kujitetea kwa haraka sana,” ameeleza.
“Wananchi sasa wamekuwa wakitegemea online TV kupata habari za bunge kwahiyo ni wazi suala la kuzuia kwa namna yoyote online TV ni mwendelezo wa kuzuia wananchi kupata habari za bunge, ni mwendelezo wa kuliweka taifa gizani.”
Sugu amependekeza kazi za online TV ziendelee hadi pale sheria hizo zitakapotungwa kwasababu uwepo wake hakuvunji sheria yoyote.

RAIS MAGUFULI AMTEUA MHANDISI JAMES MITAYAKINGI KILABA KUWA MKURUGENZI MKUU TCRA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mhandisi James Mitayakingi Kilaba

UKUTA WAIPONZA REDIO YA LOWASSA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui imekifungia kituo cha Redio 5 Arusha kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na kukitoza faini ya sh. Milioni 5 kwa kosa la kukiuka baadhi ya Kanuni za Huduma za Utangazaji (maudhui) kupitia kipindi chake cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo, katika kipindi hicho Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mh. Godbless Lema alitamka maneno ya kashfa yaliyolenga kumdhslilisha Rais John Magufuli na serikali kwa ujumla.

Wakati akisoma maamuzi ya kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Joseph Mapunda, aliongeza kuwa kituo hicho pia kilirusha maneno yaliyo tamkwa na Lema ambayo yalikuwa yakihamasisha wananchi kushiriki katika maandamano ya Ukuta yaliyopigwa marufuku na Jeshi la Polisi.

“Maneno ya Lema yalilenga kuhamasisha wananchi kupambana na jeshi la polisi na hivyo kusababisha uvunjifu wa amani na kuhatarisha usalama wa Taifa,” alisema.

Mapunda alisema uamuzi huo umetolewa na kamati hiyo baada ya kamati hiyo kusikiliza maelezo ya utetezi yaliyotolewa na wa Uongozi wa Redio 5 Arusha.

“Baada ya kusikiliza maelezo ya utetezi kamati imeridhia kuwa kipindi cha matukio kilikiuka baadhi ya kanuni za maudhui namba 5(a,b,c,d,f,h) 6(2) (b, c) na 18 (1) (b),” alisema.

Aliongeza kuwa ” kituo hicho kinatozwa faini ya sh. Milioni 5 ambazo zitatakiwa kulipwa ndani ya siku 30 kuanzia leo, kinafungiwa kwa miezi 3 na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu kwa muda wa Mwaka 1 baada ya kipindi cha kufungiwa kumalizika, “

Hata hivyo, Mapunda alisema haki ya wahusika kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo iko wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo.

Kwa upande wa kituo cha redio cha Magic Fm ambacho nacho pia kwa mujibu wa kamati hiyo kinadaiwa kukiuka kanuni za maudhui kupitia kipindi chake cha Morning Magic kipengele cha Paka Rangi ambapo kilirusha maneno yanayodaiwa kumkejeli rais na wananchi, kimepewa onyo kali pamoja na kutakiwa kuomba radhi kwa muda wa siku tatu mfululizo.

“Baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi yaliyotolewa na Uongozi wa Magic Fm Redio, Kamati ya Maudhui imeridhika kuwa kipindi cha Morning Magic kilikiuka baadhi ya kanuni za huduma za utangazaji 2005. Kamati ya maudhui inaamua kutoa onyo kali kwa Magic Radio, ” alisema na kuongeza.

“Pia inatakiwa kumuomba radhi Rais John Magufuli, wasikilizaji na wananchi kwa ujumla. Tangazo la kuomba radhi litolewe kwa siku tatu mfululizo katika taarifa za habari za saa 10.00 alasriri, na 3.00 usiku kuanzia tarehe 17,9,2016.”

TCRA YAIFUNGIA RADIO 5 MIEZI 3 PAMOJA NA FAINI, MAGIC FM YAFUNGULIWA KWA MASHARTI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maudhui Joseph Mapunda akisoma maauzi ya Kamati ya Maudhui 

 Radio 5

Maamuzi ya Kamati ya Maudhui juu ya Radio 5 Kukiuka Kanuni za Utangazaji:
Kituo kilivunja Kanuni za Maudhui kwa Kumkashifu Rais na Serikali na kuchochea na kuhamasisha uvunjifu wa amani, kupambana na Polisi.
Maamuzi:
1. Fine shilingi 5 million
2. Kufungiwa kwa miezi 3
3. Inawekwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja.

Magic FM

Magic FM yafunguliwa Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania imekifungulia rasmi kituo cha radio cha Magic Fm cha jijini Dar es salaam
Radio Magic fm ilifungiwa kwa muda usiojulikana na Waziri Nape Nauye Agosti 29, 2016 kwa tuhuma za kutangaza kipindi kinachodaiwa kukiuka sheria za utangazaji
Kwa mujibu wa David Ramadhan aliyekuwepo wakati wa kusoma maamuzi ya kamati ya maudhui ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, kamati hiyo imeitaka Radio Magic fm kutekeleza yafuatayo..

1)Kutoa onyo kali radio Magic Fm

2)Kuomba radhi kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Magufuli na wasikilizaji wake, hivyo inatakiwa kuomba radhi kwenye taarifa za habari na tangazo lipewe nafasi kubwa.

TCRA YAVITOZA FAINI YA MILIONI 19 VITUO VIWILI VYA UTANGAZAJI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania leo imevitoza faini ya jumla Sh19m vituo vya utangazaji, ITV, Clouds TV na Redio Clouds kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

TCRA wanasema Clouds Media imepigwa faini hiyo kutokana na kosa la kushabikia mapenzi ya mbuzi na binadamu kwenye chombo chao cha habari na kupiga wimbo wa mwanamuziki Mwana FA ambao unapaswa kupigwa muda maalumu ambao wameagizwa.

ITV wamepigwa faini hiyo kutokana na kipindi kutoka bungeni kilichokuwa kinaoongozwa moja kwa moja, ambapo Mbunge wa Iringa Mjini alisikika akisema "Naibu Spika amekuwa kama anavaa pampas, hataki kubanduka kwenye kiti kuongoza bunge".

TCRA imewakumbusha wadau wote kufuata sheria na maadili ya utangazaji ili kuepuka adhabu na ukiukwaji wa maadili.

TANZANIA YAZIDI KUPAA MATUMIZI YA SIMU ZA MIKONONI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbalawa akizungumza kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28)  unaoendelea jijini Dar es Salaam ukifahamika kama  2016 Mobile 360 Series – Africa  ukihusisha wadau mbalimbali wa mawasiliano ya simu za mikononi.
 Mkurugenzi Mkuu wa GSMA Bw Mats Granryad, akizungumza kwenye mkutano huo.

 Mkurugenzi wa GSMA Afrika Bw Mortimer Hope akizungumza kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo. 

Tanzania ni miongoni mwa mataifa manane barani Afrika ambayo yana soko kubwa la simu za mikononi, ripoti  mpya ya utafiti  iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam imebainisha.
 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo  ijulikanayo;  ‘Uchumi wa simu za mikononi: Afrika 2016’ iliyozinduliwa  kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28)   unahofahamika kama  2016 Mobile 360 Series – Africa  ukihusisha wadau mbalimbali wa aina hiyo ya mawasiliano, Tanzania  imeungana na mataifa ya Nigeria na Ethiopia ambayo  kwa utatu wao yanachukua zaidi ya theluthi moja  ya soko la aina hiyo ya mawasiliano barani Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya  watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga  na huduma ya simu za mikononi  huku kukiwa na idadi kubwa ya watumiaji wa aina hiyo ya mawasiliano wanaohamia kwenye huduma ya internet inayopatikana kwenye simu zao, utafiti mpya uliofanywa na na Umoja wa wadau wa Mawasiliano ya simu za mikononi  Duniani  ujulikanao kama GSMA umebaini.
Ripoti hiyo pia iliangazia mchango wa sekta ya mawasiliano ya simu hizo kiuchumi, ikiwemo ajira, ufadhiri kwa umma (Public Funding) pamoja na mchango wa mawasilian hayo katika ukuaji wa digitali na ushirikishwaji wa kifedha.
“Zaidi ya watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga na huduma ya simu za mikononi, hatua ambayo si tu inawaunganisha bali pia inatoa fursa kwao kuweza kupata huduma nyingine kama vile huduma za afya, utambuzi wa kidigitali na huduma za kifedha,’’ alibainisha Mats Granryad, Mkurugenzi Mkuu wa GSMA. “Uhamiaji wa ghafla kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu miongoni mwa watumiaji  inatoa fursa mpya kwa watumiaji, biashara, serikali na kukuza mzunguko ambao mwaka jana uliongeza zaidi ya dola bilioni 150 kwenye uchumi wa bara la Afrika,’’
Uwekezaji kwenye mtandao (Network) na simu za kisasa (Smartphones) kunachochea uhamiaji zaidi kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu.