HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Wake Wanyimwa Dhamana na Kurudishwa Rumande

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamenyimwa dhamana kwa kesi inayowakabili, wamerudishwa rumande mpaka Julai 17 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri baada ya mabishano makali ya kisheria dhidi ya mawakili wa utetezi na mawakili upande wa jamhuri (serikali).

Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti

BMT yapiga "Stop" Mchakato wa uchaguzi TFF



TFF YAPUNGUZA KIINGILIO MECHI TAIFA STARS, MWAMUZI ADONGO AONYWA

Taifa Stars - timu ya Tanzania ya mpira wa miguu kwa mwaka 2017 inaingia uwanjani kucheza na Botswana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ya kirafiki ya kimataifa katika wiki ya kalenda ya FIFA.

Kwa umuhimu wa mchezo huo na hamasa ambayo uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania umeona hivyo TFF imeatangaza kushusha bei ya kiingilio kwa watu watakaokaa mzunguko kutoka Sh 5,000 hadi Sh. 3,000.

“Wavutieni Watanzania wakaishangilie timu yao, wekeni viingilio vya bei ya chini ambayo Mtanzania itamweka katika mazingira ya kuchangia gharama kidogo kwa timu. Toeni hiyo Sh 5,000 yenu. Wekeni angalau Sh. 3,000,” ameagiza Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Pamoja na punguzo hilo kwa mashabiki wa mpira wa miguu watakaoketi Majukwaa Maalumu - VIP “A” watalipia Sh 15,000 na wale watakaoketi VIP “B” na “C” watalipia Sh 10,000.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga kwa upande wake aliwathibitishia Waandishi wa Habari kwamba kikosi chake kiko imara kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika kuanzia saa 10.00 jioni.

“Tuna morali wa hali ya juu,” alisema Mayanga ambaye aliteuliwa kuinoa timu hiyo mapema mwaka huu.

Kwa upande wa Peter Buffler – Kocha Mkuu wa Botswana, alisema kwamba anatarajiwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa sababu amegundua kuwa kikosi cha Taifa Stars kina vijana wengi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Mbali ya mchezo huo wa kesho, Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo mwingine dhidi ya Burundi Jumanne ijayo, Machi 28, mwaka huu. Mchezo ambao pia ni wa kirafiki wa kimataifa unatarajiwa kuanza saa 10.00 jioni.

MWAMUZI ADONGO AONYWA

Mwamuzi Jacob Adongo amepewa ONYO KALI kwa kushindwa kutafsiri vizuri sheria katika mechi namba 186 kati ya Simba na Mbeya City iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Onyo hilo limetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Kadhalika katika mchezo huo namba 186 (Simba 2 vs Mbeya City 2). Klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa timu yake kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, hivyo kwenda kinyume na Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu.

Adhabu dhidi ya Mbeya City imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.

Mechi namba 190 (Kagera Sugar 1 vs Majimaji 0). Klabu ya Majimaji imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kosa la kutokuwa na Daktari kwenye Kikao cha Maandalizi ya Mechi (Pre Match Meeting) na hata uwanjani wakati wa mchezo. Kitendo hicho ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Kuu, na adhabu ni uzingativu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.

Pia kwa kutumia Kanuni ya 9(8) ya Ligi Kuu imefuta kadi ya njano aliyooneshwa mshambuliaji Jaffari Salum wa Mtibwa Sugar katika mechi hiyo namba 175 kati ya African Lyon na Mtibwa Sugar iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kubaini haikuwa sahihi.

Klabu ya Yanga iandikiwe barua ya Onyo Kali kutokana na benchi lake la ufundi kumlalamikia mara kwa mara Mwamuzi wakati wa mechi ya utangulizi ya U20 kati ya timu hiyo na Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kuhusu mechi za Ligi Daraja la Pili (SDL Play Off)

Mechi namba 3 (Oljoro 1 vs Transit Camp 1). Klabu ya Oljoro imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na washabiki wa timu hiyo kumrushia mawe Mwamuzi akiwa uwanjani.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

PICHA: VIONGOZI MBALIMBALI WA KISIASA WASHUHUDIA MECHI YA SIMBA NA YANGA

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga.(Picha na Francis Dande)
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 
Freeman Mbowe akiwapungia mashabiki wa soka. 
Mbowe.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto), akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema akiwapungia mkono mashabiki wa soka waliokuja kushuhudia pambano la Simba na Yanga.  
 Lowassa akishuhudia pambano la Simba na Yanga. 
 Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya akizungumza na Edward Lowassa.
 Viongozi wakiwa wamesimama kuamboleza kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Yanga na timu ya taifa, Godfrey Bonny.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na msanii wa filamu, Wema Sepetu, wakati wakiingia Uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la Simba na Yanga.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na msanii wa filamu, Wema Sepetu, wakati wakiingia Uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, akiwasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kushuhudia pambano la Simba na Yanga. 

Ligi ya Wanawake ya sogezwa mbele

Ligi kuu ya Wanawake ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) hatua ya 6 Bora ambayo ilikuwa ianze Febrauri 18, 2017 Uwanja wa Karume, imesogezwa mbele kwa muda wa juma moja.

Ligi hiyo sasa itaanza rasmi Februari 26, 2017 kwenye uwanja huohuo wa kumbukumbu ya Karume, Ilala mahali zilipo ofisi za TFF. Hii ni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu.
Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine utaanza saa 10.00 jioni.
Ratiba mpya inaonesha kwamba siku ya Februari 26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na Sisterz.
Ratiba kamili kwa mechi inazofuata itatolewa wiki ijayo. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza au unaoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

JOHN BARNES WA LIVERPOOL KUTUA NCHINI KUANGALIA KOMBE LA STANDARD CHARTERED

  Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi (katikati) akiwa ameambatana na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (kulia) pamoja na Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba wakiwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumzia tukio adhimu la Benki ya Standard Chartered, Tanzania Limited kutimiza miaka 100 tangu ilipofungua milango yake nchini Tanzania kabla ya kumkaribisha Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Sanjay Rughani kutoa risala katika sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa iadara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said (wa pili kushoto) akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa mchezaji aliyewika wa timu ya Liverpool, John Barnes ambapo wateja wa Benki hiyo watapata fursa ya kukutana na mchezaji huyo.
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi (wa pili kulia) akitoa baraka zake kwenye sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine (kulia) akitoa salamu za TFF kwenye sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. 
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine (kulia) akimkabidhi bendera ya TFF Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi (wa pili kulia) na Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (kulia) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool akitoa uchambuzi wa timu hiyo barabara ya kuelekea Anfield wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (katikati) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi (wa pili kulia) huku wengine wakishuhudia tukio hilo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine, Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said (kushoto) na Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (kulia) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool (wa pili kushoto).
 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (katikati)akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine (kulia) kwenye sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (wa tano kulia) akimkabidhi zawadi Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (wa tatu kushoto) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool katika sherehe za uzinduzi huo. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba.
 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (kushoto) akibadilishana mawazo na Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool kabla ya kuanza kwa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi katika picha ya pamoja na timu A na B na waamuzi wa mechi hiyo ya ufunguzi wa wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi akisalimiana na vikosi vya timu A na B kabla ya kuanza kwa mechi hiyo ya ufunguzi wa wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi akibutua mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Kapteni wa timu A Majuto Omary wa gazeti la Mwananchi akiwatoka wachezaji wa timu B ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani wakati wa mechi ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mpiga picha wa Azam TV akimtoka Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani wakati wa mechi ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga akikabidhi zawadi kwa wachezaji wa timu A baada ya kuichapa bao 1-0 timu B kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Bw. Dionis Malinzi
  Kapteni wa timu A Majuto Omary kutoka  gazeti la Mwananchi akifurahia zawadi yake baada ya timu yake kuibuka kidedea dhidi ya timu B kwa bao 1-0 wakati wa mechi ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja timu A iliyoibuka kidedea dhidi ya timu B kwa bao 1-0 kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. 

Na Mwandishi wetu,
MMOJA wa wachezaji waliowika na timu ya Liverpool, John Barnes atawasili nchini mwanzoni mwa mwezi Machi tayari kwa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 yatakayohusisha timu za eneo hili la Afrika Mashariki.
Kauli hiyo imetolewa na  Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered , Tanzania Sanjay Rughani wakati wa uzinduzi wa  awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield katika sherehe murua iliyofanyika kwenye  viwanja  vya Jakaya Kikwete Youth Park.
Katika uzinduzi huo timu mbili za wachezaji watano watano zilicheza kwa dakika kumi na mshindi alipewa zawadi.
Miongoni mwa majina muhimu waliokuwa katika timu zilizoshiriki kuzindua kombe hilo ni Majuto Omar ambaye ndiye aliyetoa pande lililotikisa wavu uliokuwa ukilindwa na kipa Edina. Wengine ni Mtendaji mkuu wa benki hiyo Sanjay Rughani na mwandishi wa Nipashe Somoe Ng'itu.
John Barnes akiwa nchini atazuru mazoezi ya timu ya Taifa ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys, vijana wanaotokea katika mazingira magumu au familia za kipato cha chini pamoja na watoto ambao wana akaunti katika benki ya Standard Chartered.
Taarifa zaidi katika uzinduzi zinasema kwamba Mashindano ya  kombe la Standard yanayohusisha mpira wa miguu unaochezwa kwa dakika 10, dakika 5 kila upande na yanaandaliwa kwa kushirikiana na klabu ya mpira wa miguu ya Liverpool FC ambapo safari hii ikiwa ni mara ya pili tangu yalipozinduliwa nchini  mwaka 2015 kwa mafanikio makubwa.
Standard Chartered ndio wadhamini wakuu wa klabu ya Liverpool tangu mwaka 2010 hadi 2018/2019.
Kama sehemu ya ushirikiano wake na klabu ya Liverpool, Benki ya Standard Chartered imekuwa ikipanga mashindano ya mpira wa miguu  ambayo hulenga masoko muhimu ya benki hiyo yaliyopo katika mabara ya Asia, Afrika na Mashariki ya Kati huku pia ikiyatumia kama jukwaa linaloshirikisha kikamilifu mashabiki wa soka wa maeneo hayo na pia kuchangia katika kukuza maendeleo ya soka.
Yakiwa katika mwaka wake wa sita, mashindano ya Kombe la Sndard Chartered yamekuwa yakiimarika mwaka hata mwaka na kutoa washindi kutoka pande zote za dunia. Mataifa ambayo yamenyakua kombe hilo ni pamoja na Kenya (2016), Korea Kusini (2015) Vietnam (2014), Thailand (2013) na Singapore (2012).
Mashindano haya hufanyika katika makundi matatu ambapo ni ndani ya nchi, nchi zaidi ya moja katika bara na fainali ambazo hufanyika katika uwanja wa Liverpool wa Anfield nchini Uingereza.
Mashindano haya mwaka huu nchini Tanzania yataleta pamoja timu 32 zinazohusisha wateja wa benki hiyo, vyombo vya habari na wadau wengine muhimu. Mashindano yanatazamiwa kutimua vumbi Jumamosi Februari 25 mwaka huu.
mashindano ya mwaka huu yanakwenda sanjari na tukio kubwa na adhimu la Benki ya Standard Chartered , Tanzania Limited kutimiza miaka 100 tangu ilipofungua milango yake nchini Tanzania.
Katika kuadhimisha tukio hilo adhimu Benki pia itaendelea mashindano yatakayojumuisha nchi zingine za eneo hili la Afrika Mashariki ambazo zitaibuka washindi katika nchi za Kenya na Uganda. mashindano hayo yatakayohusisha Kenya na Uganda yatafanyika nchini Jumamosi Machi 4 mwaka huu.
Mshindi wa mashindano hayo ya mwezi Machi ataiwakilisha Afrika Mashariki katika fainali zitakazofanyika katika uwanja wa Anfield ambapo jumla ya timu 10 kutoka katika maeneo mbaliumbali yaliyoko makampuni ya Standard Chartered zitamenyana kwa ajili ya kumpata bingwa atakayeondoka na Kombe la Standard Chartered kwa mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye uzinduzi huo Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered , Sanjay Rughani alisema kuwa benki yake inaona fahari kushirikiana na klabu ya Liverpool akisistiza kwamba taasisi hizo mbili zinarandana kwa mambo mawili umakinifu na kujituma.
Aliongeza kuwa benki itafanya pia shughuli mbalimbali wakati wa mashindano kama sehemu ya kuadhimisha miaka 100 tangu ipige hodi nchini Tanzania.
"Tunapoadhimisha miaka 100 tangu tufungue milango yetu nchini Tanzania tunajisikia vizuri sana kuendesha tena mashindano kwa ajili ya Kombe la Standard Chartered.....tutakuwa pia wenyeji wa ziara ya John Barnes ambapo tutahakikisha anatoa ujuzi wake kadri atakavyoweza kwa klabu za vijana atakapokuwa hapa," Rughani alisema.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Dionizi Malinzi aliishukuru Benki ya Standard Chartered  kwa msaada wake katika kukuza michezo nchini hususani mpira wa miguu pia aliwataka wakaoshiriki kutumia fursa hiyo inayokutanisha timu 32 za ndani na zile zitakazotoka nchi jirani katika kujenga uhusiano mwema.
Mshindi wa mashindano  yatakayohusisha timu zingine za Kenya na Uganda atapata tuzo ya safari ya kwenda Anfield.
Katika safari ya Uingereza  washiriki watakaopata nafasi watasafiri kwa ndege daraja la kawaida na malazi kwa siku tatu.

Aidha timu itapata mafunzo katika chuo cha mafunzo cha Liverpool (LFC) yatakayotolewa na wakongwe wa LFC kufanya ziara katika uwanja  wa Anfield na kufanya ziara Melwood kabla ya kuhudhuria mechi moja wapo ya klabu ya Liverpool itakayopigwa mwezi Mei mwaka huu.

TFF YAITUPILIA MBALI RUFAA YA POLISI DAR ES SALAAM

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea rufaa kutoka Klabu ya Polisi Dar es Salaam dhidi ya Klabu ya Simba kuhusu kumchezesha Mchezaji Novalty Lufunga katika mchezo wao wa Raundi ya Tano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2017.


Madai ya Polisi ni kwamba Mchezaji Novalty Lufunga alioneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo kati ya Simba na Coastal Union katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016 uliofanyika Uwanja wa Taifa, Aprili 11, mwaka jana.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetupilia mbali rufaa hiyo kwa kukosa vigezo vya kikanuni katika uwasilishaji wake na hivyo kukosa sifa ya kusikilizwa. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 18 (1) na (2) ya Kanuni za Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD.

Kanuni ya 18 (1) inasema: “Malalamiko yoyote kuhusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi kwa kamishna wa mchezo au TFF sio zaidi ya masaa sabini na mbili (72hrs) baada ya kumalizika mchezo.”

Kanuni ya 18 (2) inasema: Ada ya malalamiko ni shilingi laki tatu (Tshs 300,000.00). Malalamiko yo yote yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada na kuwasilishwa nje ya muda uliowekwa hayatasikilizwa.”

Hata hivyo, Shirikisho linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kadi nyekundu aliyopewa Mchezaji Novalty Lufunga katika mashindano ya Azam Sports Federation Cup 2016/2017.

Kwa utaratibu wa mashindano haya ambayo ni ya mtoano, adhabu za kadi (njano na nyekundu) zitolewazo uwanjani, zinakoma mwisho wa msimu wa shindano husika isipokuwa kadi hizo zikiongezwa adhabu ya kinidhamu (suspension) ambayo itafahamisha kwa klabu na mchezaji kwa maandishi.

Kadhalika, Kanuni ya 16 ya Kanuni za Kombe la Shirikisho Sehemu ya Tatu inaeleza wazi kuwa matumizi ya kanuni za ligi zitahusika maeneo yanayoruhusu uendeshaji wa shindano la mtoano.

“Adhabu zote zinazohusisha katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam HD zitahusisha na shindano hili tu,” inasema kanuni ya 16 (3) na (4). 

TFF YAMPIGA CHINI KOCHA WA TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.

Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.

Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).

TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.