HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

TGNP YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUJADILI MAPENDEKEZO YA BAJETI YA MWAKA 2017/18

TGNP Mtandao imewakutanisha wadau mbalimbali kutazama nakutoa maoni yao ya bajeti iliyowasilishwa na waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alipowasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 Bungeni mjini Dodoma.

Akizungumza kwenye mkutano Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi amesema wamewakutanisha wadau hao ili kujadili bajeti pendekezwa ya mwaka 2017/18 iliyowasilishwa bungeni mjini Dodoma.

Alizungumzia bajeti hiyo kwenye mlengo wa kijinsia hasa kwa watoto wa kike wanapokuwa mashuleni na hata kwenye sekta mbalimbali zilivyoguswa na bajeti ya 2017/2018.
Mjumbe wa Bodi ya TGNP Mtandao, Edwin Mhina akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo aliyojadiliwa kuhusu hali ya uchumi 2016 na mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18 kabla ya kuaza kwa usomaji wa bajeti ya mwaka 2017/18.
Wadau mbalimbali wa Maendeleo waliokutanishwa na TGNP Mtandao wakiendelea kufuatilia Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alipokuwa anawasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 Bungeni mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi akizungumzia kuhusu kuachwa kwa mtoto wa kike nyuma kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 hasa kwenye mazingira mazuri ya mtoto wa kike anapokuwa shule mara baada ya kumalizika kwa Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alipowasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 iliyosomwa Bungeni mjini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura akizungunzia bajeti ya elimu iliyopeleka pesa nyingi kwenye elimu ya juu na kutengwa pesa ndogo kwenye shule za mzingi pamoja na sekondari ambapo inasababisha ufanisi wa elimu kushuka hapa nchini.

Baadhi ya wadau mbalimbali waliokutanishwa na TGNP Mtandao ili kuangalia bunge mubashara wakati wa uwasilishwaji wa bajeti wakichangia mada mara baada ya kumalizika kwa Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alipowasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 Bungeni mjini Dodoma.

SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA AWAASA MADIWANI WANAWAKE WA JIJI LA DAR KUJITAMBUA KATIKA JAMII.

Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anne Makinda akiwahamasisha Madiwani wanawake wa Jiji la Dar es Salaam walioudhuria mafunzo  ya uongozi, jinsia na bajeti yenye mlengo wa kijinsia pamoja na kutoa uzoefu wake kwenye maswala ya uongozi  kwa wanawake hasa ngazi za juu leo kwenye ukumbi wa TGNP Mtandano jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi Lilian Liundi akizungumza na Madiwani Wanawake kuhusu nguvu ya mwanamke kwenye  jamii  pamoja na kuwapa miongozo kuhusu nafasi zao kwenye uongozi ili kufikia lengo la hamsini kwa hamsini.

Mwanachama wa TGNP Mtandao na mkufunzi wa Mafunzo ya Madiwani wanawake wa Jiji la Dar Es Salaam Profesa Ruth Meena akiwasilisha  mada kuhusu kujitambua kwa mwanamke kwenye jamii, kujua thamani yake pamoja na mchango wake kwenye jamii katika mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbiwa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Ijenzi wa Nguvu Pamoja wa TGNP Mtandao, Grace Kisetu akizungumza jambo kwenye mafunzo ya madiwani wanawake wa Jiji la Dar es Salaam leo
Madiwani wanawake wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo ya uongozi, jinsia na bajeti yenye mlengo wa kijinsia leo kwenye ukumbi wa TGNP Mtandano.
Mkutano ukiendelea
Mwenyekiti wa Muda wa Umoja wa Madiwani Wanawake wa Jiji la Dar es Salaam, Bi. Saada  Mandwanga akitoa shukrani kwa TGNP Mtandao kutoa mafunzo ya uongozi, jinsia na bajeti yenye mlengo wa kijinsia ambayo kwao yamekuwa ni chachu kwenye jamii inayowazunguka.
Baadhi ya wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakiwa kwenye mafunzo ya Madiwani wanawake yanayofanyika kwa siku tatu


Madiwani wanawake wa vyama mbalimbali vya siasa katika Mkoa wa Dar es Salaam wamesema suala la kubadili mtazamo katika ushirikishwaji wa wanawake kwenye maendeleo ni la msingi na linapaswa kutekelezwa kuanzia ngazi za chini. 


Wakizungumza katika warsha ya siku tatu ya Uongozi wa Kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), madiwani hao wamesema haki za wanawake bado zinakandamizwa katika jamii huku vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vikishika kasi. 



Akizungumza katika mafunzo ya siku tatu Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anne Makinda amesema wanawake wanapaswa kuungana kwa pamoja wanapokuwa wanapigania haki zao za msingi. Amewasisitiza kuachana na masuala ya vyama kwenye jambo linalowahusu wanawake wote. Wakifanya hivyo wataweza kupunguza tabaka kubwa kwenye utawala na hata kwenye uzalishaji mali.



Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi Lilian Liundi amesema watoto wa kike wanakosa vipindi vya masomo kutokana na ukosefu wa elimu ya kujihifadhi hasa wanapokuwa katika hedhi. 


“Elimu ya hedhi bado duni sana, hasa vijijini kwa sababu watoto wengi wa kike wanapokuwa katika hedhi huhisi kwamba ni wagonjwa, hivyo hushindwa kuhudhuria vipindi ipasavyo lazima elimu hii itolewe kwa jamii ili kuwawezesha watoto hawa wapate elimu kama ilivyo kwa wale wa kiume,” alisema Lilian Liundi.

TGNP MTANDAO YAWAPONGEZA WASICHANA WALIOFANYA VIZURI KATIKA VYUO MBALIMBALI NCHINI

 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akizungumza na waandishi habari kuhusu kuwapongeza wahitimu waliofanya vizuri katika vyuo mbalimbali nchini katika ukumbi wa TGNP  leo jijini Dar es Salaam. 
 Msichana aliyefanya vizuri katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela akizungmza na waandishi habari juu umahiri wake ambao ulimuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya mwisho katika chuo katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo uliofanyika leo katika Ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.
 Msichana aliyefanya vizuri katika Chuo Kikuu cha  Kairuki, Flora Njiku akizungmza na waandishi habari juu rushwa ya ngono kwa watoto wa kike vyuoni katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo ya vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini uliofanyika leo katika Ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasichana waliofanya vizuri katika matokeo ya vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini wakifuatia kinachoendelea kwenye mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar

Mkutano uliendelea 


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TGNP Mtandao imesema kuwa changamoto inayowakabili wanafunzi wa vyuo  vikuu nchini ni rushwa ya ngono.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wasichana 38  waliofanya vizuri katika elimu ya Juu kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa  TGNP,  Lilian Liundi amesema wanawake wengi wanashindwa kufikia malengo kutokana na changamoto ya ngono na kufanya wanawake kuwa wanyonge.
Amesema kuwa wanawake wanaonekana daraja la pili hali ambayo inafanya kuendelea kuweka mfumo dume wa maamuzi kufanywa na wanaume.
Lilian amesema kuwa wasichana ambao wamefanya vizuri  katika vyuo mbalimbali inaonyesha ukombozi wa wanawake katika kuleta maendeleo ya kumuokoa mwanamke mwezie.
Aidha amesema kuwa TGNP Mtandao imekuwa katika mstari wa mbele katika kuendesha harakati za kumkomboa mwanamke katika changamoto mbalimbali.
Mmoja wahitimu wa waliofanya vizuri , Aisha Soudy  kutoka  Chuo cha  Teku, amesema kuwa wasichana wanachangamoto nyingi ikiwemo na mila na tamaduni ambayo unampendelea zaidi mtoto wa kiume.
Amesema kuwa yuko tayari katika kufanya ukombozi wa mwanamke kwa kutoa msaada pale anapoona anawajibu wa kufanya kwa ajili ya kumuinua Mwanamke.
Kwa upande wa Mhitimu aliyefanya vizuri katika matokeo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela amesema kuwa msichana ana nafasi yake kama  akijitambua anataka kufanya nini katika jamii yake katika kuleta tofauti  kuliko vile wanavyofikiria.
Sara amesema kuwa licha kukabiliwa na changamoto kama mtoto wa kike lakini ameweza kufanya vizuri na kuwataka wasichana kujiamini kuwa wanaweza.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MAKUMBUSHO WAPIGWA MSASA KUHUSU ELIMU YA JINSIA

Wanafuzi wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam, wamepata​ mafunzo maalum ya kuwawezesha kumudu changamoto mbalimbali katika jinsia, yanayowajengea uwezo wa kujitambua vyema na kuisaidia jamii katika maendeleo.
Mratibu wa Uraghibishi wa Wilaya ya Kinondoni chini ya Mtandao wa Jinsia nchini(TGNP) Janeth Mawinza alisema wanatoa mafunzo hayo kupitia klabu maalum za jinsia zilizoanzishwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi kuelewa na kusimamia mambo ya msingi ikiwamo masomo yao.
" Pamoja na mambo ya jinsia ikiwamo kukomesha ukatili wa kujinsia wanafundishwa pia kutambua mahitaji yao muhimu ikiwamo ulinzi na Usalama, mfano katika shule hii kuna zsidi ya wanafunzi 1,400 lakini kuna matundu ya vyoo 10 ambayo matundu mawili ni kwa ajili ya walimu 8 kwa ajili yao hayawatoshi kulingana na idadi yao,"alisema.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Uraghabishi , Bi. Rehema Mwateba akiwasilisha mada kuhusu masuala ya ukatili wa jinsia kwa watoto wa kike kwa wanafunzi wa club ya jinsia ya Shule ya sekondari ya Makumbusho yaliyofanyika leo jijini Dar leo.(Picha na Geofrey Adroph)
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akitoa mafunzo kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Makumbusho leo kwenye mafunzo ya Uraghabishi yaliyoaratibiwa na shirika la TGNP Mtandao.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho, Bi. Edina Ngelageza akizingumza na wanafunzi pamoja na wageni kutoka kwenye vituo vya taarifa na maarifa vya Jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo kwa club ya jinsia ya shuleni hapo.
Baadhi ya wageni kutoka vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na wawezeshaji wakati wa mafunzo ya siku tatu katika shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar leo.
Mraghabishi Mlezi wa Club ya shule ya Msingi Mchangani, Monica Alex  akiwasilisha mada kuhusu jinsi ya kujiandaa kwa vijana hao ili waje kuwa mabalozi wa masuala ya kijinsia wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya wadau kutoka vituo vya taarifa na maarifa wakichangia mada wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa club ya jinsia ya Shule ya sekondari ya Makumbusho yaliyofanyika leo jijini Dar.
Mwezeshaji ambaye ni Mwalimu Mlezi wa Kituo cha  Shule ya Msingi ya Mchangani, Goodluck Busago akitoa mada kwa club ya jinsia ya Shule ya sekondari ya Makumbusho.


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Makumbusho wakichangia mada wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa ili kuwaandaa wanafunzi hao ili kuwa mabalozi wazuri wa masuala ya kijinsia katika jamii.

Baadhi ya wanafunzi wa Club ya jinsia katika shule ya Sekondari ya Makumbusho wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika shule hiyo leo jijini Dar.
Wawezeshaji wa Mafunzo ya Uraghabishi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa club ya jinsi katika shule ya sekondari ya Makumbusho.

MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP) WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA


Mtandao wa Jinsia (Tanzania Gender Network Programme- TGNP) umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga nakwa ajili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.


Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili (Machi 2 na Machi 3 mwaka 2017 katika ukumbi wa Vijana Center katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga pia yamewakutanisha waandishi hao wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa vilivyopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni mwezeshaji Bi Nyanjura Kalindo alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya kijinsia na kuwakutanisha na wanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ili kuongeza nguvu ya pamoja.
“Vipaumbele vya TGNP ni vitano ambavyo ni afya,elimu,kilimo,uziduzi na maji hivyo kwa kuwapatia mafunzo waandishi wa habari tunaamini kabisa itaongeza chachu kuandika habari kwa usahihi zaidi kuhusu masuala ya kijinsia”,alieleza Kalindo.
Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bwana Rasel Madaha aliwaomba waandishi wa habari kufika katika maeneo ya pembezoni kwani vitendo vya ukatili wa kijinsia yapo na hayaandikwi hali inayosababisha vitendo hivyo kuendelea kujitokeza na kuwafanya baadhi ya watu kuendelea kunyanyasika.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Nyanjura Kalindo akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kijinsia
Mwandishi wa habari gazeti la Nipashe Marco Maduhu akichangia mada wakati wa semina/mafunzo hayo.Kulia kwake ni wanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia kutoka kata ya Mwadui-Luhumbo wilayani Kishapu wakiwa ukumbini
Mwezeshaji Nyanjura Kalindo kutoka mtandao wa jinsia Tanzania akitoa mada ukumbini
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha akizungumza ukumbini
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha akiwasisitiza waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu watu wasio na sauti katika jamii
Mwandishi wa habari wa radio Free Africa Malaki Philipo (kulia) na Steve Kanyefu kutoka Radio Faraja fm stereo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na mwezeshaji Rasel Madaha
Mwezeshaji Rasel Madaha akiendelea kutoa mada
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na mwezeshaji wa mafunzo hayo Rasel Madaha
Mafunzo yanaendelea.Kulia ni mwanaharakati wa masuala ya jinsia kutoka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Kasigwa Adram,katikati ni mwandishi wa habari Sam Bahari akifuatiwa na Charles Jilala ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka wilayani Kishapu
Katikati ni mwandishi wa habari wa DW,Veronica Natalis akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.Wa kwanza kushoto ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Elizabeth Joseph kutoka wilayani Kishapu
Mwandishi wa habari wa gazeti la Jamboleo Stephen Kidoyayi akichangia mada ukumbini.Kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja,bi Moshi Ndugulile
Katikati ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Rahel Madundo akiwa na washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Marco Maduhu akichangia mada wakati wa mafunzo hayo
Kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Stella Ibengwe akifuatiwa na Kareny Masasy wa gazeti la Habari leo na Wezay Ally kutoka radio Faraja 
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja Steve Kanyefu akichangia mada ukumbini
Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Rahel Lisesi kutoka wilayani Kishapu akielezea changamoto zinazowakabili wananchi wanaozunguka mgodi wa madini ya almasi wa Williamson uliopo Mwadui wilayani Kishapu
Mwandishi wa habari wa Azam TV,bwana Stephen Wang'anyi akichangia mada ukumbini.Kulia kwake ni mwandishi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde
Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru na Mzalendo,bwana Chibura Makorongo(aliyenyoosha mkono) akichangia hoja ukumbini
Kushoto ni mwezeshaji Nyanjura Kalindo akisisitiza jambo ukumbini
Mwandishi wa habari kutoka radio Faraja,Steve Kanyefu akichangia mada wakati wa mafunzo hayo
Kushoto ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia 
Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka wilaya ya Kishapu Charles Jilala akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata ya Mwadui-Luhumbo wilayani humo katika sekta ya afya,elimu,kilimo,uziduaji na maji
Mwandishi wa habari kutoka radio Faraja Simeo Makoba akiwa amenyoosha mkono kwa ajili ya kuchangia mada 
Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia Rahel Madundo akielezea changamoto zinazowakabili wananchi wilayani Kishapu

 Picha ya pamoja baada ya mafunzo 
 Picha ya pamojaPicha ya pamoja ,wawezashaji wa mafunzo hayo,Rasel Madaha (kushoto) na Nyanjura Kalindo na Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC)


Picha na Frank Mshana,Stephen Wang'anyi na Kadama Malunde- Malunde1 blog