HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

TAIFA STARS YAENDELEA KUJINOA NCHINI MISRI

Kipa Said Mohammed Nduda , akichupa kuzuia mpira wakati wa mazoezi yanayosimamiwa na Kocha wa Makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata aliyepiga magoti katika mazoezi yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kucheza na Lesotho Juni 10, 2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon. Picha na Alfred Lucas wa TFF.
Kiungo wa pembeni wa Taifa Stars, Simon Msuva akiwa kwenye kasi kuwahi mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kucheza na Lesotho Juni 10, 2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon. Picha na Alfred Lucas wa TFF.
Libero wa Taifa Stars, Erasto Nyoni (katikati) akijitahidi kudhibiti mpira mbele ya washambuliaji wenye njaa ya kufunga, Ibrahim Ajib (kulia) na Abderheman Mussa kabla ya kipa Said Mohammed hajatokea kusaidia wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kucheza na Lesotho Juni 10, 2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon. Picha na Alfred Lucas wa TFF.

TAIFA STARS: MWENDO WA DAKIKA 1,500 KWA SIKU 8

Mshambuliaji wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbaraka Yussuf Abeid (katikati) ‘anaposepa’ na kijiji yaani kuhama au kuondoka na idadi kubwa ya watu/mabeki waliomzunguka wakiwamo Salum Mbonde, Shomari Kapombe na Kiungo Aboubakar Salum katika mazoezi ya timu yanayofanyika Uwanja wa mazoezi wa Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL inajiandaa kucheza na Lesotho Juni 10, 2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon. Picha na Alfred Lucas wa TFF.


Mpaka leo asubuhi Juni 2, mwaka huu, Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga pamoja na wenzake katika benchi la ufundi, wamekinoa kikosi hicho kwa dakika 420 ndani ya Uwanja wa mazoezi wa Kituo cha michezo cha Tolip yaani Tolip Sports City hapa Alexandria, Misri. 

Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mayanga, Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL itafanya mazoezi yasiyopungua dakika 1,500 katika kambi iliyoanza Mei 31, 2017 usiku na kufikia kikomo Juni 7, mwaka. 

Siku ya kwanza ya kambi Mei 31, mwaka huu Kocha Mayanga alianza na dakika 120 za mwanzo baada ya kusafiri salama kutoka Tanzania hadi hapa Misri. 

Kila siku Taifa Stars ina programu mbili ambako asubuhi timu inafundishwa kwa dakika 90 uwanjani kwa mazoezi mbalimbali na kwa programu ya usiku ni dakika 120 ambako huanza saa 3.00 (saa 2100) usiku na kumaliza saa 5.00 (saa 2300) usiku kwa saa za hapa Misri. 

Kwa msingi huo, Kocha Mayanga kwa kusaidiana na benchi lake la ufiundi, anakionoa kikosi hicho kwa takribani saa 25 kwa wiki, kabla ya kurejea nyumbani. Timu itarudi Tanzania usiku wa kuamkia Juni 8, mwaka huu. 

Ikiwa nyumbani Tanzania, Mayanga atawanoa tena kwa dakika nyingine 180 tayari kabisa kuivaa Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku. 

Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon. 

Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo. 

Akizungumza mwenendo wa mazoezi kwa saa 300 za mwanzo, Kocha Mayanga amesema: “Nafarajika vijana wangu wameendelea kufunguka. Hapa hawana usumbufu wo wote, ni mazoezi na kupumzika kulingana na ratiba na chakula.” 

Mazoezi ya Mayanga hayathiri maendeleo ya mwili wa binadamu kadhalika nguzo ya funga kwa wale ambao wako kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwani ratiba huonyesha huanza kunolewa kuanzia saa 12.00 alfajiri - saa mbili baadaye baada ya daku (Uhudumiwa daku kabla ya saa 11.00 alfajiri), lakini pia saa 3.00 usiku ikiwa ni saa mbili baada ya kufuturu (Futari ni saa 12.45 jioni). 


Ikiwa hapa kambini, timu hupata huduma zote kwa upande wa chakula na wachezaji wana faraja ya kizalendo kuitumikia timu yao ambayo ina mtihani dhidi ya Lesotho wakijenga imani kabisa kwamba watafanikiwa.

TFF YAMPIGA CHINI KOCHA WA TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.

Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.

Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).

TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.

STARS YALALA 3 - 0 MBELE YA WENYEJI ZIMBABWE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mshambuliaji wsa Taifa Stars, Elius Maguri akichuana na beki wa Zimbabwe, Hadebe Teenage katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe leo. Tanzania ilifungwa mabao 3-0.
Beki Michael Aidan wa Tanzania akijiandaa kumtoka mchezaji wa Zimbabwe, Danny Phiri katika mchezo huo.

TAIFA STARS WAJIFUA UWANJA WA TAIFA ZIMBABWE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wachezaji wa kikosi cha timu ya soka cha Taifa, Taifa Stars Mbwana Sammata (kushoto)
 na Thomas Ulimwengu wakijadiliana jamabo wakati wa mazoezi ya timu hiyo katika uwanja wa Taifa Zimbabwe, Harare jana.
Wachezaji wa kikosi cha timu ya soka cha Taifa, Taifa Stars 
Wachezaji wa kikosi cha timu ya soka cha Taifa, Taifa Stars wakiwa mazoezini mjini Harare, Zimbabwe
Kocha Mkuu wa Stars, Charles Bonoifas Mkwasa ( kushoto ) akiwapa maelekezo wasaidizi wake

TAIFA STARS KUJIPIMA NA ETHIOPIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), inatarajiwa kucheza na Ethiopia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Oktoba 8, 2016.



Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), wameomba mchezo huo ufanyike kwao.

Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa atakuwa na nafasi ya kuandaa kikosi chake kuanzia Oktoba 3, 2016 mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu kabla ya kupisha kalenda hiyo ya FIFA ya michuano ya kimataifa.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.

Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani, Colombia na Brazil.

Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.

HIKI NDO KIKOSI CHA TAIFA STARS CHA WACHEZAJI 20 KITAKACHO KWENDA NIGERIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.

Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
“Tanzania hatuwezi kupuumza mchezo huu, tumeuchukulia serious (kwa umakini) kabisa kwa sababu tunacheza ugenini ambako matokeo mazuri yanaweza kutusongesha mbele na kuingia ndani ya timu 99 bora katika viwango vya FIFA,” amesema Mkwasa.
Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
“Timu itaingia kambini Agosti 28, itakaa kambini kwa siku tano kabla ya kusafiri kucheza mchezo huo wa kukamilisha ratiba ambao Misri tayari wameshafuzu fainali za Afrika,” amesema Mkwasa na kuongeza kuwa kuna mchezaji wa Tanzania, Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana baadaye amwite kuchezea timu ya taifa. Anakipiga Klabu ya Brencia Calcio ya Italia.
Wachezaji walioitwa:


Makipa

Deogratius Munishi – Young Africans
Aishi Manula – Azam FC


Mabeki

Kelvin Yondani – Young Africans
Vicent Andrew – Young Africans
Mwinyi Haji – Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe – Azam FC
David Mwantika – Azam FC


Viungo

Himid Mao – Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi – Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania


Washambuliaji

Simon Msuva – Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco – Azam FC
Mbwana Samatta – CK Genk ya Ubelgiji

MKWASA AAHIRISHA KAMBI TAIFA STARS

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kutokana na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu, imefahamika.

Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC.

Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki wa klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.

Taifa Stars ina mchezo na jijini Lagos, Nigeria Septemba 2, 2016 ambao ni wa kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad kujitoa. Wachezaji ambao Mkwasa aliwaita mapema wiki hii ni: Makipa: Deogratius Munishi, Aishi Manula, Benny Kakolanya, Mebeki: Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Mohamed Husein ‘Tshabalala’, Juma Abdul, Erasto Nyoni, Viungo: Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Juma Mahadhi, Hassan Kabunda, Washambuliaji: Simon Msuva, Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Ajib, John Bocco, Jeremia Juma