HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA SASA RUKSA KUTUMIA MIHURI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa muda kwa waraka uliotoa muungozo wa matumizi ya Mihuri kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji leo jijini Dar es Salaam.
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali imesitisha waraka wa muongozo uliotolewa kuhusu matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa Mitaa na vijiji mpaka pale itakaposhirikiana na kukubaliana namna bora ya kuendesha masuala ya kuhudumia wananchi.

Akizungumza na baadhi ya wenyeviti wa mtaa, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewataka wenyeviti wa mitaa nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.

Mhe.Simbachawene alisema kuwa nia ya kusitisha waraka huo ni kuweka utendaji mzuri baina ya Serikali na watendaji wake wa chini.

“Utaratibu uliopo uendelee mpaka pale Serikali itakapotoa utaratibu mwingine wa matumizi mbalimbali ya mihuri hiyo baada ya kujadiliwa na kushirikiana vya kutosha” alifafanua Waziri Simbachawene.

Mhe.Simbachawene alisema kuwa kuna baadhi ya wenyeviti wa mitaa wamekuwa wakitumia vibaya mihuri hiyo na kupelekea migongano na migogoro ya ardhi katika vijiji na mitaa ikiwemo maeneo ya Ununio, Temeke.

Mbali na hayo alisema kuwa katika Tangazo la Serikali namba 3 lililotolewa 5 Septemba, 1994 limeeleza baadhi ya vitendea kazi vya mwenyekiti wa mtaa ni bendera yenye nembo ya Halmashauri, daftari ya kutunza kumbukumbu na rejista ya makazi.

Alisema kuwa mamlaka ya mwenyekiti haitokani na mihuri, bali utendaji uliopo ndani ya mtaa au kijiji husika, hivyo mamlaka ya mwenyekiti ipo pale pale na haibemwi na muhuri bali muhuri huonesha nguvu ya ofisi baada ya kuwashirikisha watendaji tofauti ndani ya kijiji katika kutoa maamuzi.

 “Mhuri si mali ya mwenyekiti binafsi, hivyo kwa yeyote atakayekiuka matumizi ya mihuri hiyo Sheria itachukua mkondo wake” alisisitiza Mhe. Simbachawene.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke Bakiri Makele, ameahidi kushirikiana na Serikali kwa kutumia mihuri hiyo kwa kufuata Sheria na taraibu zilizopo.

Naye Katibu wa Wenyeviti hao, Marium Machicha alimshukuru Waziri mwenye dhamana kwa kauli aliyoitoa baada ya kuliona tatizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi.

Serikali ilitoa Muongozo huo wa namna wa matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa mitaa na vijiji kwa sababu ya matumizi mabaya ya mihuri kwa baadhi ya wenyeviti wa mtaa na vijiji nchini.

MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA MBEYA DAY ASIMAMISHWA KAZI BAADA YA TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI SHULENI HAPO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.




RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.




NAIBU WAZIRI TAMISEMI,SELMANI JAFO ANUSURIKA KIFO AJALINI MBEYA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.

Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin bahat nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguz alisema hakuumia popote ni wazima.

Alisema baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge.
Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.
Askari wa usalama barabaran wilayani Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea
Picha zote kwa hisani ya Mbeya yetu

TAZAMA HAPA ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ofisi ya Rais -TAMISEMI inatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili (Second Selection) kwa mwaka 2016. 

Jumla ya wanafunzi 3,918 wakiwemo wasichana 2,413 na wavulana 1,505 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza.
 
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740 sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.
 
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2015 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii.
 
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz 

Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI 


WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA MACHINGA WAONDOLEWE KARIAKOO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga katika maeneo ya soko la Kariakoo na barabarani, hususan karibu na barabara za mabasi ya mwendo kasi.

Akizungumza jana na Kamati ya Bunge, Waziri huyo wa TAMISEMI alisema kuwa kurejea kwa wafanyabiashara hao katika maeneo hayo kumeleta usumbufu mkubwa na uchafu wa mazingira katika maeneo ya jiji.

“Namuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaondoe na asilegeze kamba,” alisema Waziri Simbachawene.

Alisema kuwa hali hiyo imetokana na tafsiri isiyo sahihi ya agizo la Rais John Magufuli alipokuwa ziarani Mkoani Mwanza.

“Wala agizo  la Mheshimiwa Rais halikumaanisha hicho. Mheshimiwa Rais alisema tuwatafutie maeneo mbadala ambao wapo maeneo kama ya Mwanza na walikuwa wanafanya biashara ya kuuza nguo, akizungumzia wale particular group walioko pale Mwanza. Kwa Dar es Salaam tulishamaliza huko,” alisema.

Aidha, alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha hakuna hata machinga mmoja atakayeonekana akifanya biashara katika maeneo ya barabara za mabasi yaendayo kasi.

Aigizo hilo la Waziri Simbachawene liliungwa Mkono na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge ambao walisema kuwa hali ya soko la Kariakoo imekuwa mbaya kutokana na kuzagaa kwa machinga.

MBUNGE WA ARUSHA MJINI NA DC ARUSHA WAVAANA MBELE YA JAFO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kikao cha Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo na watendaji jijini hapa nusra kivurugike baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Goodbless Lema kumtuhumu mkuu wa wilaya hiyo, Mrisho Gambo kwa kutumia madaraka yake vibaya na kutokuheshimu mipaka yake ya kazi.
Lema amedai kuwa kitendo cha DC kuandika barua Tamisemi na kutoa nakala Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza ongezeko la posho za madiwani kutoka Sh100,000 hadi Sh120,000 zilizopitishwa na kupata baraka za Ofisi ya Katibu Tawala, kinaonesha anafanya siasa zisizo na tija.
Pia alimtuhumu kuingilia utaratibu wa vibanda vya wafanyabiashara kupitia madalali jambo linalopingwa na baraza la madiwani linaloongozwa na Chadema.
Hata hivyo Gambo alisema yeye ni kiongozi mkuu wa wilaya na vyombo vyote viko chini yake na anawajibika kuingilia kati pale anapoona kuna changamoto zinazohitaji kupatiwa ufumbuzi.
Alisema hatasita kuchukua hatua zinapaswa kwani ameaminiwa na Rais, ndio maana ameendelea na wadhifa huo na haitaji kujifunza ukuu wa wilaya kwani amekuwa kwenye nafasi hiyo kwa miaka mitano sasa.

CHANZO: MWANANCHI