Rais Dokta Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Misenyi muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha Kabyaile wilayani misenyi mkoani Kagera.
MAJALIWA APOKEA MSAADA WA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA
By: VIJIMAMBO on December 22, 2016 / comment : 0 Kassim Majaliwa, Matukio, Tetemeko la Bukoba, waziri mkuu
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa shilingi milioni 10 kutoka Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dkt. Brown Mwakipesele ukiwa ni mchango wa kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi yake , Oysterbay jijini Dar es salaam Desemba 22, 2016. Katikati ni Mchungaji Pray God Mgonja wa kanisa hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT, Dkt. Brown Mwakipesile kabla ya kupokea msada wa shilingi milioni 10 uliotolewa na kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 22, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dkt. Brown Mwakipesile kabla ya kupokea msaada wa Shilingi milioni 10 ukiwa ni mchango wa kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Desemba 22., 2016.
PLATINUM CREDIT TANZANIA YACHANGIA MAAFA YA KAGERA
By: VIJIMAMBO on October 21, 2016 / comment : 0 Matukio, Mkuu wa Mkoa, Tetemeko la Bukoba
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Afisa masoko Platinum Credit
Tanzania, Gideon Lufunyo (kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji
ambayo ni sawa na tani 15 kwa Mkuu wa mkoa Kagera, Salum Kijuu ikiwa ni msaada
wa taasisi hiyo kwa waathirika wa tetemekonla Ardhi mkoani humo.
Kampuni ya Platnum Credit
Tanzania Leo imekabidhi msaada wa mifuko 300 ya sumenti kwa mkuu wa mkoa wa
Bukoba Salum Kajuu kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea
hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo Jana ofisa masomo wa kampuni hiyo Gideon Lufunyo
alisema tetemeko hilo limeleta madhara
mkubwa ambayo yamewagusa n kwamba nia yao ni kuona shule kinaendelea na ratiba
ya kawaida ili watoto wasikose elimu.
Video: Kagera All Star Ft Baghdad - Inaanza Na Wewe (Tetemeko Kagera)
By: VIJIMAMBO on October 15, 2016 / comment : 0 Burudani, Music, Tetemeko la Bukoba, Video
NAIBU WAZIRI STELLAH MANYANYA AWAONYA WAKANDARASI UJENZI NYAKATO NA IHUNGO
By: VIJIMAMBO on October 04, 2016 / comment : 0 Matukio, Mkuu wa Mkoa, Naibu Waziri, Tetemeko la Bukoba
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo Mjini Bukoba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu akimueleza Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kurudisha hali baada ya tetemeko la ardhi kutokea mkoani huko.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya leo amewasili Mkoani Kagera na kutembelea miundombinu ya sekta ya elimu ili kujionea namna serikali inavyorejesha hali kama awali kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea September 10 mwaka huu.
Akiwa katika shule ya sekondari ya Ihungo, Mhandisi Manyanya amewataka wakandarasi waliopewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa majengo mapya ya Shule za Ihungo na Nyakato kujenga kwa kuzingatia viwango sahihi kulingana na maelekezo ya wataalam wa miamba.
“Mmepewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa shule hii, nawaombeni muzingatie viwango sahihi wakati mnajenga hasa kwa kuangalia mapendekezo ya wataalam wa miamba waliyoyatoa ili kuyaweka majengo katika hali ya usalama” Alisema Mhandishi Manyanya.
Aidha Mhandisi Manyanya amewatahadharisha wakandarasi wenye tabia ya kudokoa vifaa vya ujenzi kutothubutu kufanya hivyo kwani yeyote atayeiba vifaa hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Katika kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu tofauti wanapata elimu sawa Mhandisi Manyanya amewataka walimu wa shule ya msingi Mgeza Mseto kutenda haki sawa wanafunzi wote bila kujali aina ya ulemavu alionao mwanafunzi.
Katika hatua nyingine Mhandisi Manyanya amezitaka shule hasa za sekondari nchini kuanzisha mashamba darasa yatakayowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo shughuli za kilimo na kusaidia kuifanya shule kuwa na hifadhi ya kutosha ya chakula.
Kwa upande wa walimu Mhandisi Manyanya amewapongeza walimu wa wilaya ya Bukoba kwa kujituma na kuwekeza katika kilimo cha migomba na kuwataka walimu kote nchini kuiga mfano huo ili kuwa na chakula cha kutosha na kujiongezea kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Elimu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikagua vifaa ndani ya maabara katika shule ya sekondari ya Ihungo ambayo pia iliathiriwa kiasi kikubwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September 2016
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiongea na baadhi ya wafanyakazi waliopo katika eneo la ujenzi mpya wa shule ya sekondari ya Ihungo na kuwataka kufanya kazi kwa viwango stahiki na kwa wakati pamoja na wakijiepusha na vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akioneshwa baadhi ya majengo yatayojengwa upya katika shule ya sekondari ya Nyakato ambayo pia baadhi ya majengo yake yaliathiriwa na tetemeko la ardhi hiyo kuifanya kuamuliwa kujengwa upya.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimuonesha jambo mwanafunzi mwenye ulemavu katika shule ya msingi Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiwaeleza jambo watoto wenye ulemavu wa ngozi (ALBINISM) wa shule ya Msingi ya Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.
PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO
WATUMISHI Watatu wa Serikali na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bukoba Wamepandishwa Kizimbani
By: VIJIMAMBO on September 29, 2016 / comment : 0 Habari, Katibu tawala, Mahakama, mkuu wa wilaya, Tetemeko la Bukoba
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
WATUMISHI watatu wa serekali akiwemo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la
Bukoba mjini wamepandishwa kizimbani jana na kusomewa mashtaka mawili
ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kufungua akaunti
feki ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye kesi namba 239/2016.
Watumishi
waliofikishwa mahakamani hapo leo ni aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa
Kagera Amantus Msole,mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Kelvin
Makonda,Muhasibu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja wa banki ya CRDB Tawi la Bukoba Carlo Sendwa.
Akiwasomea mashtaka yao kwenye mahakama ya hakimu mkazi ya Bukoba
wakili wa serekali Hashimu Ngole alisema kuwa watuhumiwa hao
wanashitakiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni watuhumiwa walikula
njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana
na jina la akaunti ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye no.015225617300 ,ambapo
wao walifungua akaunti yenye jina la KAMATI MAAFA KAGERA yenye namba
no.0150225617300
Alilitaja shitaka la pili kuwa ni watuhumiwa wanashitakiwa kwa kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume cha sheria.
Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walimwomba hakimu awapatie dhamana
wateja wao kwakuwa bado ni watumishi wa serekali na wanao uwezo wa
kujidhamini wenyewe na hawawezi kutoka nje ya Kagera
Hakimu Mkazi
wa mahakama ya Bukoba Denis Mbelemwa alihairisha kesho hiyo hadi kesho
saa tatu asubuhi baada ya kupitia upya vifungu vya sheria na
kujiridhisha kama watuhumiwa wanasitahili dhamana na kutaka watuhumiwa
warudishwe rumande.
"Nahairisha shauri hili hadi kesho asubuhi
saa tatu nikapitie tena vifungu vya sheria,kutokana na ukubwa wa kesi
hii nione kama watuhumiwa wanadhaminika"alisema
CHANZO: BUKOBA WADAU BLOG
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE APOKEA MSAADA KUTOKA BURUNDI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA.
By: VIJIMAMBO on September 27, 2016 / comment : 0 Matukio, Naibu Waziri, Tetemeko la Bukoba
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akipokea msaada wa chakula kutoka kwa Mhe. Leontine Nzeyimana, Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya Burundi kwa ajili ya Waathirika wa tetemeko la ardhi huko Mkoani Kagera. Msaada huo ni pamoja na mchele tani 100, sukari tani 30, mahindi tani 50 na majani ya chai tani 3.
Mhe. Dkt. Kolimba akitoa shukrani za dhati kwa niaba ya Serikali kwenda Serikali ya Burundi baada ya kupokea msaada huo wa chakula.
Mhe. Dkt. Kolimba akiwa katika picha ya pamoja Mhe. Nzeyimana na wadau wengine. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu akifuatiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi.
WAFANYABIASHARA KARIAKOO WACHANGA SH. MILIONI 60.7 KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA
By: VIJIMAMBO on September 26, 2016 / comment : 0 biashara, Jamii, Matukio, Tetemeko la Bukoba, Uchumi
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, akizungumza jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea michango ya fedha na vifaa kutoka kwa wanachama wa jumuia hiyo kwa ajili ya walioathirika kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Jumla walichanga fedha na vifaa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 60.7. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mtaa Muhonda, Kariakoo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Philimon Chonde, fedha taslimi mchango kutoka kwa wafanyabioashara hao kwa ajili ya walioathirika kwa tetemeko Kagera. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa JWK, Abdalah Mwinyi na Mweka Hazina wa jumuia hiyo, Silvanus Mande.
Katibu wa JWK, Mtaa wa Raha Square, Frank Nduta akikabidhi vitenge na bidhaa nyingine kwa Mwenyekiti wa JWK, Philimon Chonde
Wafanyabiashara wa Mtaa wa Mchikichi Kariakoo, wakitoa msaada wa misumari kwa ajili ya waathirika wa tetemeke, Kagera.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Subscribe to:
Posts (Atom)
PAMOJA BLOG
WANAOTUTEMBELEA
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi kwa kushiriki Maonesho ya...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
WAZIRI DKT. BASHIRU AIAGIZA BODI MPYA YA TAFICO KUIGEUZA TAFICO KUWA INJINI YA UCHUMI SEKTA YA UVUVIWaziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameitaka Bodi mpya ya pili ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kuhakikis...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
-
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu na mafunzo kwa vyuo vikuu pamoja na shule za sekondar...
-
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tati...
BLOGU MARAFIKI
KUMBUKUMBU
HABARI ZINGINE
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015
November 01, 2015
MPYAA: TAZAMA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014
November 07, 2014




















