HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

UN Tanzania Chief visits projects in Zanzibar

UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative, Alvaro Rodriguez (front right) and Deputy Minister of Home Affairs and founder of Tanzania Youth Icon, Hon. Hamad Masauni join local community members in listening to a presentation on the first phase of the UNDP water project.

The UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative, Mr. Alvaro Rodriguez visits the island in a continuation and expansion of UNDP-supported projectsin Unguja and Pemba. Marking his tenth visit to Zanzibar, the UN Chief made several stops in Unguja, to seeseveral water-access projects as well as an environmental conservation project. Mr. Rodriguez is also expected to visit schools in both Pemba and Unguja to assess their facilities ahead of an upcomingwater and sanitation project which will involve ten schools. Thethree-day field visit in Zanzibar is part of UN efforts to monitor projects and meet beneficiaries in communities.
 In Unguja, Mr. Rodriguez visited a USD 90,000 water project in KijwajuniConstituency, Zanzibar Town, where the lives of over 25,000 people have improved through the project which facilitates access to clean water. He later visiteda USD 50,000 UNDP-supported Community Based Conservation Project in Kajengwa, Makunduchi. The conservation project has helped over 15,000 people, mostly women, who previously depended on firewood for cooking. They now have access to more efficient cooking stoves. The project supported the community in planting over 100,000 trees in the area and established 200 beehives which have helped improve nutrition and provide additional income. 
The water and the conservation projects have been running for several years and now that the first phase have been successfully implemented, both projects will be scaled-up. Each project is set to receive USD 50,000 this year through the UNDP Small Grants Programme to begin implementation of phase two. On Friday and Saturday, the UN Chief will also visit a number of schools where UN agencies, namely UNICEF and UNDP, are set to begin Water, Sanitation and Hygiene (WASH) projects later this year. These WASH projects will cover ten schools. Of these ten schools,the ones that will be visited include Mkwajuni Secondary School in Kaskazini, Unguja and Wingwi Primary School in Micheweni District, Pemba. Chairperson of Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Othman Miraji (left); UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative, Mr. Alvaro Rodriguez (far left); and Deputy Minister of Home Affairs and founder of Tanzania Youth Icon, Hon. Hamad Masauni (middle left) visit a new building that TAYI built with support from the European Union through UNICEF.

“The United Nations in Tanzania is keen to see the Revolutionary Government of Zanzibar reach its social and development goals through MKUZA III. Education and Climate Change are two of the priorities of the revolutionary government.In terms of education,the authorities wish to achieve a higher quality education and supporting Goal 6: ‘Clean Water and Sanitation’ at the school level will help achieve this objective. We all believe that a healthy student has a better chance of performing well in school and reaching his or her full potential,” said Mr.Rodriguez. 
Two of the districts where WASH will be implemented, Micheweni and Kaskazini districts offer an example of the current needs that exist when it comes to need to improve the ratio of toilets to students in Zanzibar.For example, the number of students per toilet in KaskaziniA is 1 to 143 for girls and1 to 278 for boys. Sustained intervention is needed to reach the international standard which is1 to 20 for girls and 1 to 25 for boys. UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative, Alvaro Rodriguez (left) being shown some art done by kids who are of programmes being implemented by Tanzania Youth Icon (TAYI). 
UN staff are shown some of the 200 beehives that were created as a result of UNDP's environmental conservation project in Kajengwa, Makunduchi Zanzibar. Some of the Beehives established by the UNDP energy conservation project in Kajengwa, Makunduchi, Zanzibar. UN, Tanzania Youth Icon and government officials visit the borehole that was drilled during the first phase of the clean water access project. UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative Alvaro Rodriguez (right) draws water that is accessible because of the project and places it on the head of one of the local women. UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative, Alvaro Rodriguez announces that UNDP will give an additional sh110m to scale up the clean water access project. Representative of Kikwajuni constituency, Nassor Salim Ali (Jazira); Ministry of Lands, Water, Energy and Environment-Hon. Salama Aboud Talib; UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative, Alvaro Rodriguez; Sheha of Shehia at Kikwajuni, Juma Sadati Haji; Deputy Home Affairs Minister and founder of Tanzania Youth Icon (TAYI), Hon Hamad Masauni take a group photo after announcing phase two of the UNDP water project. UN officials and members of NGO 'Kamati ya Uhifadhi Misitu ya eneo la Kajengwa' pose by some of the over 200,000 trees that were planted by the NGO through the UNDP energy conservation project. Women from Kikwajuni, Zanzibar who will benefit from the second phase of the project listen as the UN, the government and Tanzania Youth Icon (TAYI) explain how they will try and ensure clean water access for them.

UN YAENDELEA KUHAMASISHA VIJANA KUTAMBUA MALENGO 17 YA DUNIA (SDGS)

Umoja wa Mataifa nchini umeendelea na hekaheka za ufundishaji wa machampioni wa kusaidia kueneza malengo 17 ya dunia yanayohusu maendeleo endelevu. Miongoni mwa mambo yaliyofanywa siku ya pili ya ziara ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ni kuendelea kwa mkutano wa vijana unaoakisi Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini Arusha , na kuoongoza kampeni ya elimu ya maendeleo endelevu katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU). Akiwa MoCU Rodriguez aliwataka vijana kujikita katika kuyaelewa malengo ya dunia na kuyafanyia kazi. 
Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akiitambulisha meza kuu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wakati wa kutoa uelewa juu ya malengo ya dunia chuoni hapo.
Akifafanua mchango wa vijana katika kufanikisha malengo hayo, Matibu huyo alisema: “Mchango wa vijana ni muhimu katika kufanikisha malengo endelevu kufika mwaka 2030; hivyo ni vyema kila kijana akafahamu na kuwafundisha vijana wenzie malengo hayo muhimu.” Septemba 2015, wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya malengo mapya ya dunia, malengo ya maendeleo endelevu. 
Malengo hayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 ijayo na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, uchumi na mazingira kwa namna ya kuwa endelevu. Wakati Umoja wa Mataifa (UN) mwaka jana ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake, Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa aliahidi kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya maendeleo kutokana na idadi yao kubwa kubwa zaidi ya asilimia 67 na pia kwa kuwa wao ndio wanaobeba hali ya baadaye ya nchi hii. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza juu ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) walioshiriki semina ya uelewa wa malengo hayo 17 ya dunia iliyofanyika chuoni hapo.

 Aidha alisema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo. "UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu 20,000 wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza," alisema. Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akitoa neno kwa wanafunzi wa MoCU wakati wa semina ya uelewa wa Malengo ya Dunia iliyofanyika chuoni hapo.
Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu na jinsi ya vijana watakavyoweza kujiajiri. Akiwa Moshi jana, alizungumza na wanachuo na wahadhiri ambapo katika chuo hicho cha MoCU 460 walipatiwa mafunzo na pia walimhoji mambo mbalimbali yanayohusu Umoja wa Mataifa na malengo ya dunia ya maendeleo endelevu. Kwa mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha Umoja wa Mataifa ulifua vijana 50 ambao ni machampioni. Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa MoCU wakati wa semina ya uelewa wa malengo ya dunia iliyofanyika chuoni hapo.

Aidha idadi ya vijana waliofikiwa na mafunzo hayo kwa kuambukizana wameongezeka na kufikia zaidi ya elfu 20. Tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo na mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, mwaka jana vijana zaidi wamepata elimu katika maeneo yao kwa kupitia machampioni wa malengo. Kwa sasa Tanzania imehusisha malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano. Picha juu na chini ni wanafunzi na walimu MoCU walioshiriki semina ya uelewa wa malengo ya dunia iliyoendeshwa na Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini chuoni hapo. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na Eng. Salvatory Matemu kutoka Ofisi ya RC Kilimanjaro huku Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Rasilimali watu MoCU, Daud Massambu wakielekea kwenye zoezi la picha ya pamoja. Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa MoCU. Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa MoCU. Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa UN Chapter MoCU, Isaac Evarist (kushoto) pamoja na wanafunzi chuoni hicho. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwapiga msasa machapioni wa malengo ya dunia katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha. Mmoja wa machampioni akipitia kipeperushi kinachoelezea kwa kina malengo 17 ya dunia wakati wa mafunzo yaliyoendeshwa na Mratibu Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (hayupo pichani). Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akisikiliza swali kwa umakini kutoka kwa Waziri wa Habari wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha, John Semindu wakati wa mafunzo kwa machampioni wa SDGs chuoni hapo. Mmoja wa machampioni wa Makumira akiuliza swali kwa Mratibu wa Mashirika ya UN nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani). Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi vyeti kwa machampioni wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha na Taasisi ya Uhasibu ya Arusha (Institute of Accountancy Arusha -IAA) walioshiriki mafunzo hayo. Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akimuelekeza jambo mmoja wa machampioni wa malengo ya dunia wakati wa mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya machampioni wa malengo ya dunia chuoni hapo.

Serikali yamuondoa Mkurugenzi wa UNDP nchini

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP), Bi. Awa Dabo aliyeondolewa nchini.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP) kwa upande wa Tanzania kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Awa Dabo.

Serikali ilifikia uamuzi huo kutokana na  Bi. Dabo kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya Watumishi wenzake na Menejimenti ya Shirika hilo, hivyo kupelekea kuzoretesha utendaji wa shirika hilo nchini na kupunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka zisingechukuliwa.

Baada ya kuthibitishiwa kuondoka nchini, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imetoa rai kwa UNDP kuwakumbusha Watumishi wake kuwa kipaumbele chao ni kufanya kazi na Serikali ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo yamefafanuliwa katika Agenda ya Mwaka 2030.
  
Mwisho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasilino ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 25 Aprili, 2017.

Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa aipongeza Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Benjamin Willium Mkapa. Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini. 
Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiwasikiliza kwa makini. 
Picha ya pamoja 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Bi. Mindi Kasiga naye akiagana na Mhe. Guterres 
Mhe. Guterres akiagana na Dkt. Mahiga mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo yao.
PRESS RELEASE 
UN SECRETARY GENERAL STOPS IN DAR ON HIS WAY TO NEW YORK
H.E. Dr. John Pombe Magufuli, the President of the United Republic of Tanzania has urged the United Nations to continue its support in bringing about political stability in Burundi and the Democratic Republic of Congo.

In his special message to the United Nations Secretary General Mr. Antonio Guterres President Magufuli explained that the recent instability in the two countries has created refugees’ influx in Tanzania and its neighbors, hence the region is committed to ensure political stability is restored. 

Delivering President Magufuli’s message to the United Nations Secretary General Mr. Antonio Guterres, Tanzania’s Foreign Minister Augustine Mahiga said that as the chair of EAC, Tanzania is hopeful with the progress been made in the mediation process in Burundi under the leadership of President Yoweri Museveni of Uganda and facilitated by the former President of Tanzania, H.E. Benjamin William Mkapa. Hon. Mahiga also informed the UN Secretary General that the upcoming EAC Summit is expected to receive a progressive report about the process. 

With regards to the Democratic Republic of Congo, Minister Mahiga revealed that the Southern African Development Community is intending to include the agenda of political transition in DRC, whereby SADC member states are expecting positive deliberations. Tanzania is the current chair of the SADC organ of political, defense and security with the mandate to support the achievement and maintenance of peace and security as well as the rule of law in the SADC region. 

Upon receiving President Magufuli’s message, Mr. Guterres praised Tanzania for its ability to uphold principles of good governance in the country as well as maintaining peace and creating a peaceful environment in the EAC and SADC regions.

Mr. Guterres commended President Magufuli’s efforts in Burundi peace process, and his readiness to host refugees from Burundi, emphasizing the role played by regional communities in Africa in resolving leadership crisis in African countries. 

“The United Nations appreciates the work done by President Mkapa in Burundi under the EAC and its leadership. If the region come together the way EAC has done in the case of Burundi, I am sure together they will be able to establish lasting solutions” he remarked. 

Minister Mahiga told the reporters that President Magufuli met Mr. Guterres during the AU Summit in Addis Ababa earlier this year, where the two leaders exchanged cordial discussions about various issues concerning the region. 

“President Magufuli instructed me to deliver his message to Mr. Guterres, and has also extended an invitation to the Secretary General at an appropriate time to have a working visit in the country” concluded Hon. Mahiga.

Mr. Guterres was met and held talks with Foreign Minister Mahiga at the Julius Nyerere International Airport yesterday night where he was on transit from Somalia and Kenya for a working visit. Also present at the airport was the United Nations Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez and officials from the Ministry of Foreign Affairs including the Director of Multilateral Cooperation Ambassador Celestine Mushy and Ministry’s Spokesperson Ms. Mindi Kasiga. 

Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dar es salaam, Tanzania
March 9, 2017.

UN Tanzania yaadhimisha Siku Kuwakumbuka Wahanga wa Maangamizi ya Moto

Shirika la Umoja wa Mataifa nchini limeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi kwa kuwakutanisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam na kuwapa elimu kuhusu maangamizi hayo. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alisema ni jambo jema kwa wanafunzi hao kupata elimu kuhusu maangamizi ambayo yalifanywa na kiongozi wa zamani wa Ujerumani, Adolf Hitler kwani hata wao wanaweza kuja kuwa viongozi kwa miaka ijayo hivyo kama watapatiwa elimu mapema watajifunza ni mambo gani kiongozi anapaswa kufanya na yapi hapaswi kwa faida ya kila mmoja. “Kwa nyie kama wanafunzi ambao kwa miaka ya baadae wengine mtakuwa viongozi mnapaswa kujifunza kwa jambo kama hili ambalo alifanya Hitler kuwa sio jambo jema, kila binadamu ana haki sawa hakuna ambaye anamshinda mwenzake na huo ndiyo msimamo wa Umoja wa Mataifa,” alisema Vuzo. 
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi kutoka shule ya Chang'ombe, Kibasila, Jitegemee, Kigamboni, Dar es Salaam, Gerezani, Airwing na vijana kutoka Temeke Youth Development Network (TEYODEN) kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na Kuwakumbuka Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto ambapo watu mil. 55 wanakadiriwa kuwa walipoteza maisha. (Picha na Rabi Hume - MO Dewji Blog)

Aidha Afisa Habari huyo alizungumza kuhusu siku mauaji ambayo yalifanywa na Hitler wakati akiwa kiongozi wa Ujerumani katika kipindi cha mwaka 1933 hadi 1939, “Alikuwa akichagua watu ambao wanaonekana kuwa tofauti na kuwaondoa katika jamii ya Wajerumani, anawapeleka katika kambi maalumu na anawaua wengine wanawekwa katika kambi maalumu wanafanyishwa kazi ngumu bila malipo na waliokuwa wanashindwa na wao wanauawa kwa kuchomwa moto hadi kufa, Vuzo aliongeza kwa kusema kuwa, “Mauaji ya moto ni mauaji hatari kuwahi kutokea duniani, ilikuwa ni dhana ya Adolf Hitler kutaka Wanazi kuwa ni watu ambao wamenyoka lakini kumbe ilitakiwa aishi na watu wote katika jamii lakini alipinga hilo,” “Lakini pia alikuwa hawapendi Wayahudi, walikuwa wafanyabiashara wazuri lakini yeye aliwapinga na hata akawa anawambia wananchi wake kuwa Wayahudi kuwa hawafai katika jamii na wasinunue kitu chochote kutoka kwao.” 
Afisa Habari wa Ubalozi wa Ujerumani nchini, Susann Keller akizungumza kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na Kuwakumbuka Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto.

Kwa upande wa Afisa Habari wa Ubalozi wa Ujerumani nchini, Susann Keller alisema kitendo ambacho kilifanywa na Hitler hakikubaliki na ni jambo ambalo Wajerumani wamekuwa wakijutia kila muda kutokana na vitendo vya kikatili ambavyo vilifanyika vilivyosababisha watu wanaokadiriwa kufikia milioni 55 na kati yao milioni sita wakiwa ni Wayahudi kupoteza maisha. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Elimu kwa ajili ya maisha Bora ya Baadae.” Na Rabi Hume, MO Dewji Blog 
Wanafunzi kutoka shule ya Chang'ombe, Kibasila, Jitegemee, Kigamboni, Dar es Salaam, Gerezani, Airwing na vijana kutoka Temeke Youth Development Network (TEYODEN) wakiangalia video inayoelezea historia ya Adolf Hitler na mauaji ambayo alikuwa akiyafanya.
Baadhi ya wanafunzi wakitoa maoni na kuuliza maswali.



Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

MKURUGENZI MKUU WA UNEP AFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA


Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo(kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP), Eric Solheim katika ziara yake mkoani Arusha,Gambo ameiomba UNEP kusaidia fedha mradi wa kulinda chanzo cha maji cha Olgilai kilichopo wilayani Arumeru kinachotumika kusambaza maji jijini Arusha ambacho kimesongwa na shughuli za binadamu kikiwemo kilimo na upandaji miti ambayo sio rafiki na vyanzo vya maji. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP), Eric Solheim akiwa na ujumbe wake wakifatilia mada iliyowasilishwa na Meneja wa Baraza la Mazingira Kanda ya Kaskazini(NEMC) Novatus Mushi.
Mratibu wa kitaifa wa UNEP nchini, Clara Makenya akizungumza jambo kwenye ziara hiyo,kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP), Eric Solheim(kushoto kwake) naa maafisa wengine wa UN pamoja na ofisi ya Mkuu wa mkoa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP), Eric Solheim (mwenye tai) akiangalia chanzo cha maji cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiri jijini Arusha (AUWSA) eneo la Olgilai Kata ya Kiutu alikofika kuangalia uharibifu wa chanzo hicho.