HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

UNESCO YATOA TAHADHARI ONGEZEKO LA JANGWA

Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu. Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo - hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa. Mchango wa mabadiliko ya mazingira katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote. Idadi kubwa ya 'wakimbizi wa mazingira' sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. Na hili hii inategemewa kundelea kuongezeka. 
Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka 2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na Ulaya. Utabiri huu unaonyesha kuwa sehemu zilizo kame na zile zilizo kame zaidi huathirika zaidi na kuenea kwa jangwa na kuhama kwa watu. 
Watu wanaokaa vijijini amabao hutegemea ufugaji wa wanyama, kilimo na maliasili watakuwa katika hatari zaidi ya kuwa wahanga wa athari hizo, ambazo hujumuisha umaskini, kudorora kwa elimu, ukosefu wa uwekezaji, umbali kutoka huduma muhimu, na kutengwa. Ni lazima tukabiliane na hali hii na hii inamaanisha kufanya kazi katika ngazi mbili: Kwanza, ni lazima tusimamie ardhi kwa usahihi,hii ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa jangwa na katika kulinda kiwango chake cha uzalishaji. 
Hifadhi ya Bayongahewa ya Las Bardenas Reales ya UNESCO iliyoko nchini Hispania inaonyesha kwamba usimamizi wa ardhi kame unaotumia taarifa sahihi, kwa kuzingatia kupishana kati ya matumizi ya malisho, ukulima na vipindi ya bila ya kuilima ardhi hupelekea si tu kusitisha kuwepo hali ya kuenea kwa jangwa lakini pia huleta uwezekano wa kurejesha ardhi kama ilivyokua awali. 
Hii ndio sababu Programu ya Kimataifa ya UNESCO ya Nishati-Maji imejikita katika kujenga uwezo na kutoa mwongozo wa sera na zana za kushughulikia ukame, kuenea kw jangwa na changamoto zinazotikana na hayo, hasa kuhusiana na usimamizi wa rasilimali maji, kwa njia ya Mtandao wa Kimataifa unaohusika na Maji na Maendeleo ya Taarifa ya Ardhi Kame (G- WADI). 
Pili, inatupasa kuimarisha ustahimilivu wa watu walio katika mazingira hatarishi kwa kuwawezesha kuwa na njia mbadala za kujipatia kipato ili tuweze kuuharibu mduara wa kuenea kwa jangwa na madhara yake ya kijamii na kiuchumi ambayo mara nyingi husababisha watu kuyahama makazi yao. 
Katika kutafuta na kuendeleza elimu na kujenga uwezo katika sayansi, teknolojia na uhandisi, kwa wasichana na wavulana katika nchi zilizo katika hatari zaidi, Programu ya Sayansi ya Msingi ya Kimataifa ya UNESCO inafanya kazi ya kujenga fursa mpya za ajira kwa vijana, kupunguza utegemezi wa rasilimali zinazotegema hali ya hewa, ili kuwapatia watu maisha yenye ustahimivu katika makazi yao. 
Katika siku hii, ni lazima tutambue kuwa hali ya kuenea kwa jangwa ni jambo la kimataifa ambalo linalomtishia kila mtu na ni lazima lishughulikiwe kwa pamoja ili kujenga mustakabali endelevu na imara kwa wote. Ujumbe kutoka kwa Bi. Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, 17 Juni 2017

UNESCO organize 3 day symposium to address gender gap in STEM subjects

Girls and women face multiple challenges that compromise their education opportunities. One area of longstanding concern is the low rate of female participation in science, technology, engineering and mathematics (STEM) education and consequently STEM careers. This is a major concern, as STEM careers are often called ‘jobs of the future,’ driving social and personal well-being, inclusive growth and sustainable development, through innovation and creativity.

Why does this gender gap exist and how can it be addressed? The UNESCO International Symposium and Policy Forum will be organized over three days, serving as a platform for debate and hands-on learning, seeking to: 


Present latest findings from research and practice 

Facilitate policy dialogue, experience-sharing and networking
Make the case for strengthening girls’ education in STEM subjects

The programme will be based on the overarching theme of girls’ education in STEM, with four sub-themes/tracks:


 Building the foundations: Gender-responsive quality STEM education

Changing the equation: Addressing stereotypes and bias hindering girls’ participation
Gravitating into the field: Reaching out, engaging and empowering girls and women
Wiring the network: Partnerships, cross-sector learning and cooperation

This event will bring together over 200 delegates including: the Ministry of education and other officials; education practitioners and educators; researchers and experts; representatives of intergovernmental and non-governmental organizations; development partners; civil society representatives; private sector stakeholders and others.


INTERESTED IN JOINING?
Participation will be by invitation only. Interested participants can register, submit a proposal for a presentation or a workshop, or reserve an exhibition booth online before 19 June 2017. To ensure a balanced audience, all requests will be evaluated based on profile, gender and geographical representation. 
Submit a request to reserve an exhibition booth (link is external)

UNESCO YATAKA WANANCHI KUENZI URITHI WA DUNIA KWA KUTEMBELEA

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova, katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo ametaka wananchi mbalimbali kutenga muda binafsi na kutembelea moja ya maeneo ambayo ni urithi wa dunia yakifadhiliwa na UNESCO.
Amesema anaamini kuwa kwa wananchi kushiriki watashawishika kuendelea kuishi kwenye maeneo hayo na kuyaenzi.
Amesema kitendo hicho kidhati kitakuwa kimewaunganisha watu na asili na hivyo kuondoa dhana ya zamani ya kuweka maeneo hayo mbali na watu.
“Inaweza kuwa vigumu kuamini sasa, lakini miaka hamsini iliyopita ilidhaniwa kuwa njia bora ya kulinda asili ni kuiweka mbali na watu ...Hii leo, tunajua vyema zaidi kwamba kwa kadri uhusiano baina ya watu na mazingira yao unavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo watu wanavyofahamu zaidi juu ya umuhimu wa asili na viumbe hai, urithi na maji, kwa ajili ya ustawi wao binafsi na kwa ajili ya hali ya baadaye ya sayari yetu.” Alisema.
Mkuu huyo alisema hayo akizungumzia umuhimu na uhifadhi kwa maeneio zaidi ya 2000 duniani ya bayongahewa, maeneo ya hifadhi ya jiolojia ya na maeneo ya Urithi wa Dunia yanayodhaminiwa na UNESCO.
Alisema maeneo hayo pamoja na kuhifadhi urithi wa dunia pia hutoa ajira kwa watu wanaoyazunguka na milango yake iko wazi kwa umma wote.
“Maeneo ya hifadhi ya jiolojia ni vitabu vilivyo wazi vya kihistoria ambavyo huturudisha nyuma mamilioni ya miaka. Hifadhi za Bayongahewa ni mahali ambapo jamii hukabiliana na changamoto za maendeleo kwa kuunda njia mpya za kijamii na uchumi endelevu. Maeneo ya hifadhi ya jiolojia na hifadhi za Bayongahewa huunganisha uhifadhi na elimu kwa mbinu mpya ya maendeleo endelevu, kama vile utalii wa mazingira na kilimo hai.” alisema katika ujumbe wake kwa dunia.
Aliwataka wananchi kuheshimu mazingira ya asili hutokana na uelewa.
Aliwataka wananchi kupitia katika tafakari ya kina kujitumbukiza katika Bustani ya Kiajemi ya Iran ambako maji hufanya ishara za maumbo ya mapambo mbalimbali.
Aidha alisema vyema kuona eneo la hifadhi ya jiolojia la UNESCO la Tumbler Ridge nchini Canada, na kuogelea katika maziwa ya Alpine yenye maji angavu kama kioo na kulala chini ya nyota.
Pia amewataka kufanya safari ya kutembea kwa miguu katika hifadhi ya Bayongahewa ya Mujib huko Jordan ambayo ipo mita 420 chini ya usawa wa bahari ikiwa karibu wake na Bahari ya Chumvi.
Mkuu huyo wa Unesco ametaka wakazi wa dunia hii wakati wakiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, kutumia ipasavyo maeneo teule ya UNESCO kila mahali kuungana na asili inayowazunguka na inayoleta uzuri, maana na amani katika maisha.

WASICHANA 8000 KUNUFAIKA NA MRADI WA UNESCO WA ELIMU

 Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA)nchini, Dk. Hashina Begum akitoa neno kwa niaba ya UNFPA.
  Msimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Tanzania, Bi. Hodan Addou akitoa neno kwa niaba ya UN Woman.
 Mkurugenzi wa Shirika lake la Kimataifa la misaada Korea International Cooperation Agency KOICA nchini, Joonsung Park akitoa neon kuhusu ufadhili wa KOICA ambao imeutoa katika mradi huo na mipango yao ya kusaidia Tanzania.
 Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji Dkt Leonard Akwilapo akifungua rasmi kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.
 Anna Holmström kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa washiriki waliohudhuria kongamano hilo.
 Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
 Washiriki wa kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Wasichana  8,000 waliopo shuleni na  600 ambao hawako shuleni watanufaika na mradi mkubwa wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana  kupata elimu.
Mradi huo wa miaka minne wenye gharama ya dola za Marekani milioni 5 utafanyika katika wilaya tano nchini.
Wilaya hizo ni Ngorongoro, Kasulu, Sengerema, Micheweni na Mkoani.
Mradi huo ambao upo hatua ya pili umeanza kwa kongamano lililofunguliwa jana na Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leonard Akwilapo.
Mradi huo mkubwa kwa mujibu wa Katibu mkuu huyo umelenga kuwaokoa wanafunzi  kabla hawajakumbwa na matatizo yanayokatisha masomo yao.
Aidha utawapa fursa za kuboresha zaidi mafunzo mbalimbali waliyonayo ambao utawafanya kuwa watu wazuri zaidi katika jamii na hivyo kuchangia maendeleo ya taifa na jamii walizopo.
Katibu mkuu huyo ambaye alifungua kongamano na kuzindua mradi huoi awamu ya pili alisema kwamba  ni matumaini yake kwamba jamii itaukumbatia mradi huo ili kuwa na taifa lenye mafanikio makubwa katika malengo ya maendeleo endelevu ya dunia kwa kuzingatia lengo namba tano.
Amewataka wazazi na vijana kutimiza wajibu wao kwa kubadilika kitabia na kutambua umuhimu wa elimu katika kufanikisha wanachotaka ambacho ni maendeleo binafsi , familia na taifa kwa ujumla.
Katika hotuba yake alisema ni matumaini kwamba wadau katika mradi huo watafaikisha katika kipindi cha miaka minne mipango yote iliyolenga kuboresha huduma kwa wasichana na wanawake vijana, kushawishi jamii kubadilika na kuachana na tamaduni mbaya kama ndoa za utotoni na ukeketaji.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni UNESCO, Zulmira Rodrigues  alisema mradi huo ulioanza mwaka jana na kufanyiwa tathmini umeonesha changamoto kubwa ya watoto wa kike ikiwamo mimba za utotoni,ukeketaji na kushindwa masomo.
Alisema lengo la mradi ni kuhakikisha kwamba mwanamke anapata fursa za kupambana katika mazingira yake kama anavyofanya mwanaume kwa kuwezeshwa na kuzuia mila, tabia na tamaduniu mbaya ambazo zinakwamisha uwezo wake wa kuhudhuria masomo.
Aidha alisema mradi huo utatoa nafasi kwa wanawake vijana ambao wamekosa masomo au wameacha masomo au hawakwenda shule kabisa kupata nafasi ya kusoma.
Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la kimataifa la misaada la Korea (KOICA) kupitia UNESCO na kufanyiwa kazi pia na mashirika ya UN Women na UNFPA unaangalia namna bora ya kukabiliana na changamoto za mabinti wanaokwenda shule katika wilaya hizo ili kuwawezesha kuwa watu bora katika jamii siku za usoni.
Mradi huo ni sehemu ya mradi wa Global Initiative unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO), Shirika la Mpango wa watu (UNFPA)  na Shirika la Umoja wa mataifa la wanawake(UN Women) wa kuwawezesha wanawake kupitia elimu uliozinduliwa katika nchi sita duniani.
Awamu ya kwanza ya mradi huo umelenga kufanywa katika nchi tatu za Mali, Nepal na Tanzania na ulitiwa saini mwaka jana, 2016.
Katika mradi huo  serikali ya Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto;  na Wizara ya Katiba na Sheria  ambayo ikiratibu mradi kwa niaba ya serikali ya Tanzania.
Aidha UNESCO inatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na UNFPA na UN Women.
Katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa  KOICA Tanzania, Joosung Park pia alizungumza umuhimu wa kufundisha watoto wa kike na kuwapa fursa na kusema kwamba unapofunza wanawake unafunza taifa huku akisema kwamba wazazi wanahusika sana katika hilo akitolea mfano waziri wa mambo ya nje wa Korea wa sasa ambaye ni mwanamke kwa mara ya kwanza katika miaka mingi ya historia ya nchi hiyo.
Mzungumzaji mwingine ni  ambaye alikuwa Mwakilishi wa  UNFPA Tanzania, Dk Hashina Begum alitaka jamii kuhakikisha kwamba inatoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuzuia uzazi usiokuwa na mpango ambao unakwamisha maendeleo.

TIBA MTANDAO KUANZIA OLOLOSOKWAN OKTOBA MWAKA HUU

WATU waliopembezoni ambao wamekuwa na shida kubwa ya kupata madaktari bingwa, wataanza kupata nafuu baada ya kuanza kwa mradi wa tiba mtandao unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili, UNESCO pamoja na wadau wengine.

Hayo yalisemwa katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza.

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.

Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.

Alikuwa anatarajia mifumo yote kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na nafasi ya kuwa katika matibabu ifikapo Oktoba. Katika warsha hiyo aliwahimiza wataalamu kujadiliana kiundani changamoto mbalimbali na namna ya kuweka ripoti ili kuja kusaidia wakati mradi utakapoenda kitaifa.

Katika warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa na Dk Liggyle Vumilia alielezea matumaini yake kuhusiana na mradi huo wa majaribio.

Aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuona uwezekano wa kuanza mradio huo mapema zaidi baada ya kuhakikisha kwamba dhana imekubalika na namna ya kuitekeleza inaeleweka miongoni mwa wadau.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya alipokuwa akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Mradio huo unaoanza kwa majaribio kufuatia juhudi za UNESCO zilizoanzishwa kwa msaada wa Samsung unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan na kwa kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa, masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza kufanya tiba kwa kutumia mtandao.

Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mnamo mwezi Novemba mwaka 2016.

Wataalamu hao kutoka Shirika la Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro, wataalamu kutoka KCMC na MUHAS wamekutana jana katika Kampasi ya Muhimbili (MUHAS), ili kuangalia dhana mpya kwa ajili ya utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao katika kijiji cha Wamasai, Mkoani Arusha cha Ololosokwan.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea jijini Dar Es Salaam


Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo.

Mradi huo ukifanikiwa unatarajiwa kupanuliwa kwenda sehemu mbalimbali zinazohitaji matibabu ya mabingwa lakini uwezo wa kufika huko haupo.

“Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,” alisema Zulmira na kuongeza kuwa dhana ya utabibu mtandao inalenga hasa kuinua utumiaji wa teknolojia ya kidigitali ya kisasa, ambapo utekelezaji wake utakuwa mfano elekezi wa kuboresha matumizi ya teknologia katika karne ya ishirini na moja katika utoaji wa huduma za afya nchini na barani Afrika.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akitoa neno katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.


Warsha inayochambua dhana ya tiba mtandao ni awamu ya pili yenye kuendeleza juhudi za kutumia uwapo wa huduma hiyo Ololosokwan kwa kuwakutanisha wabunifu, wataalamu wa afya na wanateknolojia ili kudadavua dhana ya utekelezaji kamilifu wa jaribio la utoaji wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na baadaye kuirasimisha kama mfumo wa kuboresha afya maeneo yaliyo pembezoni ya miji na vijijini.

Katika warsha hiyo washiriki walipata nafasi ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Unesco na MUHAS wa ushirikiano katika utekelezaji wa dhana hiyo ya tiba mtandao.
Akifafanua zaidi Dk Vumilia alisema kwamba tiba mtandao itahusisha upasuaji mdogo ambao utafanywa na wataalamu waliopo katika kliniki za kijiji hicho wakielekezwa na mtaalamu bingwa.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifuatilia kwa umakini hotuba mbalimbali zilizowasilishwa kwenye warsha hiyo.
Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen akifafanua jambo kwenye warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya kurasimisha ushirikiano wao katika uendeshwaji wa mradi mzima wa Kijiji cha Uvumbuzi wa Dijitali ya Afya. Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (kulia).
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda wakishuhudia Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kushoto) akiweka saini kama shahidi wa makubaliano hayo.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya wakibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya kurasimisha ushirikiano wao katika uendeshwaji wa mradi mzima wa Kijiji cha Uvumbuzi wa Dijitali ya Afya huku tukio hilo likishuhudiwa na wataalamu kutoka Shirika la Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro, wataalamu kutoka KCMC na MUHAS.

Picha juu na chini ni wataalamu kutoka KCMC, MUHAS wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, pamoja na Maafisa wa Afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro wanaoshiriki warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya (kulia) akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari wakati wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS) jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya.
Picha ya pamoja.

UNESCO KUENDELEA KUSAIDIA REDIO JAMII KUKUZA DEMOKRASIA

Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na vyombo vingine. Alisema kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa jamii kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila kufanya uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari badala ya kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi. 
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay akizungumza machache wakati wa mkutano mkuu wa wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

Aliwashauri wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa mtandao huo. “Ninawaomba sana, COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.

‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni” alisema Zulmira Rodrigues
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari jamii waliokutana kwenye mkutano mkuu ili kujadili changamoto na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya uliodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA, Prosper Kwigize alisema kuwa ipo changamoto kwa baadhi ya maafisa habari mikoani na wilayani kuleta urasimu mkubwa katika utoaji wa taarifa zinazohitajika kwa waandishi wa habari hivyo kukwamisha upatikanaji wa habri kwa umma. Pia kuna changamoto mbalimbali kwenye chama hicho hivyo ni vyema kuzitafutia suluhiso la msingi ili mtandao huwe imara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera alisema kuwa kwa siku za nyuma redio ilikuwa ni chombo cha kuaminika katika utoaji wa habari hivyo kujijengea umaarufu na kuaminika zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo kuna upotoshaji mkubwa. Pia aliweza kuyatolea majibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa bodi ya COMNETA ili kuimarisha uwajibikaji katika Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Prosper Kwigize akizungumza na viongozi wa vyombo vya habari jamii wakati wa mkutano mkuu wa COMNETA unaondelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya COMNETA, Balozi Christopher Liundi akizungumza jambo wakati wa mkutano mkuu Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa UNESCO.
Katibu wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Marco Mipawa akisoma marejesho kwenye mkutano mkuu unaondelea OUT jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya COMNETA ambao pia ni Mameneja na wawakilishi wa vituo vya redio jamii nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

Kutoka kushoto ni Afisa Programu wa Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Nancy Kaizilege na Mkufunzi wa Redio Jamii UNESCO, Rose Haji Mwalimu wakirekodi mambo muhimu katika mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea.

NDALICHAKO KUMALIZA MIGOGORO YA WALIMU KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA NYINGINE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


  Mwenyekiti wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akiendesha mjadala wa kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili wa wadau wa elimu kutoka nchi 13 uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conventional Centre (JNICC) jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige)
Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, iliyona makazi yake nchini Marekani akielezea kuhusu mradi wa XPRIZE unahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao ukilenga watoto wa miaka 5-12 wakati wa kuhitimisha mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akielezea jitihada zitakazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu kuelekea utekelezaji wa SDG4 kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Elimu, Rasilimali Watu na Tafiti za Kisayansi wa Mauritius, Leela Dookon Luchoomon (kushoto) akieleza mipango ya serikali yake katika kuboresha elimu wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank.
 Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles akizungumza kwa niaba ya nchi wahisani wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Djibouti, Mh. Moustapha Mohamed Mahamoud akiwasilisha mapendekezo ya serikali yake katika kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Waziri wa Elimu na shule za msingi wa Uganda, Mh. Nansubuga Rosemary Seninde (kulia) akitoa mapendekezo ya serikali yake katika kuboresha elimu kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mh. Mhandisi Stella Manyanya (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo wakiandika mapendekezo muhimu yaliyokuwa yakiwasilisha kwenye mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.

 Sehemu ya mawazi wa elimu kutoka Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia, Somalia, Comoro na Djibouti walioshiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
  Sehemu ya wadau wa sekta ya elimu kutoka nchi 13 walioshiriki kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Mwenyekiti wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa na wadau wa sekta ya elimu wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) walioshiriki kufanikisha mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo (kushoto) akijadiliana jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.


Na Zainul Mzige
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba wizara yake itashirikiana na wizara nyingine nchini kuhakikisha kwamba migogoro ya walimu inamalizwa ili kufanikisha utoaji wa elimu kuwa bora na jumuishi.
Kauli hiyo aliitoa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika siku ya pili ya kuhitimisha kwa mkutano ulioshirikisha nchi 13 za Afrika Mashariki kujadili lengo la nne la elimu kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs)
Alisema kwamba migogoro ya walimu inayogusa mishahara, marupurupu pamoja na mazingira bora ya kazi linagusa pia Wizara za TAMISEMI na UTUMISHI na kusema kwamba wao kama wasimamizi wa elimu watakachoweza kufanya ni kuzungumza na wenzao kuhakikisha kwamba migogoro hiyo inafutwa ili utoaji wa elimu uendane na mipango ya kitaifa na kidunia ya lengo la maendeleo 2030.
Pamoja na kujibu swali hilo Prof Ndalichako alizungumzia  kwamba walimu walikuwa ni ajenda muhimu  na humo walikubaliana kwamba mwalimu ni kila kitu katika utoaji wa elimu na kuwa hawawezi kufanikiwa katika elimu bora na jumishi bila kuwa na walimu wenye umahiri, wanaowezeshwa kufanya hivyo.
Kutokana na ukweli huo wamejipanga kuhakikisha kwamba walimu wanapata mafunzo bora na kuwakutanisha kubadilishana uzoefu.
Alisema kila nchi itakuwa na mpango mkakati wake na kuonesha viashiria kwamba vinatekelezwa kwa namna gani. Mwisho wa siku mwaka 2030 mataifa yote yanapaswa kuhakikisha kwamba agenda namba 4 ya maendeleo endelevu ya elimu imetekelezwa.
Alisema katika mkutano huo wa siku mbili wa mawaziri wa elimu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank wamebainisha kwamba mikakati ya pamoja ni lazima ichukuliwe ili kufanikisha elimu jumuishi yenye usawa na ubora kwa watu wote huku ikitoa fursa ya elimu kwa wakati wote.
Alisema kwamba mkutano ulitambua kwamba elimu haina mwisho, elimu inataka kuwa na mfumo wa kuwa na maendeleo ya kujifunza kwani mambo hayasimami kutokana na kubadilika kwa teknolojia, hivyo elimu inayotolewa haina budi kujazia nafasi hiyo kwa kuwapa uhuru watu kujisogeza zaidi.
Alisema nchi hizo 13 zimekubaliana kwa pamoja kufikia malengo endelevu 2030 kama yalivyosainiwa na kila nchi mwaka 2015 kwa kuweka mikakati ili mataifa hayo yaweze kufikia malengo yanayotakiwa.
Aidha alisema kama walikubaliana kwanza kuimarisha elimu ya awali kwa lengo la kuweka msingi wa kujifunzia, kwani ipo methali inayoaminika kwamba samaki mkunje angali mbichi na taifa likitaka watoto wasome ni lazima kuwaanzia wadogo.

Aidha  mataifa hayo yamekubaliana upimaji wa wanafunzi kufanyika kwa ajili ya kujifunza, ukilenga kutumia matokeo kuandaa mafunzo kwa wanafunzi. Upimaji uoneshe eneo la ambalo walimu watalazimika kufanya kazi ya ziada ili wanafunzi wao waelewe.
Mfumo wa sasa wa kupima umelenga kujua watoto wangapi wamefaulu na wangapi wamefeli.
Ndalichako alisema ni vyema upimaji huo kutumika kuimarisha mafunzo ya walimu.
Jambo la tatu ambalo walikubaliana ni kuhakikisha kwamba mtoto wa kike anasoma na wale wenye mazingira hatarishi pia; na bila kujali kujali mazingira yao nchi zinatakiwa kuweka mikakati ya  elimu iliyobora kwa wote.
"Suala muhimu katika elimu ni kupanga mipango sahihi. Takwimu sahihi ni changamoto kutokana na ukweli kuwa takwimu hazipatikani kwa wakati au hazina usahihi au hazifanyiwi uchambuzi katika kufanya maamuzi vizuri, " alisema Prof Ndalichako.
Pia mataifa hayo yakiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia, Somalia, Comoro na Djibouti yamesisitiza haja ya kuimarisha elimu nje ya mfumo rasmi na kwa kuwa kuna mfumo wa elimu wa kujiendeleza wa wakati wote mfano wa uhasibu.
Alisema inafaa kuimarisha mifumo ya elimu nje ya mfumo rasmi bila kusahau elimu ya watu wazima. Pia wametaka watoto wanaolikoroga kwa sababu moja au nyingine na kujikuta hawapati masomo ni vyema wakarudishwa shuleni kuendelea na masomo hivyo ipo haja ya kutengeneza mfumo wa kupata elimu kwa staili hiyo.

"Katika hili tumekubaliana watoto walionje ya shule wanarudi shuleni au wanatengeneza mfumo wa kupata elimu" alisema na kuongeza kuwa pia ilionekana ipo haja ya kuimarisha elimu na ufundi stadi ili elimu hiyo imwezeshe kujiajiri, kujijenga na kuwa na ujuzi kuendana na soko la ajira.
Aidha alisema kwamba  kunatakiwa kuanzishwa kwa kampeni maalumu ya kufichua wasichana wasiopelekwa shule ili kuwepo mwenedelezo wa kila mtu kuingia shule.
WAKATI huo huo serikali ya Uganda imesema itaongeza nguvu katika shule za awali kuimarisha msingi wa utoaji elimu kwa watu wake.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na shule za msingi wa Uganda, Mh. Nansubuga Rosemary Seninde wakati akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki kuhusiana na lengo namba 4 la elimu kati ya malengo 17 ya dunia.
Alisema serikali yake imejikita katika kuhakikisha kwamba waganda wanapata elimu nzuri na yenye ushindani ikihakikisha ujuzi na uzoefu katika ujuzi.
Aklisema nchi yake haiwezi kumpa mtu digrii mpaka awe amefanya “intern” na hilo linasaidia sana kujenga uzoefu wa kile alichosomea.
Alisema ingawa kuna tatizo la bajeti, mipango ni muhimu kuhakikisha kwamba taifa linatoka katika changamoto za utoaji wa elimu bora.

Alisema badala ya kusubiri sera, watendaji wanatakiwa kuangalia maeneo ya kuanzia na kisha kutengenezea taratibu za kubadilishwa kwa sera ili iendane na kasi inayotakiwa.