HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

RC RUKWA ASHAURI NANENANE NYANDA ZA JUU KUSINI KUSHIRIKISHA NCHI ZA SADC

RC Rukwa akijaribu kuendesha moja ya Trector za John Deere katika maonyesho ya Nanenae Mbeya
RC Rukwa (kushoto aliyevaa miwani) akipokea maelekezo kutoka katika moja ya mabanda ya SAGCOT

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa KamishnMstaafu Zelote Stephen ameishauri kamati ya maandalizi ya nanenane nyanda za juu kusini kufikiria kushirikisha nchi za SADC ili kuongeza hamasa na kuleta ushindani kwa watanzania wafahamu yanayofanyika katika nchi za jirani.

Ametoa ushauri alipokuwa akifanya majumuisho baada ya kutembelea mabanda 16 ya bidhaa mbalimbali za kilimo katika maonesho ya nane nane kwa kanda ya nyanda za juu kusini yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya ambapo Mh. Zelote Stephen alikuwa mgeni rasmi wa siku ya tatu tangu ufunguzi wa maonesho hayo. 

“Tuachane na mazoea, maonyesho haya yana miaka 25 sasa tuyaboreshe zaidi, isiswe ni mikoa hii tu saba, tupanue wigo, kwakiwa huku ni nyanda za juu kusini basi tufikirie kuzishirikisha nchi za SADC ambazo zitasaidia kubadilishana biashara na teknolojia pamoja na kutafuta masoko,” Alifafanua. 


Akisisitiza suala hilo Mh. Zelote alibainisha kuwa nchi ya Tanzania inafikika kwa njia zote, ardhini, majini na angani huku akitaja meli mbili zilizozinduliwa Mkoani Mbeya na Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa, treni ya TAZARA pamoja na ndege zinazomilikiwa na nchi yetu. 

Aidha amezishauri halmashauri kuanza maandalizi kwa kuwa na siku maalum kwaajili ya maadhimisho hayo kihalmashauri ili kuwapa ujuzi na kujua ubora wa vitu ambavyo vinaweza kupelekwa kwenye maadhimisho ya nanenane kikanda ili kuimarisha ushindani na kumpa kila mwananchi nafasi ya kuelimika ili kuwa na kilimo chenye tija.

Akiunga Mkono Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mh. Kilolo Ntila alityekuwemo katika msafara huo alisisitiza kuwa maonesho ya nanenane yanayofanyika kikanda yanalenga watu wenye kipato cha kutoka katika halmashauri zao na kukusanyika jijini Mbeya huku wakulima wasio na uwezo wakikosa elimu inayopatikana kutokana na maonyesho hayo.

“Nikiongezea aliyoyasema Mheshimiwa Mkuu wangu wa Mkoa, kwa nafasi yake namuomba aweze kushawishi haya makampuni makubwa kuweza kusambaza wataalamu wao katika Halmashauri zetu ambapo kuna uhitaji mkubwa wa elimu hii inayotolewa hapa katika viwanja hivi vya nanenane na wao ndio walengwa wakubwa wa shughuli hii,” alisema.


Pamoja na hayo Mh. Zelote alitoa wito kwa wananchi wote wenye nafasi wajitokeze kwa wingi kwenye maonyesho hayo ili waweze kuelimika kutokana na mafunzo mbalimbali yanayotolewa viwanja hivyo vya nanenane na kusifu maandalizi ya sherehe hizo.

UFUNGASHAJI BIDHAA KUWAINGIZA AKINAMAMA KWENYE SOKO LA USHINDANI

Mwezeshaji wa mafunzo ya nembo na vifungashio, Emmanuel Bakashaya, akifundisha akinamama wa Green Voices jinsi nembo na vifungashio vinavyopaswa kuonekana.
Akinamama wa Green Voices wakiwa katika ofisi  za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakijifunza kutoka kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Raymond Wigenge, hivi karibuni.
Green Voices katika majadiliano ya vikundi juu ya njia mbali mbali za kutafuta rasilimali wakati wa mafunzo chini ya mwezeshaji Richard Jackson. 
Green Voices wakiangalia bidhaa za ujasiriamali za Mama Rocky (mwenye mtandio wa buluu) katika supermarket. Hii ni baada ya kumtembelea kiwandani kwake katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) jijini Dar es Salaam.
Dkt. Alicia Cedaba, Meneja wa Mradi wa Green Voices kutoka Hispania, akifundisha akinamama wanaotekeleza mradi huo nchini Tanzania. 
Akinamama wa Green Voices wakiwa katika mafunzo kwa vitendo katika makao makuu ya SIDO jijini Dar es Salaam.
Green Voices baada ya kuhitimu mafunzo. Walioketi kutoka kushoto ni Mratibu wa Green Voices nchini Tanzania, Secelela Balisidya, Mkurugenzi wa taasisi ya IMED iliyotoa mafunzo, Dkt. Donath Olomi na Meneja wa Mradi wa Green Voices kutoka Madrid, Hispania, Dkt. Alicia Cebada.


AKINAMAMA wanaotekeleza mradi wa Green Voices nchini Tanzania sasa wanalenga kuboresha bidhaa za kilimo wanazozalisha ili kuongeza tija ikiwa ni katika azma yao ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Wakizungumza baada ya semina ya wiki moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, akinamama hao walisema elimu waliyoipata imewapa mwanga wa kuendeleza miradi yao na kuhakikisha wanaboresha bidhaa zao ili ziwezi kuingia katika soko la ushindani.
Miradi inayotekelezwa kupitia Green Voices Tanzania ni kilimo cha mihogo, kilimo cha matunda, uyoga, ufugaji wa nyuki, ukaushaji wa mbogamboga na utengenezaji wa majiko rafiki wa mazingira ambayo inatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Kigoma, Mwanza na Kilimanjaro.
“Nilikuwa nimekata tamaa nisijue nitauendelezaje mradi wangu, lakini kwa mafunzo niliyoyapata kutoka kwa wataalam mbalimbali, hakika nimehamasika na kuona kwamba ninaweza kusimama na kusonga mbele,” alisema Farida Makame ambaye anasimamia mradi wa Majiko ya Umeme-Jua mkoani Kilimanjaro.
Farida alisema amehamasishwa zaidi na mafunzo hayo, ambayo yamempatia mbinu mpya zaidi za kuendeleza mradi huo kwa wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Abiah Magembe anayesimamia mradi wa Usindikaji wa Muhogo na Mtama katika Kijiji cha Kitanga, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, amesema mafunzo ya jinsi ya kufungasha na kuweka nembo kwenye bidhaa yamempa mwanga mkubwa na kwamba sasa yeye na wenzake watazalisha bidhaa zao kwa kujiamini na kuziingiza kwenye soko la ndani na la kimataifa.
“Tunatengeneza bidhaa nyingi zinazotokana na muhogo na zina viwango vizuri, lakini kwa mafunzo tuliyoyapata, sasa tunaweza kuziboresha kwa kuhusisha taasisi husika kama Shirika la Taifa la Viwango (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ili tuingie kwenye ushindani wa kitaifa na kimataifa,” alisema Bi. Magembe.
Bi. Magembe alisema kwamba, bidhaa wanazozalisha kutokana na zao la muhogo ni unga unaotumika kwa uji na ugali, vitafunwa kama keki, mikate, skonzi, biskuiti, mandazi, sabuni ya unga pamoja na bidhaa nyingine nyingi.
Mazao mengine yanayopatikana katika muhogo ni mzizi wenyewe ambao unatafunwa mbichi au ukiwa umepikwa au kukaangwa, kwenye futari, miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai za viwandani kama vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na plastiki wakati ambapo wanga (starch) hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup).
Takwimu za kilimo cha muhogo duniani zinaonyesha kuwa, Afrika ni bara la tatu duniani kwa kuzalisha zaidi muhogo ambapo huzalisha takriban tani milioni 102.6 kila mwaka.
Tanzania ni nchi ya nne kati ya wazalishaji wakubwa wa muhogo barani Afrika baada ya Nigeria, Ghana na Congo DRC ambapo inaelezwa kwamba karibu ekari 670,000 za ardhi ya kilimo zinatumika kuzalisha muhogo, zao linalochangia karibu asilimia 15 za chakula kwa nchi nzima na karibu kaya 1,213,958 huzalisha muhogo nchini.
Regina Kamuli ambaye anasimamia mradi wa Majiko Banifu wilayani Mkuranga, alisema anashukuru wanakikundi wenzake wamejizatiti na sasa wanapata fursa ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali yakiwemo ya kilimo kuonyesha majiko hayo ambayo ni rafiki wa mazingira.
“Hivi sasa baada ya kikundi kusajiliwa akinamama wamenufaika na mikopo nafuu kutoka Halmashauri ya Wilaya na kwa mafunzo haya tutaboresha majiko yetu ili tuyanadi katika maeneo mengi nchini Tanzania kwa sababu yanatumia kuni kidogo, hivyo kuokoa mazingira,” alisema Regina.
Magdalena Bukuku anaongoza kikundi cha akinamama wanaoshiriki Kilimo cha Uyoga huko Bunju jijini Dar es Salaam, ambapo anasema mafunzo ya ufungashaji na uwekaji wa nembo yamempa mwanga mkubwa ili kwenda kuboresha bidhaa zao ziingie kwenye ushindani.
“Tunazalisha uyoga kwa wingi kwa sasa na wateja wameongezeka, hata hivyo, ikiwa tutafungasha vizuri na kupanua kilimo chetu tunaweza kulifikia hata soko la kimataifa,” alisema.
 Mariam Bigambo na Monica Kagya wao wanashiriki ufugaji wa nyuki ambapo mbali ya kuvuna asali, lakini wanasaidia kutunza mazingira na kuongeza tija katika mazao ya kilimo kutokana na uchavushaji.
Wakati Mama Bigambo anaendesha Ufugaji wa Nyuki huko Dakawa, Morogoro, Bi. Monica yeye na akinamama wenzake wana jukumu kubwa la kutunza misitu ya Pugu na Kazimzumbwi wilayani Kisarawe kutokana na Ufugaji wa Nyuki.
“Tunataka tujikite katika kufungasha vizuri asali na kuziwekea nembo ili tuingie kwenye ushindani,” walisema.
Suala la ufungashaji na uwekaji wa nembo nalo limewagusa Esther Muffui, Dkt. Sophia Mlote na Leocadia Vedasto ambao wanashiriki katika kilimo na ukaushaji wa mboga na matunda.
“Tunajihusisha na Ukaushaji wa Mboga na Matunda kule Morogoro, sasa tulikuwa tunashindwa kufungasha vizuri, naamini tumepata mwanga wa namna ya kufungasha bidhaa zetu ili tupate tija zaidi,” alisema Bi. Esther.
Leocadia yeye anashiriki mradi wa Kilimo na Usindikaji wa Viazi Lishe huko Ukerewe mkoani Mwanza wakati Dkt. Mlote anashiriki mradi wa Kilimo Hai cha Nyanya na Mbogamboga Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Naye Evelyn Kahembe ambaye anaendesha Kilimo cha Matunda huko Uvinza, Kigoma, amesema mafunzo hayo yamemuongezea ujasiri wa kuendeleza mradi huo akishirikiana na wanawake wengine huko Kigoma.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Green Voices Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, alisema mafunzo waliyoyapata yametoa mwanga mkubwa kwa washiriki na kuleta mtazamo wa kibiashara zaidi tofauti na hapo mwanzo.
“Suala la ufungashaji wa bidhaa ni la muhimu na imekuwa vyema tumepata mafunzo ya kina pamoja na kutembelea taasisi kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) pamoja na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), tumejifunza mengi ambayo yamebadili mtazamo wetu,” alisema Secelela.

DR. MENGI ATAKA EAC KUTUMIA UTAJIRI WAKE KUTENGENEZA MABILIONEA

MWENYEKITI wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi amezitaka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kutumia utajiri wake mkubwa wa raslimali kunufaika kiuchumi. Ushirikiano huo ni pamoja na kuzindeleza raslimali hizo na kutumia nembo moja ya kibiashara ili kuzalisha mabilionea wakubwa duniani. Mwenyekiti huyo alisema hayo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.
Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi akizungumza wakati akifungua mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kutoa wito huo Dk Mengi pia amempongeza Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli pamoja na serikali yake kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya. Aidha alisema dhamira yake ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda itasaidia kuwakwamua Watanzania kutoka katika umaskini. Katika mazungumzo hayo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania –TPSF Dr Reginald Mengi na Ujumbe wa Kenya umeongozwa na Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor. Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi kwa kutoa risala nzuri ya ufunguzi wa mkutano huo.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye amesema mkutano huo umeitishwa kutokana na kujitokeza vikwazo vya kufanya biashara baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, jambo linalokwamisha malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kujenga uchumi unaoongozwa na sekta Binafsi. Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa KEPSA Bw. George Owuor amesema Wafanyabiashara wa Kenya wanapenda sana kushirikiana kibiashara na wenzao wa Tanzania, na wangependa kuona vikwazo vinavyokwamisha mahusiano ya kibiashara vinaondolewa. Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akiwasilisha mada kuhusu kupunguza pengo la biashara kati ya Tanzania na Kenya na kutumia fursa zilizopo na kutanua biashara nje ya mipaka katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Meneja anayeshughulikia Utafiti, Uchambuzi na Sera wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA, Victor Ogalo (kushoto) akitoa mada kuhusu changamoto za kisera za Tanzania na Kenya katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia walioketi ni Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi wakifuatilia kwa umakini mada hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alaska Tanzania, Jennifer Bash wakifuatilia mada mbalimbali zikizokuwa zikiwasilishwa ukumbini hapo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ujumbe wa Tanzania na Kenya ulioshiriki mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption] Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi katika mkutano huo. Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye akijibu maswali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi.

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta,Petrol, Dizel zashuka, Mafuta ya taa yapanda

Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zinaanza kutumika kesho ambapo bei ya mafuta ya Petroli imeshuka kwa shilingi 36 kwa lita, Dizeli ikishuka kwa shilingi 44 kwa lita, ilihali bei ya mafuta ya taa ikipanda kwa shilingi 24 kwa lita.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Titus Kaguo amesema bei hizo ni kwa mafuta yanayopakuliwa jijini Dar es Salaam, ili hali yale ya mkoani tanga yakibakia bei yake ileile ya mwezi uliopita.

WANA-ARUSHA WAFURIKA KATIKA AMSHA AMSHA YA KUCHANGAMKIA FURSA ZA SOKO LA EAC

Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (The Foundation for Civil Society-FCS), Bw. Francis Kiwanga alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi Arusha kwa ajili ya kufungua kongamano la siku moja la kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa za kibiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kongamano hilo ambalo lilikuwa na kaulimbiu "Chungulia fursa Boda to Boda" liliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, FCS na Clouds Media kwa udhamini wa Trademark East Africa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa ambapo pia alieleza sababu za kufanya kampeni ya kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za EAC. Bw, Kiwanga alisema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na FCS na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam zimebaini kuwa wastani wa vijana asilimia 11 katika nchi za EAC hawana ajira na asilimia 59 hawana taarifa kuhusu fursa zilizopo katika Jumuiya hiyo. Hivyo, Kongamano hilo ni kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu fursa zilizopo ili vijana waweze kujiajiri. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega akisoma hotuba ya ufunguzi ambapo alisisitiza umuhimu wa vijana kung'amua fursa mbalimbali na kubuni bidhaa zitakazokidhi soko la EAC lenye watu zaidi ya 150. 
Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria kongamano hilo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi. 
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Richard Kaisi akitoa neno ambapo alihimiza vijana kujifunza elimu ya ufundi wa aina mbalimbali ili waweze kuwa wabunifu wazuri kutokana na teknolojia ya kisasa. 
Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akitoa maelezo kuhusu sheria, kanuni na taratibu za kufuata endapo mtu anataka kufanya biashara katika nchi za Afrika Mashariki. Aidha, alisisitiza umuhimu wa vijana kujiunga katika vikundi ili iwe rahisi kupata huduma kama za mikopo. 
Watu wa makundi mbalimbali walishiriki kongamano hilo wakiwemo watu wenye mahitaji maalum. Pichani mlemavu wa masikio akipatiwa tafsri kwa lugha ya alama wa masuala yanayojiri katika shughuli hiyo. 
Huwezi kufanya biashara katika nchi za EAC bila ya kuwa na Hati halali ya kusafiria. Pichani ni Bw. Suleiman Masoud, Afisa wa Uhamiaji akitoa maelezo namna ya kupata Hati ya Kusafiria. 
Mlemavu wa macho akitoa maoni yake na kuuliza swali kwa watoa mada. Alidai kuwa taasisi za Serikali ndio zinakwamisha na kuwachelewesha Watanzania wasiweze kuchangamki ipasavyo fursa za EAC kutokana na ukiritimba usiokuwa na sababu. 
Kama kawaida ujumbe ulifikishwa kwa njia tofauti. Pichani ni wasanii wa bendi ya Cocodo wakicheza wimbo wa kuhamasisha biashara za kuvuka mipaka. 
Vijana walifuatwa katika maeneo yao mtaani ili kufikishiwa neno la kuwahamasisha kufanya biashara za kuvuka mipaka ndani ya EAC. Pichani ni Mtaalmu wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Abel Maganya akiwahamasisha vijana wanaofanya biashara zao kando ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. 
Sehemu ya watu waliohudhuria wakisikiliza neno kutoka kwa Bw. Maganya. 
Hamasa kwa njia ya muziki 
Bw. Kisoka akisisitiza vijana waondoe hofu na wajiunge katika vikundi na Serikali ipo nyuma yao kuwaunga mkono. 
Wafanyabiashara wa Soko la Mbauda wakisikiliza ujumbe kwa makini. 
Binti huyo akitoa ujumbe kwa njia ya ngojera ili mradi watu wahamasike na kuona umuhimu wa kujikwamua kimaisha kwa kufanya biashara za kuvuka mipaka. 
Kinanda na gitaa vilipigwa kwa ustadi mkubwa na kutoa ujumbe kwa Watanzania wasibweteke kwani fursa zipo lukuki katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

DKT. MPANGO ATANGAZA MAPATO KODI YA MAJENGO SHILINGI BILIONI 32.5.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akivipongeza Vituo vya Mafuta vya Puma na Total kwa kuonesha mfano wa kufunga mashine za EFDs katika Pampu zote za mafuta kwenye vituo vyao, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.  (Picha: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwaomba wananchi kulipa kodi ya Majengo mapema kwa mwaka wa Fedha 2017/18 ili kuepuka usumbufu wa msongamano, alipofanya Mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akitoa agizo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha kuwa mashine za kutolea risiti za kielektroniki (EFDs) zinatumika ipasavyo na kutengenezwa mara moja zinapoharibika na kwamba zisipotengenezwa ndani ya saa 48 zifungwe na wamiliki wake watozwe faini, alipozungumza na wanahabari, Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) ambapo Waziri huyo aliwashukuru wananchi kwa kulipa kodi ya Majengo kiasi cha Sh. Bilioni 32.5 kufikia Julai 15, 2017, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam.

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam 
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Sh bilioni 32.5 ya kodi ya majengo, kwa mwaka wa fedha 2016/17 kutoka katika Majiji, Miji na Manispaa 30 nchini. 


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) amewaambia waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kwamba makusanyo hayo ni sawa na asilimia 56 ya lengo lililowekwa Mwaka wa Fedha uliopita la kukusanya shilingi bilioni 58. 

Alisema kuwa hatua niyo ni mafanikio makubwa tangu TRA ipewe jukumu la kukusanya kodi hiyo ambapo mwaka wa fedha 2015/2016 katika maeneo hayo, Halmashauri zilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 28.3 wakati TRA imekusanya kiasi hicho cha shilingi bilioni 32.5 tangu ianze kukusanya kodi hiyo mwezi Oktoba mwaka wa fedha 2016/2017. 

“Mpaka kufikia tarehe 15 Julai mwaka huu TRA imekusanya sh. bil 32.5 kipindi ambacho ni kifupi, na kwamba mapato hayo yanatarajiwa kuongezeka kutokana na mwitio mkubwa wa wananchi kulipa kodi ya majengo”Alisema Dkt. Mpango. 

Dkt. Mpango aliwapongeza wananchi kwa mwitio wao mkubwa wa kulipa kodi ya majengo na kwamba wameonesha uzalendo wa kweli na ndio maana Serikali imeamua kuongeza muda wa kulipa kodi hiyo bila adhabu hadi Julai 30 mwaka huu, hali anayoamini itapandisha zaidi mapato hayo. 

Katika hatua nyingine Dkt, Philip Mpango aliwapongeza wamiliki wa vituo vya mafuta waliotii maagizo ya Serikali, kwa kufunga mashine stahiki za EFDs, akitolea mfano vituo vya PUMA na TOTAL ambavyo vimefunga mashine hizo kwenye pampu zao zote. 

Aliwaonya wamiliki wote wa vituo vya mafuta ambao hawatafunga mashine hizo za EFDs ndani ya siku 14 kama agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli linavyoelekeza na kwamba yeye kama Waziri mwenye dhamana atahakikisha analisimamia kikamilifu na kwamba baada ya muda huo mtu asijekuilaumu Serikali baada ya kuanza kuchukua hatua kali za kisheria. 

Aliwataka wamiliki wa vituo hivyo kupitia chama chao cha wamiliki wa vituo vya mafuta TAPSOA kuheshimu maelekezo ya Serikali na kuacha majibizano yasiyo na tija kuhusu amri hiyo ya Rais kwenye vyombo vya habari kwa kuwa huo ni utovu wa nidhamu. 

Aliwageukia wenye maduka ya vifaa vya ujenzi, vileo na maduka makubwa ‘supermarket’ nao watumie mashine hizo za kukusanyia mapato ya Serikali (EFDs) kikamilifu na kutoa risiti kwa wateja wao huku akiwaasa wateja nao kudai risiti wanapofanya manunuzi kulingana na kiwango halisi cha bidhaa wanazonunua. 

Alipiga marufuku wafanyabiashara wanaosingizia mashine za EFDs kuwa mbovu na kuwaonesha wateja wao makaratasi waliyotoa taarifa TRA kwamba mashine zao zilikuwa mbovu kwa kipindi kifrefu na kuaigiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kusimamia jambo hilo ili kuhakikisha kuwa linakoma kabisa. 

“TRA mtimize majukumu yenu mliyodhaminiwa na Serikali na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara ambao mashine zitakuwa hazitumiki ndani ya saa 48 kwa kisingizio cha kuharibika zifungiwe na wamiliki watozwe faini na kulipa kodi ya Serikali ipasavyo” aliagiza Dkt. Mpango. 

“Serikali ya Awamu ya Tano haijaribiwi, tumeazimia tutafanya kazi kwa niaba ya wanyonge ili nchi yetu iende mbele na kwa hili watusamehe.” Alisisitiza Dkt. Mpango 

Dkt Mpango alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kujitoa kwake kuwatumikia wananchi na kuongoza mapambano ya uchumi yatakayo ifikisha nchi kwenye uchumi wa kati ambao hata watu wa kawaida watajisikia kuwa unakua kwa kutatua changamoto zao za maisha. 

Alisitiza watanzania wafanye kazi kwa bidii kujenge nchi ili kila Mtanzania apate huduma bora, barabara bora, tiba nzuri, maji, yote haya hayawezi kufanyika bila mapato yakutosha na kwamba Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe.

MAENDELEO PAMOJA NA WEWE


 Maendeleo Bank pamoja na wewe. Bank ya Maendeleo leo imezindua promosheni iitwayo Maendeleo pamoja na wewe. Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba alisema “  Leo tumekutana hapa kwa ajili ya tukio fupi tu la kuzindua rasmi promosheni tuliyoipa jina la Maendeleo Bank pamoja na wewe”.

Aliongeza kusema “Promosheni ya Maendeleo Bank pamoja na wewe ni mahususi kwa wateja waliopo au wapya. Kama mnavyojua Maendeleo Bank imeanzishwa miaka 4 iliyopita na imepiga hatua kubwa sana; Tumeongeza matawi kutoka moja hadi 3 ambayo ni Luther House, Mwenge na Kariakoo, tumebuni bidhaa nyingi, tumepata faida nzuri katika kipindi kifupi hadi kufikia Milioni 550, Amana za benki zimeongezeka hadi kufikia Bilioni 34,tumetoa mikopo inayofikia Bilioni 27 tumeajiri wafanyakazi 63, na kama tutaruhusiwa na CMSA tunatarajia kukaribisha wanahisa wapya kupitia Soko la awali yaani IPO hivyo kukuza wigo wa umiliki wa benki na mtaji wa kufanya mambo mengi zaidi”.

alimalizia kwa kusema , Sisi kama benki yenye kulenga kuwapa wateja wetu Maendeleo tunawapa wateja watakaofungua akaunti za akiba au timiza nafasi yakujishindia ; Viwanja, tani za cement, mabati au ada za shule kwa wale watakao fungua au kuweka amana kwenye Maendeleo Junior.
Promosheni hii ni ya miezi 3.

GARI INAUZWA

Toyota Landcruiser for Sale (Mwanza)
*Year 2000
*Used in Tanzania
*Diesel
*Automatic
*55 Milion (Negotiable)


‘COCA-COLA BILA SUKARI’ YAZINDULIWA KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO MWANZA

Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Sia-Louise Shayo akizungumza na umati wa wasambazaji na mawakala wa soda ya Coca-Cola jijini Mwanza wakati wa hafla maalumu ya uzinduzi wa kinywaji kipya cha ‘Coca-Cola Bila Sukari’. Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda cha Nyanza Bottlers mkoani Mwanza, ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya.

Kampuni ya Coca-Cola leo imezindua katika soko la Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, soda mpya ya “Coca-Cola Bila Sukari”. Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda cha Nyanza Bottlers mkoani Mwanza, ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa Dar es Salaam na Mbeya ambapo awali ulifanyika mjini Moshi .
Soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari’ ladha yake imeboreshwa zaidi kutokana na soda isiyo na sukari iliyokuwa inatengenezwa hapo awali ya Coca-Cola Zero ambapo soda mpya ladha yake inashabihiana na soda ya Coca-Cola asilia lakini haina sukari kabisa.
Tangia mwaka 2006 wakati soda ya Coke Zero imeingia kwenye masoko, kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha inatengeneza soda mpya ya Coca-Cola isiyo na sukari lakini yenye ladha sambamba na Coca-Cola asilia na imefanikiwa kuja na soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari’ kinywaji ambacho kitawezesha watumiaji wa Coca-Cola kuipata kwa ladha asilia hata kama watachagua kuipata isiyotengenezwa kwa sukari.
“Soda ya Coca-Cola Zero ina ladha nzuri pia, lakini pamoja na ubora wake timu ya Coca-Cola imekuwa ikifanyia kazi kuhakikisha inapatikana soda isiyo na sukari lakini yenye ladha inayoshabiana na Coca-Cola asilia”. Alisema Meneja Mauzo Mwandamizi wa Nyanza Bottlers, Deus Kadico.
Kadico aliongeza kuwa; “Ubunifu wa wataalamu wetu umewezesha kupatikana soda mpya ya ‘Coca Cola Bila Sukari’ ambayo inatoa wigo kwa wateja kuwa na chaguo la kupata kinywaji cha Coca-Cola kwa radha asilia kwa kadri wanavyotaka,ikiwa na ladha ya sukari ama isiyo na sukari”.
Pamoja na hayo, Kadico alisisitiza kuwa lengo kubwa ni kuhakikisha watumiaji wa soda ya Coca-Cola wanafurahia ladha yake halisi na asilia wanapokunywa soda yenye sukari au ‘Coca-Cola Bila Sukari’.
Soda za ‘Coca Cola Bila Sukari’ zimeanza kuwa kwenye soko la Tanzania kuanzia mwezi uliopita katika sehemu zote zinapouzwa soda na bei yake ni sawa na soda aina nyingine zote zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Coca-Cola.

Standard Chartered Bank’s Group Chief Information Officer to visit Tanzania.

Standard Chartered Bank’s Group Chief Information Officer, Dr. Michael Gorriz is expected to visit the Bank’s offices in Tanzania today.

According to a statement issued by Standard Chartered Bank Tanzania Limited, during his visit Dr. Gorriz will meet with various internal and external stakeholders of the Bank in Tanzania with a view of exploring ways in which the Bank can further enhance its business and support economic growth in the country.

Dr. Gorriz was appointed Group Chief Information Officer on 25 March 2015 and is responsible for the banking operations, systems development and technology infrastructure which underpin the Bank’s client services, and defines and implements the Bank’s digital and innovation agenda.

His visit to Tanzania comes as the Bank commemorates its centenary anniversary since it first opened its doors in Tanzania in 1917. The visit is a continuation of key Group visits that have been taking place to mark the Bank’s historical milestone in Tanzania as well as further reiterate the Group’s commitment to Tanzania.

Dr. Gorriz will be accompanied by Top Team Members of the Group’s Information Technology and Operations Segment. These include; Bhupendra Warathe, the Global Head of the Bank’s Operations, Venkatesh Rathnam, the Global Head of Business Operations covering the Bank’s Retail Banking, Wealth Management and Private Banking Segments, and Toby Blythen, the Chief Financial Officer for the Information Technology and Operations Segment.

In March this year the Bank also hosted over thirty of its Top Management Team members from its Africa and Middle East Region. The delegation, the biggest ever to have visited the country at one go, was led by the Regional Chief Executive, Africa and Middle East, Sunil Kaushal. The members held business meetings with various Government Officials and members of the business community, as well as joined the staff in Tanzania to launch its centenary anniversary.

Africa, and the Bank’s business in Tanzania, continue to be a key market for the Standard Chartered Group. The Group’s highly ranked officials, therefore, continue to visit Tanzania with a view of further understanding the business on the ground thereby offering the necessary support to enhance its banking solutions leading towards further enhancing the country’s economy.

Standard Chartered Bank in Tanzania is known to have revolutionized Banking in Tanzania leveraging on its innovation in technology. The Bank introduced the country’s first Automated Teller Machine in 1997, the country’s first Visa Electron Debit card, and the country’s first Web Banking services for corporate clients.
Last year in July, the Bank became the first to launch a unique biometric enabled Mobile App. which has now attracted more than ten thousand downloads.

Dr. Gorriz, who is responsible for the Bank’s operations, systems development and technology infrastructure which underpin the Bank’s client services, has wide experience in the Technology field. Prior to joining Standard Chartered, Dr. Gorriz was the Vice President and Chief Information Officer at Daimler AG where he was globally responsible for strategy, planning and development of the Group’s IT systems, as well as the operation of its technical infrastructure.

During his 14 years at Daimler, Dr. Gorriz progressed through specialist research and design roles in aerospace to general management roles.
He is a physicist and engineer by background and obtained a PhD in Engineering.