HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

BREAKING NEWS: ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2017


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa.

Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.

Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.

Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.

Simbachawene alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.

Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.

"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.

Kuangalia majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa 


Tazama hapa Majina ya Wanafunzi Kidato cha Sita Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2017



TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.

TGGA YAZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA HEDHI SALAMA KWA WASICHANA

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi, Thomas Safari akizindua rasmi Kampeni ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani itakayofikia kilele Mei 28. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi leo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TGGA, Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA.
 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Lindi wakiingia kwa maandamano kwenye Uwanja wa Ilulu, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.


Na Richard Mwaikenda-Lindi
SERIKALI ya Mkoa wa Lindi imekubali ombi la Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), kwa kila shule kutenga chumba kimoja kwa ajili ya kujistiri wasichana wakati wa hedhi.

Ombi hilo lilitolewa na Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi, ambapo aliiomba serikali na walimu wakuu wa shule kutenga vyumba mashuleni vya wasichana kujihifadhi wakati hedhi.

Shaba ambaye ni mwalimu mstaafu, alisema kuwa wakati akitumikia ualimu katika shule mbalimbali alikuwa anatenga vyumba kwa ajili ya kazi hiyo na kwamba viliwasaidia sana wanafunzi wasichana.

Akihutubia wakati wa hafla hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya, Thomas Safari alisema vyumba vya siri kwa ajili ya wasichana wakati wa hedhi ni muhimu sana kwani vinawafanya wawe salama kiafya na wasafi wakati wote.

Alisema watahakikisha kwa kila shule katika mkoa huo inakuwa na chumba cha siri kwa wasichana, iliwe mfano hata kwa mikoa mingine na taifa kwa ujumla.

Pia aliwaasa wazazi, walezi na waalimu kueneza elimu hiyo ili watoto waelewe vizuri umuhimu wa usafi wakati wa hedhi, jambo ambalo litawafanya wawe na furaha, afya na usafi, hivyo kuondokana na mazoea ya kujinynyapaa na kulifanya la siri.

"Tuondokane na baadhi ya mila zetu potofu zinazolifanya suala la hedhi kuwa la siri, inatakiwa kuanzia sasa watoto wa kike wabebe begi lenye vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia wakati wa hedhi, ikiwemo khanga, pedi, vitambaa na mtandio. "alisema Safari.

"Inabidi sote tuwe mabalozi kwa kuongea na watoto, tutunze afya na usafi wao, kwani hao ndiyo viongozi wa taifa letu la kesho


. Bila kuwa na afya njema hatutakuwa na viongozi imara wa  Taifa letu."Alisisitiza Safari.

Dhima na lengo la TGGA ambayo ina wanachama zaidi 100,000 nchininni kuwajengea wasichana nafasi ya kujithamini, ari ya maendeleo, uzalendo kwa nchi na kujiamini.


 Wanafunzi wakiimba wimbo wa hamasa ya kampeni hiyo
 Mmoja wa wanafunzi akielezea jinsi ya kutumia pedi

 Maandamano ya wanafunzi kwenye Uwanja wa Ilulu
 Wanafunzi wa kike wakiwa na furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
 Rehema Kijazi wa TGGA Makao Makuu akiwahamasisha wanafunzi wakati wa maandamano
 Wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kuhamasisha matumizi salama ya vihifadhi yaani Pedi


 Viongozi wa TGGA Mkoa wa Lindi wakiwa eneo la uzinduzi wa kampeni hiyo
 Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Saharifa Mkwango akisherehesha 
hafla hiyo

 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa kuwaeleza  dhima na lengo la chama hicho kuwaelimisha wasichana kuhusu maadili mema na matumizi sahihi ya pedi wakati wa hedhi.
 Baadhi ya wazazi miongoni mwao wakiwemo walimu wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi

 Girl Guids kutoka Rwanda, Uganda na Madagascar wakihamasisha matumizi ya pedi wakati wa hedhi

 Mgeni rasmi, Thomas Safari akihutubia
 Safari akizindua rasmi kampeni hiyo kwa kufungua kasha lenye pedi
 Mgeni rasmi akikabidhi makasha yenye pedi yaani vihifadhi kwa wanafunzi wa shule mbalimbali



 Wanafunzi wakisakata muziki wakati wa kampeni hiyo

 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliokabidhiwa makasha ya pedi zitakazogawiwa shuleni kwao

 Girl Guids wakiwa katika picha ya pamoja

 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akisaidiana na mwanafunzi Caren Seki kumwagilia mti alioupanda katika shule ya Msingi Mtuleni
Mgeni rasmi, Thomas Safari akipanda mti wa kumbukumbu katika Shule ya Msingi Mtuleni
Girl Guids kutoka Rwanda, Madagascar na Uganda ambao wapo nchini kwa mpango wa kubadilishana uzoefu wakipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya msingi Mtuleni, Lindi

WANAFUNZI WA LUCKY VICENT WALIOPATA AJALI WAPATA VISA YA KWENDA MAREKANI KWA MATIBABU

Mbunge wa Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu amesema Ubalozi wa Marekani umetoa hati ya kusafiria (visa) kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi watatu wa Shule ya Lucky Vincent kupata matibabu nchini Marekani.
Katika ukurasa wake wa Facebook leo Nyalandu amesema waliopata Visa ni wazazi,watoto na wataalamu wawili wa afya ambao watasafiri kwenda Marekani.
"Wote wamepewa visa asubuhi ya leo Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam. Akina Mama watatu, watoto wote watatu, na Daktari Moja na Nurse Moja. Kansela wa Ubalozi wa Marekani alinipigia simu asubuhi akiwasubiri katika siku ambayo haikuwa ya kazi,” amesema Nyalandu na kuongeza:
“Mungu ambariki sana kwa moyo huu. Napenda pia kutoa taarifa kuwa ndege yao aina ya DC 8 inatarajiwa kutua Leo usiku saa 2:15 majira ya Afrika Mashariki katika uwanja wa KIA. Mungu wa Watanzania awabariki wote kwa sala na dua zenu kwa ajili ya hawa watoto. Sifa na utukufu kwa Mungu wetu.”
Katika taarifa ya awali kwa vyombo vya habari Nyalandu amesema safari ya kuelekea Marekani itakua kesho asubuhi na ndege itatua Charlotte,New York na kisha wagonjwa pamoja na waliowasindikiza wataingia katika ndege nyingine maalumu ya kubeba wagonjwa hadi katika mji wa Sioux City,Iowa
Watoto hao watatu walijeruhiwa wakati wakiwa katika safari ya masomo wilayani Karatu mkoa wa Arusha jumamosi iliyopita na kusababisha vifo vya wanafunzi 32,walimu wawili na dereva wao.

SKULI YA KIJINI NA MBUYU TENDEE MATEMWE WAFAIDIKA NA MRADI WA UJENZI WA KIJIJI CHA UTALII CHA PENNYROYAL KWA KUTOA ELIMU YA AFYA NA MAZINGIRA

Maafisa Afya na Mazingira kutoka (SUZA) Nahya Khamis Nassor Mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Chuo cha SUZA ametoa mafunzo ya Afya na mazingira kwa Wanafunzi wa Skuli ya Kijini Matemwe akizungumza na waandishi wa habari kufanikiwa kwa zoezi hilo la kutowa elimu kwa wanafunzi wa Skuli hiyo jinsi ya kuhifadhi mazingira na afya yao. Mradi huo unaosimamiwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Kitalii Matemwe Pennyroyal kwa kutowa elimu hiyo.
Amesema umeleta mafanikio makubwa kwa watoto hao jinsi ya kujilinda na maradhi ya mripuko kwa kupata elimu hiyo.
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa SUZA Nahya Khamis Nossor akitoa mafunzo ya Afya ya Mazingira kwa Wanafunzo wa Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe jinsi ya kujikinga na maradhi ya mripuko kwa kutunza mazingira safi katika maeneo yao na skuli, Mradi huo wa Elimu hiyo unafadhiliwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Matemwe  Pennyroyal.  
Wanafunzo wa Skuli ya Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakifuatila mafunzo hayo wakiwa katika darasa wakifuatilia kwa utulivu  wakiangalia vipeperushi vinavyoelezea utungaji wa Afya na Mazingira katika jamii.

Afisa Afya na Mazingira Bi Zeldat Masoud Khamis akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe jinsi ya elimu ya afya ya mazingira kwa wanafunzi hao. 
Mafunzo ya vitendo jinsi ya kusafisha mikono kujinginga na maradhi na kuweka mazingira mazuri ya afya yake kwa kutumia maji na sabuni kufanya usafi kabla ya kula na baada ya kutoka msalani.

Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe wakisoma kipeperushi kinachoelezea Afya ya Mazingira wakati wa mafunzo hayo. 
Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisoma vipeperushi vinavyoeleza utunzaji wa Afya na Mazingira ili kujikinga na maradhi ya matumbo na kipindupindu, Mafunzo hayo yanatolewa na Mradi wa Kampuni ya Pennyroyal inayojenga Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar.


Imetayarishwa na Othman Mapara wa Zanzinews.com

MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AMALIZA ZIARA JIMBONI,WANANCHI WALIA NJAA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemaliza kufanya ziara yake ya siku tatu katika jimbo la Shinyanga.


Katika ziara hiyo ya kikazi iliyoanza Februari 15,2017 kumalizika Februari 17,2017 ,Mheshimiwa Masele amekagua miradi ya maendeleo na kufanya vikao na wananchi wa kata 14 kisha kujadili na kuzitafutia ufumbuzi kero za wananchi.

Katika maeneo mengi aliyopita,Mheshimiwa Masele amekutana na kilio kikubwa cha tatizo la njaa linalowakabili wananchi ambao walidai wamekuwa wakiendesha maisha yao kwa kunywa uji hivyo kuiomba serikali iwaone kwa jicho la huruma na kuwapatia chakula.
Mheshimiwa Masele pia amekumbana na kilio cha bei kubwa ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA),huku wananchi katika maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria wakiomba huduma hiyo ili kuondokana na kero ya maji.
Viongozi wa shule za msingi nao walipaza sauti zao juu ya uhaba wa walimu katika shule,matundu machache ya vyoo ukilinganisha na idadi kubwa ya wanafunzi,upungufu wa madarasa huku wengine wakiomba kupatiwa huduma ya maji na umeme katika shule zao.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Mheshimiwa Masele alisema yeye kama mbunge hayupo tayari kunyamaza juu ya matatizo yanayowakabili wananchi wake na kuahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka zinazohusika ili kumaliza changamoto hizo.
“Naomba serikali yetu itambue kuwa wananchi wa jimbo la Shinyanga Mjini wana njaa,wanahitaji chakula,hatuhitaji chakula cha bure bali tunataka chakula cha bei nafuu,wananchi wanalala njaa,shule zetu hazina walimu wa kutosha,bado bei ya maji iko juu sana ukilinganisha na kipato cha wananchi”,alieleza Masele.
Siku ya kwanza ya ziara,mheshimiwa Masele alitembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja la Galamba na kuangalia,siku ya pili na tatu katika ziara yake ametembelea shule za msingi na kufanya vikao mbalimbali.
Katikati ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akienda kuangalia eneo ambapo patajengwa choo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.Kulia ni diwani wa kata ya Mwamalili Paul Machela (CCM),wa kwanza kushoto 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiangalia eneo ambapo patajengwa choo kwa ajili ya shule ya msingi Twendepamoja yenye jumla ya wanafunzi 820 wanaotumia matundu 6 ya choo na walimu 8 pekee.Wa kwanza kushoto ni mwalimu Cephrine Philip anayefundisha katika shule hiyo.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Twende Pamoja ambapo alisema kupitia mfuko wa jimbo ametoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo.
Kulia ni Mwalimu mkuu Msaidizi katika shule hiyo Regina Bundala akimwonesha mheshimiwa Masele eneo ambapo watajenga choo kipya kwa ajili ya shule hiyo yenye wanafunzi 662 wakitumia matundu manne ya choo huku walimu nane waliopo katika choo hicho wakiwa hawana choo.
Katikati ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza akiwa katika ofisi ya walimu shule ya msingi Ujamaa ambapo alisema mfuko wa jimbo umetoa shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa choo cha wanafunzi na walimu wa shule hiyo.Kulia ni Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Shinyanga Gideon Kyungai,kushoto ni diwani wa kata ya Mwamalili Paul Machela.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Ujamaa na kuwataka wasome kwa bidii kwani elimu ina faida na itawasaidia kujikomboa katika maisha yao.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa amebeba mtoto katika ofisi ya mtendaji wa kijiji cha Seseko inayotumika kama Zahanati ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya kliniki kwa watoto
Hapa ni katika shule ya Msingi Old Shinyanga iliyopo katika kata ya Old Shinyanga, Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akikagua choo kipya (kushoto) cha wanafunzi kinachojengwa chenye matundu 8 baada ya choo cha zamani kujaa na kuhatarisha maisha ya wanafunzi.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya choo kipya akiangalia ujenzi unavyoendelea.Kushoto kwake ni diwani wa tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa Picca Chogelo (CCM).
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza nje ya choo hicho ambapo alisema mfuko wa jimbo umetoa shilingi milioni 2.3 kusaidia katika shughuli za maendeleo ya kata ya Old Shinyanga.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa katika jengo la kituo cha Maendeleo ya awali ya watoto kilichojengwa na shirika la Save the Children kilichopo katika shule ya msingi Old Shinyanga katika kata ya Old Shinyanga
Diwani wa tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa Picca Chogelo (CCM) akielezea changamoto zilizopo katika kata ya Old Shinyanga wakati wa kikao cha mbunge Masele na wananchi wa eneo hilo ambapo alisema ni pamoja na uhaba wa matundu ya vyoo, katika shule,zahanati ya Old Shinyanga kukosa chumba kwa ajili ya akina mama wajawazito na eneo la zahanati kukosa uzio kutenganisha na mnada uliopo katika zahanati hiyo
Mbunge wa Shinyanga Mjini Mheshimwa Stephen Masele akizungumza wakati wa kikao na wananchi wa kata ya Old Shinyanga kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto za wananchi.Masele alilipongeza shirika la Save the Children kujenga jengo kwa ajili ya maendeleo ya awali ya watoto katika kata hiyo na kwamba serikali itaendelea kusaidia katika miradi mbalimbali katika kata hiyo.Kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi 
Mkazi wa Old Shinyanga akimwelezea Mbunge Masele jinsi wakazi wa eneo hilo wanavyoshinda na njaa kutokana na uhaba wa chakula inayochangiwa na chakula kuuzwa kwa bei kubwa
Mheshimiwa Masele akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya msingi Old Shinyanga
Mheshimiwa Masele akizungumza na baadhi ya vijana wa Old Shinyanga walioamua kuzuia gari lake asiendelee na safari ili asalimiane nao
Aliyesimama ni ni Diwani wa tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa Picca Chogelo (CCM) akizungumza katika kikao cha mbunge na wananchi wa kata ya Chibe ambapo alisema kata hiyo haina shule ya sekondari watoto wanalazimika kusafiri umbali mrefu kwenda Old Shinyanga,eneo hilo halina huduma ya maji huku akiomba kata hiyo ijengewe barabara kwa kiwango cha lami kwani mji huo unakua kwa kasi
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wakazi wa Chibe ambapo alisema anachofanya hivi sasa ni kuhakikisha shule zote za msingi katika jimbo lake zinamaliza changamoto ya uhaba wa matundu cha choo
Wananchi wa Chibe wakimsikiliza mbunge wao 
Wananchi wakiwa katika kikao
Katikati ni diwani wa kata ya Lubaga mheshimiwa Obeid Jilala (CHADEMA)akimpokea mheshimiwa Stephen Masele
Mheshimiwa Masele(CCM) akiwa na Obeid Jilala (CHADEMA) katika kikao cha kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa kero za wananchi
Diwani wa kata Lubaga mheshimiwa Jilala akimkaribisha mheshimiwa Masele (kushoto) ili azungumze na wananchi wa kata ya Lubaga.Kulia ni katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Rajabu Makuburi
Mheshimiwa Masele akizungumza katika kikao cha majadiliano kuhusu maendeleo ya kata ambapo alisema ametoa shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo ya kata hiyo
Mheshimiwa Masele akijibu hoja ya ongezeko la bei kubwa ya maji na kero ya maji machafu yanayotoka kwenye mabomba ya maji ambayo yanasambazwa na SHUWASA
Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Shinyanga Gideon Kyungai akielezea kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na changamoto ya uhaba wa walimu na matundu ya vyoo katika shule mbalimbali za manispaa ya Shinyanga
Aliyesimama ni diwani wa kata hiyo Morice Mugini (CCM) akimkaribisha mheshimiwa Masele katika shule ya msingi Ushirika iliyopo katika manispaa ya Shinyanga
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ushirika Lucia Amede akielezea changamoto ya matundu ya choo katika shule hiyo ambayo ina wanafunzi 844,matundu 6 pekee ya choo hali inayosababisha wanafunzi wapange foleni wakati wa kujisaidia
Mheshimiwa Masele alizungumza katika kikao na wakazi wa kata ya Chamaguha ambapo alisema amesema pia kuna pesa kutoka mfuko wa jimbo imetolewa kusaidia ujenzi wa choo kipya cha shule hiyo 
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akielezea jinsi ilani ya uchaguzi ya CCM inavyoendelea kutekelezwa katika kata mbalimbali za jimbo la Shinyanga
Mheshimiwa Masele akiangalia choo kipya inachojengwa katika shule ya msingi Ushirika
 Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Shinyanga Gideon Kyungai akizungumza katika shule ya msingi Kizumbi
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizumbi Neema Mkanga akitoa taarifa fupi kuhusu shule ya msingi Kizumbi kwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele.Alisema shule hiyo ina wanafunzi 502,matundu ya choo 6 ya wanafunzi,walimu 10 wanaotumia ambao hawana choo bali wanatumia tundu moja la choo cha wanafunzi
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akizungumza katika shule ya msingi Kizumbi 
Mheshimiwa Masele akizungumza na wananchi wa Kizumbi
Mheshimiwa Masele akisisitiza kuhusu huduma ya maji katika eneo hilo ambapo alisema huduma hiyo inatakiwa iwafikie kutokana na bomba la maji kupita eneo la kata hiyo
Mheshimiwa Masele akizungumza na wananchi wa Kizumbi
Mzee Paul Kashinje mkazi wa kijiji cha Bugayambele kata ya Kizumbi akiomba serikali iwapatie chakula kwani wanashinda na njaa kunywa uji 
Mheshimiwa akiwa katika eneo la choo cha shule ambacho kinatumiwa na walimu na wanafunzi,eneo hilo ndipo pia patajengwa choo kipya
Mheshimiwa Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Kizumbi
Mheshimiwa Masele akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Kizumbi
Wanafunzi wakimpokea mheshimiwa Masele
Mheshimiwa Masele akiangalia matofali yanayotumika katika ujenzi wa choo cha shule ya msingi Ibinzamata
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ibinzamata Vaileth Lumelezi akisoma risala kwa mheshimwa Masele ambapo alisema shule hiyo haina huduma ya umeme japo nguzo za umeme zinapita hapo.Alisema shule ina jumla ya wanafunzi 965 na matundu manne pekee ya choo
Mheshimiwa Masele akizungumza katika shule ya msingi Ibinzamata.Kulia kwake ni diwani wa kata ya Ibinzamata Reuben Kitinya
Wazazi wakimsikiliza mheshimiwa Masele
Mheshimiwa Masele akizungumza na wazazi wa wanafunzi
Hapa ni katika shule ya msingi Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga,Pichani ni diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Ngunila (CHADEMA) akimkaribisha mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele ili azungumze na wakazi wa wanafunzi katika shule hiyo
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kitangiri Chrizestom Kitale akisoma risala kwa mheshimiwa Masele ambapo alisema shule hiyo ina wanafunzi 1265,na kwamba inakabiliwa na uhaba wa madarasa na matundu ya vyoo
Mheshimiwa Masele akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ametoa shilingi milioni moja kusaidia maendeleo ya kata hiyo ikiwemo ujenzi wa matundu ya choo
Mheshimiwa Masele akizungumza na wazazi
Diwani wa Viti Maalum Mariam Nyangaka(CCM) akisisitiza jambo katika kikao hicho
Wazazi wakiwa kwenye kikao