HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Steve Nyerere – Kuna wasanii wanajifanya ‘Mungu watu’

Msanii wa filamu, Steve Nyerere, amedai wasanii wa filamu wanashindwa kufanikiwa kutokana na kukosa ushirikiano huku akidai kuna baadhi yao wanajifanya wao ni mungu watu.

Muigizaji huyo amedai hakuna mtu wa nje ambaye ataweza kuja kuikomboa tasnia yao ya filamu isipokuwa wao wenyewe.
“Leo hatupo katika umoja, kwanza ili tuweze kufanikiwa mafanikio hayapo ya mmoja mmoja, mafanikio yote duniani yalipita kwa watu ndiyo wewe ukafanikiwa kwa hiyo lazima tukubaliane, tupendane na nyoyo zetu ziwe zimefunguka kwa kufanya vitu vizuri,” Steve alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aliongeza, “Kuna ma-director wazuri zaidi lakini leo wote hawapo, wanachokikosa ni ushirikiano, tunao ma-director wazuri tu, wanaweza wakafanya kitu kizuri tu ‘site’ lakini ushirikiano hawana, kuna watu wanakuwa Mungu watu haiwezekani, haiwezekani kuwa Mungu mtu jamani Mungu ni mmoja tu,”
Muigizaji huyo amekuwa akipingana na wasanii wenzake wa filamu walioandamana mwezi mmoja uliopita wakiishinikiza serikali kuzifungia filamu za nje ambazo hazilipi kodi kwa madai zinawaharibia soko lao la filamu za ndani.

SAKATA LA ROMA : WASANII WAINGIWA NA HOFU KUU, WAFUNGUKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Ni siku ya pili sasa, Roma, Moni Centrozone, producer wa Tongwe Records, Bin Laden na vijana wengine waliotekwa na watu wasiojulikana walipokuwa katika studio hizo, bado haijafamika walipo.

Jitihada za awali zilizofanywa na watu wao wa karibu, akiwemo mke wa Roma,Nancy zimegonga mwamba. Katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari, Nancy amesema amezunguka katika vituo vingi vikubwa vya polisi kuulizia taarifa za mumewe jibu analokutana nalo ni ‘hatuna taarifa zozote, tutashughulikia.’ Majibu hayo hayana matumaini kwa Nancy ambaye ni siku ya pili sasa hajamuona wala kusikia sauti yake mume wake aliyemuuaga usiku wa juzi kuwa anaenda Tongwe Records, studio ambayo hurekodi nyimbo zake.
“Serikali, waandishi wa habari, Watanzania, yeyote aliyeona, aliyesikia, anayeweza kutusaidia Roma yuko wapi naombeni msaada wenu,” anasema Nancy ambaye yeye na Roma wamebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Ivan.
“Nahitaji kufahamu yuko wapi, yuko katika hali gani,” anaongea kwa uchungu.
Roma na wenzake wako wapi? Ni swali ambalo kila mtu anajiuliza kwa sasa? Wasanii wengi wameingiwa na hofu kubwa. Haya ni baadhi ya maoni yao:

Vanessa Mdee
Wherever you are, God is Bigger than, Stronger than, Realer than all the other forces that be. Stay UP brother @roma2030 #VivaRoma #FreeRoma #FreeMoni roho inauma na nimetoka kumsikiliza mkeo redioni hajui hata ulipo sasa ndiyo nini 😡😡😡😡😠is this where we are at now? Ma studio yanavamiwa, watu wanakamatwa kama wanyama pori. Aaaarrrrgh

Diamond
Wakati mwingine natafakari sijui hata wapi tunaelekea… lla kwakuwa Mwenyezi Mungu ndio Mpangaji wa yote basi naamini hata hili litapita tu… Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya @roma2030 na wanamziki wenzetu wote ambao hadi sasa haijajulikana walipo..

Nay wa Mitego
Siku nzima ya leo nimekosa raha kabisa, cjui Mshkaji wangu Yupo kwenye hali gani, mazingira gani.? Roma yuko wapi.?! Sim yake ukipiga inaita Kama kawaidi, Masege Whatsup zinasomwa, Sim hazipokelewi. Vyombo husika tunaomba mtusaidie, tunaitaji kujua ndugu zetu wako wapi.? Hatuwezi kukaa kimya.
Hivi kweli tumefikia huku.? Tunaenda wapi.? #FreeRoma✊🏿
#Wapo


Professor Jay
Wakati sisi tunakosa Usingizi na kuendelea kupaza Sauti, Kuna wengine wameweka miguu juu wanaona hili haliwahusu na wengine wanakwenda mbali zaidi na kudiriki kusema hii ni KICK ya Muziki tu..
Narudia tena kuwaambia ndugu zangu WAKIMALIZANA NA SISI WATAKUJA KUMALIZANA NA NYINYI😭😭😭
#Bring Back our SOLDIERS Alive.

Ray C

Nimeanza kuingiwa na woga,nafikiria mambo mengi Roma alipo Sasa,anafanywa nini na tatizo ni nini mpaka imekuwa hivi na masaa yanaenda hakuna jibu lililo kamili!!hisia mchanganyiko na zote sio nzuri….Nini kinaendelea?Tatizo ni nini??Sababu ni nini?Bado najiuliza sipati jibu………

Fid Q
Nimeipokea hii HABARI kwa mstuko mkubwa.. sio tu kwasababu TONGWE ni moja kati ya wadhamini wetu wa #OpenMicThursday pia ni moja kati ya studio ambazo zimekua msaada mkubwa sana ktk kunyanyua vipaji na C E O @j_murder_tongwe amekua mstari mbele sana ktk kufanikisha hilo.. kinachonistua na kuninyima raha zaidi ni hili la hawa ndugu zetu akina @roma2030 @moni_centrozone Producer Belo na mlinzi kuwa hawajulikani waliko hadi hivi sasa.. ninaiomba MAMLAKA HUSIKA ya USALAMA itusaidie ili waweze kupatikana mapema na kuifutilia mbali ile hofu iliyotanda mioyoni mwa ndugu, jamaa na marafiki… mwisho namuomba MUWEZA WA VYOTE azifanyie wepesi familia za ndugu zetu waliopotelea kusikojulikana in sha Allah

AY
Vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka tujue hali za wasanii wenzetu wako kwenye hali gani..@romamkatoliki Mungu yupo pamoja nanyi awaepushie lolote baya.. @tongwerecords @j_murder_tongwe

Waziri Nape: Sikupinga vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya bali nilishauri busara itumike

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa ufafanuzi juu ya kauli iliyonukuliwa ikionyesha kuwa alipinga vita dhidi ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amedai kuwa hakupinga vita hiyo bali alitaka busara itumike kwa washukiwa.

Waziri Nape alitoa ufafanuzi huo katika kipindi cha dakika 45 cha ITV, alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho kutaka kujua kuhusu kauli yake iliyoonesha kupinga utaratibu uliotumika wa kuwakamata au kuwapata watuhumiwa wa dawa za kulevya.

“Niseme kwanza ilitokea nilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, ukienda leo ukanitaja Nape ukaniambia baada ya siku mbili njoo kituoni, hata kama nilikuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwangu hivi unayakutaje? 

'Kwasababu kwa vyovyote vile nitayachukua, ntayaficha, ntakuja kituoni ntaripoti utanibana ntakwambia twende nyumbani kwangu ukakague mnaenda mnakagua mnakuta hamna, si basi! 

"Kwahiyo nikawa na wasiwasi kwamba inawezekana kabisa nia ilikuwa njema lakini nilidhani pangeweza kutengenezwa utaratibu bora zaidi ya namna ya kuwapata, kwasababu hapa kuna watumiaji, kuna wauzaji na wale ambao wanaleta sasa madawa ya kulevya,” alisema Nape.

Aliendelea, “Ukishughulika na mtumiaji huyu ukadhani ndiye mhalifu wako unakosea, kwasababu huyu ni muathirika na muathirika anahitaji dawa anahitaji huduma ameshaathirika, hapa wahalifu wetu nikuanzia huyu anayemletea halafu kuna huyu anayempa yule aliyemletea, sasa ili uwapate hawa wawili lazima umtumie huyu vizuri ili akupeleke kwa hawa wawili. Lakini ukimkamata huyu ukamtia ndani sasa hawa wawili watakimbia.”

“Kwahiyo mimi nikaona kwamba tunaivuruga vita yenyewe, anayeingiza madawa ya kulevya na anayesambaza kwa maana ya kuyauza, hawa ndiyo tatizo letu. Na ndio maana nikasema hebu tutumieni busara, watu wakadhani nimepinga. 

"Tena mimi nilisema mara nyingi sana tumieni busara namna ya kuiendesha vita hii. Madhara ya kutotumia busara katika vita hii ni makubwa sana, kwasababu ukimweka huyu mtu mmoja ndani hawa wengine wataendelea kuwaathiri wengine na ndiyo maana nasema hii vita tutumieni busara. 

"Hii vita ni ya kupigana kimya kimya kwasababu wanaofanya biashara hii hawaifanyi hadharani wanafanya kwa kificho. Shughulika nao kwa kificho, hii vita hakuna mahali ambapo wameshawahi pigana hadharani, tukitajana hadharani hata wenye chuki watatajana humo humo,” alisisitiza.

STEVE NYERERE : WEMA SEPETU HADAI CHOCHOTE CCM, AOMBA MSAMAHA BAADA YA KURECODIWA

Baada ya sauti zilizosambaa zikimuhusisha Mwigizaji Steve Nyerere na Mama wa mwigizaji Wema Sepetu wakizungumza huku akitaja baadhi ya viongozi mbalimbali aliodili nao kwenye sakata la Wema kushikwa na Polisi, leo Steve Nyerere ameita Waandishi wa habari na kuongea nao.

Steve Nyerere amesema kuwa hakuna msanii hata mmoja ambaye anakidai Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema mambo ambayo anasema Weme Sepetu kuwa anakidai chama hicho ni uongo na uzushi mtupu.

Amesema katika wasanii mbalimbali ambao huenda walilipwa pesa nyingi zaidi ni Wema Sepetu pamoja na yeye na kusema wao pamoja na wasanii waliokuwa wanaendesha kampeni ya 'Mama ongea na mwanao' ni wasanii ambao walilipwa vizuri sana na Chama Cha Mapinduzi kuliko wasanii wengine wowote wale.

Steve Nyerere anasema katika mkataba walioingia na Chama Cha Mapinduzi hakuna sehemu mkataba huo unasema ukikamatwa na madawa ya kulevya, bangi  chama hicho kitakuja kukusaidia. 

Pia Steve Nyerere anakiri wazi kuwa sauti ambayo inazunguka kwenye mitandao ya kijamii ni kweli ni sauti yake na alikuwa akiongea vile ili kumridhisha mama yake na Wema Sepetu kwani wakati huo jambo hilo lilikuwa ngumu kwake. 
Aliyoyasema haya hapa
'Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu yasipindishwe"-Steve Nyerere

"Kwenye kampeni tulilipwa hakuna aliyefanya kazi bila kulipwa, kundi la mama ongea na mwanao mimi ndio nilikuwa mwenyekiti"Steve Nyerere

"Uwezo wa kuwaambia Wabunge au kuwaelekeza cha kufanya sina, sina ujanja huo.... namuomba radhi Spika Job Ndugai" -Steve Nyerere

"Ninaimani aliyelipwa fedha nyingi kwenye mama ongea na mwanao ni dada 'Wema' hakuna msanii hata mmoja anayeidai CCM"-Steve Nyerere

"Ile audio imekuja kuachiwa juzi wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo makusudi" - Steve Nyerere

"Namuomba radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza"-Steve Nyerere

"Nimetaja viongozi ktk ile audio alafu unakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa Nchi, Mama alichofanya kuisambaza ni mauaji" - Steve Nyerere

"Watanzania wenzangu usimuamini binadamu yeyote, Mama Wema alitaka kuniharibia maisha yangu, Mama kanikosea.. namuachia Mungu"-STEVE NYERERE

"Nina miaka 25 kwenye sanaa, leo mtu anatoa vitu ambavyo tulikuwa tunaongea kwa ajili ya mwanae, alitaka kuniharibia maisha yangu"-Steve

Wema Sepetu kuhamia CHADEMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kunatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwamo msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu(28).
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.
Msanii huyo ambaye alishinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.

KESI YA WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA HADI MACHI 15

Wema Sepetu akiwa na Martin Kadinda

Malkia wa filamu Wema Sepetu Jumatano hii alirudi Mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana kwenye sakata la dawa za kulevya.
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya upande wa mashtaka kusema upelelezi haujakamilika hivyo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa 15 March 2017.
Muigizaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao walitajwa kwenye list ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda yawatuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Katika upelelezi wa awali ambao ulifanywa na jeshi la polisi, walidai wamekuta msokoto wa bangi nyumbani kwa muigizaji huyo

Ray C: Nampenda sana Rayvanny

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Ray C amedai kuwa anamkubali zaidi Rayvanny kutoka lebo ya WCB.

Ray C amesema kuwa amesikia msanii huyo amewaandikia wasanii wengi nyimbo hivyo na yeye anatamani siku moja aje kufanya naye kazi.
“Nampenda sana yule mtoto Rayvanny. Anaandika sana mashairi, nasikia anaandikia wasanii wengi nyimbo hata mimi natamani kufanya naye kazi,” Ray C amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Mbali na hilo msanii huyo ameongeza kuwa anamheshimu sana Diamond Platnumz kutokana na kule alipofika kwakuwa muziki wake umefika sehemu ambayo wao hapo mwanzo hawakuwahi kufika.

PICHA: WAZIRI NAPE AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA KARIAKOO, AKAMATA KAZI FEKI ZA WASANII

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye leo ameongoza timu yake katika operesheni maalumu ya kufanya msako mkali wa wauzaji wa kazi za wasanii bila vibali vya Bodi ya filamu ya Tanzania.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia bidhaa za filamu na muziki zilizofeki leo hii.
Waziri huyo amevamia maduka yanayouza CD FEKI pamoja na ofisi ambayo inajihusisha na kurudufu kazi za wasanii kutoka ndani na nje ya nchini.
Hii ni ziara ya Pili kuifanya Kariakoo. Ziara ya kwanza ya kushitukiza aliifanya July 15, 2016 ambapo aliwataka wauzaji wa CD kote nchini kufuata sheria ya kuuza CD zenye stika huku akisema mtu yoyote ambaye atakutwa na CD ambayo haina stika mnunuaji na muuzaji wote watakamatwa. Operesheni hizi zinafanywa kwa lengo la kutokomeza uharamia wa bidhaa za filamu na muziki kwa kuokoa pato la TAIFA

Amesema Seikali itawachukulia hatua za kisheria ikiweemo kuwafutia leseni wauzaji na wasambazaji wa filamu nchini ambao wamekuwa wakiuza bidhaa hizo bila vibali kutoka kutoka mamlaka husika jambo ambalo likiikosesha serikali mapato pamoja na kuchangia momonyoko wa maadili katika jamii.