HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

Benki ya CRDB kushirikiana na Water.Org kuborosha miradi ya maji na usafi


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Water.Org, Eng. Francis Musinguzi kwa pamoja wakionesha mikataba ya ushirikiano mara baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam tarehe 18 Julai 2024. Wangeni pichani ni wanasheria wa Benki ya CRDB na Shirika la Water.Org.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Water.Org, Eng. Francis Musinguzi wakibadilishana mikataba ya ushirikiano ushirikiano katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam tarehe 18 Julai 2024.

=========  ========

Dar es Salaam. Tarehe 18 Julai 2024: Benki ya CRDB imesaini mkataba wa makubaliano na shirika la Water.Org Afrika unaolenga kuboresha upatikanaji wa maji safi na mazingira safi katika maeneo mbalimbali nchini. Ushirikiano huu unaonyesha dhamira ya Benki ya CRDB katika kuchangia maendeleo endelevu na ustawi wa jamii.

Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki hiyo, Bruce Mwile alisema kuwa makubaliano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Benki ya CRDB ambayo inaelekeza katika kutoa suluhisho bunifu kwa jamii ili kukuza ustawi wa wadau wake. 

"Tunajivunia kuona tunaendelea kuishi azma yetu ya kuchochea ustawi wa jamii kupitia ubia wa kimkakati na wenzetu wa Water.Org. Nizishukuru timu zetu za kitaalamu ambazo zimefanya kazi kubwa hadi kufikia hatua hii ambayo inatoa fursa kwa jamii kunufaika na uwezeshaji katika sekta ya maji na usafi," alisema Mkurugenzi huyo.

Mwile amesema ushirikiano huo utawezesha miradi ya sekta ya maji pamoja na usafi wa mazingira kwa kutumia fedha zitakazotengwa katika maeneo mbalimbali. Miongoni ya maeneo hayo ni pamoja na utafiti na ufadhili wa miradi ya maji na usafi wa mazingira, mikopo ya miundombinu ya maji na usafi.

Benki hiyo intarajia pia kutoa mikopo midogo kwa watu binafsi, wajasiriamali, biashara, na taasisi kwa ajili ya kufunga miundombinu ya maji ya nyumbani, vifaa vya matumizi ya maji kwa ufanisi, na ujenzi wa vyoo na matangi ya maji safi na maji taka.

Aidha alisema mikopo hiyo pia itaelekezwa kwa sekta ya kilimo hususani kwa wakulima wanaotumia mifumo ya umwagiliaji yenye matumizi ya maji kwa ufanisi. “Ushirikiano huu pia utawezesha uanzishwaji wa huduma za bima zitakazotoa ulinzi dhidi ya majanga yanayoathiri miundombinu ya maji.” aliongezea Mwile.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Water.Org, Injinia Francis Musinguzi amesema kuwa ushirikiano huu unalenga kwenye kuboresha maisha ya jamii inayotuzunguka pamoja na hayo aliongezea kuwa utawezesha ufadhili wa tafiti za hatifungani za maji na usafi wa mazingira, pamoja na kuanzishwa kwa miradi endelevu ya maji na usafi. 

“Ushirikiano huu pia utawezesha ufadhili wa tafiti za ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi katika kufadhili miradi mikubwa ya usambazaji maji na usafi, pamoja na ufadhili wa bunifu za usimamizi wa maji kwa teknolojia,” alisema Injinia Musingizi.

Katika eneo la elimu na uhamasishaji, Benki ya CRDB na Water.Org watashirikiana kufadhili kampeni za elimu na uhamasishaji kuhusu umuhimu wa usafi ili kuzuia magonjwa, kupitia taasisi ya CRDB Bank Foundation ambayo imejikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii na kutoa mitaji wezeshi kwa wajasiriamali wanawake na vijana.

Makaubaliano ambayo Benki ya CRDB imeingia na Water.Org ni mwendelezo dhamira yake ya kuchangia ufikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), hususan Lengo namba 6, 'Maji Safi na Usafi wa Mazingira'.

WANAHISA WA MAENDELEO BANK KUKUTANA JUNI 23 MWAKA HUU

MAENDELEO BANK - PLC, inatarajia kufanya Mkutano mkuu wa 4 wa mwaka Mkutano huo utakaowakutanisha Wanahisa wote utafanyika Juni 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.Hayo yametanabaishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Bwa. Ibrahim Mwangalaba alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maendeleo Bank, uliopo makao makuu ya Banki, katika jengo la Luther House, siku ya jana jumatano .

Pamoja na taarifa hiyo Mwangalaba alifafanua dhamiria ya Banki katika kijitanua zaidi kwa kudumisha utendaji bora wa utoaji huduma hadi kufikia hadhi ya kitaifa jambo lililopelekea kutoa toleo jipya la hisa lililoanza tangu mwishoni mwa mwaka 2017.
Ifikapo tarehe 09 Septemba mwaka huu, Maendeleo Bank itakua inatimiza miaka 5 tangu kuanzishwa kwake.


Maendeleo Bank inaendelea Kutoka huduma kwenye matawi yake matatu ya yaliyopo Luther, Kariakoo na Mwenge. Pia inatoa huduma kupitia MB Mobile na zaidi ya ATM 270 za umoja nchi nzima.

Mufti ahimiza uadilifu futari ya Standard Chartered

 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally (kulia) akiongozana na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) pamoja na Mshereheshaji wa futari hiyo, Abdulssamad Ayoub (katikati) mara baada ya kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mheshimiwa Prof. Dk. Ratlan Pardede (katikati) akiongozana na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kulia) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kawaida benki ya Standard Chartered nchini, Ajmar Riaz (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akisalimiana na mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally mara baada kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) na Mshereheshaji wa futari hiyo, Abdulssamad Ayoub (kushoto)
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akisalimiana na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mheshimiwa Prof. Dk. Ratlan (katikati) mara baada ya kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kawaida benki ya Standard Chartered nchini, Ajmar Riaz.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kawaida benki ya Standard Chartered nchini, Ajmar Riaz (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally akitoa mawaidha kwa wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwakwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akizungumza na wateja pamoja na wageni waalikwa wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Indonesia nchini, Prof Dk Ratlan Pardede akizungumza na wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini, Mh. Hussein Hamadi akitoa salamu za mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally (kulia) wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi Rughani (kulia) akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wanaowasili ukumbini hapo kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.




 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (wa nne kulia) wakiongoza baadhi ya wateja na wageni waalikwa kupakua futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani, Balozi wa Indonesia nchini, Prof Dk Ratlan Pardede pamoja na Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini Hussein Hamadi wakiwa meza kuu wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally katika picha ya pamoja na meza kuu na baadhi ya viongozi wa Bakwata mara baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Pichani juu na chini ni baadhi ya wateja na wadau wa benki ya Standard Chartered waliohudhuria futari iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (katikati) akimkabidhi zawadi Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini, Mh. Hussein Hamadi (kushoto) ikiwa ni shukran kwa kushiriki futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo mara baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Na mwandishi wetu
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally amesema Waislamu na walimwengu kwa ujumla wananafasi kubwa ya kujifunza mawaidha yanayotolewa katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwamo kumcha Mungu na uadilifu.

Mufti alisema hayo kwenye futari iliyoandaliwa na benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena.

Alisema katika hafla hiyo ambayo pia walikuwemo wageni wastahiki Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mheshimiwa Prof. Dk. Ratlan Pardede na Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini Tanzania, Hussein Hamadi, kuwa mwezi wa Ramadhani ni chuo ambacho kinafunza mambo mbalimbali.

Alisema mafunzo hayo yanatarajiwa kutumika muda wote katika miezi 11 iliyobaki katika mwaka.

Alisema mambo ambayo yanazungumzwa katika Chuo hicho ni mengi lakini makubwa ni mahusiano katika masuala ya kiroho, kijamii, kiuchumi na kimaadili.

Alisema mafunzo yanayopatikana katika mwezi huo mmoja wa kumcha Mungu wenye siku takribani 29 hadi 30 yanatengeneza uaminifu si kwa Mungu pekee bali na kwa viumbe wake.

Aidha alisema amefurahishwa na Benki hiyo kutambua umuhimu wa mwezi huu kwa kutenga muda na mali ili kuwakutanisha wanajamii ili waweze kumcha Mungu na kujuana.

Alisema anaamini watu wa Standard Chartered ni waaminifu, waadilifu katika kutoa huduma na hilo ndilo Mungu analihitaji ugawaji wa haki kwa jamii katika usawa.

Katika futari hiyo Balozi wa Indonesia Prof Dk Ratlan Pardede aliwataka Waislamu katika umoja wao kuthamini matunda ya mwezi mtukufu wa Ramadhan na kutekeleza maagizo yake kwa manufaa yao ya kiroho, kijamii na kiuchumi.

Aidha Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini Hussein Hamadi alishukuru kwa hafla hiyo na kusema ni kitendo kinachokumbusha kuangalia haja ya umoja na kusaidia wasiokuwa nacho.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sanjay Rughani alisema kwamba hafla hiyo wameifanya kwa kutambua haja ya umoja katika tofauti za kidini zilizopo.

Alisema Benki yake imeandaa futari hiyo kwa kuzingatia kalenda yake katika kushiriki masuala ya kijamii yakiwemo matendo ya kidini.

Alisema matendo hayo ya kidini yanatekelezwa kwa lengo la kuheshimu dini za wateja wake na pia kuwakutanisha wateja na watendaji wakuu wa benki ili waweze kuwasilisha maoni yao.


Bw. Rughani pia alisema kwamba ili kuwawezesha wafanyakazi wake kushiriki kikamilifu katika mfungo wamefanya mabadiliko kadha yanayofanya mfungo kuwa rafiki na kazi zao.

UBA Restates Commitment to Growing Infrastructure, Deepens Financial Inclusion in Tanzania

UBA Tanzania, a subsidiary of the UBA Group, a pan African financial institution with presence in 20 African countries, Monday restated its commitment to support the Tanzanian government’s initiative to grow the country’s infrastructure, while also affirming the bank’s obligation to deepen the retail banking space in the country.
The assurance was given during a press conference addressed by the Bank’s Chief Operating Officer, Chris Byaruhanga in Dar Es Salaam, noting that as a member of UBA Group with asset of over $13 billion, the Tanzanian franchise has the capacity to finance any project irrespective of amount or size. “UBA Tanzania, relying on the strength of our group has capacity to finance any transactions irrespective of its size in either private or public sector. As a pan African with presence in key international markets of the world, we are positioned to provide the necessesary financial intermediation critical to the development of Tanzania,” says Byaruhanga.
Byaruhanga further informed the journalists of the key projects that have been financed by the Bank in Tanzania in recent times, including the provision of over $25 million facility for the construction of Kigogo Road in Dar Es Salaam and TZS15BN/- support Tanzania Electricity Supply Company (TANESCO), among other interventions. “Apart from these involvements, UBA Tanzania, a bank with strong retail base has come up with many innovations, especially in digital space to provide financial solutions to the needs of the banking consumers in this market,” the COO said while explaining the Bank’s strategy, claiming further that UBA Tanzania prioritises businesses whether they are small and medium scale enterprises (SMEs) or large corporates.
Speaking on the roles being played by UBA Group in the support of the economic development of the African continent, Nasir Ramon, Head, External Relations of UBA Plc, said UBA Group has continuously played big in the continent’s financial sector, saying that the UBA has committed over $5 billion into various projects on the continent in recent times.
United Bank for Africa is one of Africa’s leading financial institutions, with operations in 20 countries and 3 global financial centers: London, Paris and New York. From a single country operation in Nigeria, Africa’s largest economy, UBA has evolved into a pan-African provider of banking and related financial services through diverse channels globally.
UBA Tanzania is a subsidiary of UBA Plc and licensed by the Bank of Tanzania.  The Bank has been in Tanzania since 2009 and has continued to play a critical role in the Tanzania banking industry. UBA Tanzania offers a full range of banking products catering for large local corporates, public sector clients and multinational corporations that include trade finance lines, working capital facilities, collection solutions and robust payment platforms.

MKAZI WA NEWALA,SHAKILA AMRI ASHINDA MILIONI 140 SIKU YA MAMA DUNIANI

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema jana jijini Dar,wakati wa kumtambulisha mshindi Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku 'akimbust' Mama yake kwenye sehemu ya usindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.

  Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku akifafanua zaidi kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyofanikiwa kushinda kitita hicho cha TatuMzuka,aidha kufuatia ushindi huo Shakila pia  'alimbust' Mama yake kwenye sehemu ya ushindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.
 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku 'akimbust' Mama yake kwenye sehemu ya usindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.

Mchezo wa namba unaongoza nchini Tanzania wa Tatu Mzuka leo umemtangaza na kumtambulisha mbele ya vyombo vya habari mama aliyejinyakulia kitita cha milioni 140 na wakati huo ‘kumbusti’ mama yake kwenye sehemu ya ushindi wake.

Shakila Amri Nyani, ambaye ni mkazi wa Newala, Mtwara na mama wa watoto 3 alisherehekea siku ya mama duniani kwa kumpa mama yake milioni 30 kama ishara ya kutambua mchango wake katika siku hiyo muhimu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Bwana Sebastian Maganga alikuwepo kuwakab
idhi hundi Bi Nyani pamoja na mama yake. “Mama zetu ni hazina na hakuna kiwango chochote cha pesa kinachoweza kutosha kulipa upendo, msaada na kazi kubwa walioifanya katika kutulea. Kwa ushindi huu Tatu Mzuka tunaamini Bi Nyani na mama yake watafurahia na kuboresha maisha yao pamoja na familia zao” alisema Maganga

Bi Nyani, mwenye miaka 38 alikuwepo kuelezea furaha yake na namna ambavyo alicheza mpaka akapata ushindi huo mnono wa milioni 140.“ Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kwa muda mrefu sasa. Nina furaha kubwa sana. Sikuwahi hata kuota kama naweza kupata nafasi kama hii. Mimi ni mjasiriamali na ninapanga kutumia pesa nilizoshinda kuongeza mtaji wa biashara yangu” alisema Bi Nyani

Bi Fatuma Bakari ambaye ni mama mzazi wa Nyani aliishukuru Tatu Mzuka kwa kuja na kampeni ya ‘Wiki Maalumu ya mama’ ambayo imemfanya akabustiwa kwa pesa nyingi baada ya mtoto wake kushinda.“Mimi pia nitatumia pesa nilizobustiwa kuwabusti ndugu wengine na kufanya shughuli za maendeleo ili kuboresha hali ya maisha ya familia yangu.” Alisema Bi Fatuma

Maganga alimalizia shughuli kwa kutoa dondoo ya kampeni mpya ilioanza leo – Mzukapaswedi. “Na hapa kinachohitajika ni namba zako 3 tu!! Za Bahati, ambazo zitakufanya ufikie mafanikio yako,iwe ni kuongeza elimu,kununua gari,kujenga frame za maduka, kuwekeza kwenye kilimo, nk, fanikisha matunda ya mzuka-paswedi yako kwa ushindi wa laki 1 hadi millioni 6 kila saa.
Ushindi wa millioni 10 katika mzuka deile leo saa tatu na nusu usiku, na ushindi wa millioni 60, jumapili hii kuanzia saa 3 na nusu usiku, tuma 500 hadi 30,000 kwenda namba ya kampuni 555111, na kumbukumbu namba ni namba zako 3 za bahati zikifuatiwa na neno mzukapaswedi kutoka 3mzuka, ukishinda Tanzania inashinda...

Tatu Mzuka yatangaza ushirikiano wa kibiashara na Wema Sepetu


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar kuhusu Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, kutangaza kuanza ushirikiano wa kibiashara na mrembo maarufu nchini Bi. Wema Sepetu pichani kushoto.

‘Muda wote tunaangalia kipaji ambacho tunahisi kinaendana na bidhaa yetu na hivyo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Katika biashara yetu tayari tuna ushirikiano na Millard Ayo, Brother K, Shilawadu na wengine wengi na leo tunatangaza kumwongeza Wema Sepetu kwenye orodha hiyo’ alisema Maganga.

Wema ambaye alikuwepo pia kuelezea furaha yake baada ya kutangaza ushirikiano na Tatu Mzuka, alisisitiza kwamba ana hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha mashabiki wake mambo mazuri ambayo amewaandalia.

Bi Wema Sepetu akizungumza mbele ya waanidishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, kutangaza kuanza ushirikiano nae wa kibiashara .

Wema Sepetu akifurahia jambo mara baada ya kutangazwa ushirikiano wake na kampuni ya The Netwek-ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania.


Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, leo imetangaza kuanza ushirikiano wa kibiashara na mrembo maarufu nchini Bi. Wema Sepetu.

Ushirikiano huu ni mwendelezo wa mpango mkakakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania katika kuboresha maisha yao. Kusudi hasa la Tatu Mzuka kama ilivyoelezwa ni kusambaza fursa kwa watu wengi kadri inavyowezekana ili kubadilisha maisha yao.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga alisema kwamba ushirikiano huu ni mmojawapo kati ya nyingi ambazo Tatu Mzuka wanajihusisha nazo.‘Muda wote tunaangalia kipaji ambacho tunahisi kinaendana na bidhaa yetu na hivyo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Katika biashara yetu tayari tuna ushirikiano na Millard Ayo, Brother K, Shilawadu na wengine wengi na leo tunatangaza kumwongeza Wema Sepetu kwenye orodha hiyo’ alisema Maganga.

Wema ambaye alikuwepo pia kuelezea furaha yake baada ya kutangaza ushirikiano na Tatu Mzuka, alisisitiza kwamba ana hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha mashabiki wake mambo mazuri ambayo amewaandalia.‘Ninawashukuru sana Tatu Mzuka kwa ushirikiano huu, ambao hakika sio tu utanigusa mimi bali mashabiki zangu na watanzania kwa ujumla wao katika kujitengenezea fursa za kuboresha maisha yao’ alisema Wema.

Wema alisema kwa kuanza, anaomba mashabiki zake wachangamkie fursa ya kucheza Tatu Mzuka, ambapo kama unatumia MPESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY, unaingiza namba ya kampuni ambayo ni 555111 na baada ya hapo unaweka namba zako 3 za bahati zikifuatiwa na jina langu WEMA na baada ya hapo ingiza kiasi unachotaka kuanzia shilingi 500 mpaka 30,000.

‘Pamoja na kujiongezea nafasi za kushinda za kawaida za Tatu Mzuka kila saa hadi milioni 6, kila siku unaweza kushinda milioni 10 pamoja na zaidi ya milioni 140 kila Jumapili, utapata fursa zaidi ya zawadi mbalimbali kutoka kwa Wema’ alisema Wema. Pamoja na utambulisho wa Wema, Tatu Mzuka pia ilitangaza kwamba Jumapili hii ya tarehe 13 ambayo ni siku ya mama duniani kuna milioni 140 ambayo lazima itolewe kwa mtu mmoja pamoja na mama yake.

‘Hii ni fursa kwa kila mtanzania ambaye kwa namna moja ama nyingine angependa kumshukuru mama yake au mlezi wake kwa kazi kubwa aliyofanya, na hivyo ukicheza sasa, unaingia kwenye Mzuka Deile ambayo inafanyika kila siku Jumatatu hadi Jumamosi, ambapo milioni 10 lazima itoke kwa mtanzania mmoja na yeye atamgawia mama yake milioni 3, wakati Jumapili hii kwenye Mzuka Jackpot yeyote atakayeshinda milioni 140 atambusti mama yake kwa milioni 30’ alihitimisha Maganga

UBA Shareholders Hail Performance, Higher Dividend Payout

Group Managing Director/CEO, United Bank for Africa(UBA) Plc, Mr. Kennedy Uzoka, Group Chairman, UBA Plc, Mr. Tony Elumelu; Company Secretary, Mr. Bili Odum; and Group Deputy Managing Director, Mr. Victor Osadolor, at the 56th Annual General Meeting of the Bank held in Lagos
 Group Managing Director/CEO, United Bank for Africa(UBA) Plc, Mr. Kennedy Uzoka; Group Chairman, UBA Plc, Mr. Tony Elumelu; Company Secretary, Mr. Bili Odum; Group Deputy Managing Director, Mr. Victor Osadolor; and Director, Ambassador Adekunle Olumide, at the 56th Annual General Meeting of UBA Plc  held in Lagos on Monday


Shareholders of United Bank for Africa (UBA) Plc on Monday hailed the board and management of the bank for the impressive performance recorded in 2017 and were highly pleased with the remarkable contributions of its African subsidiaries that accounted for over 45 percent of the group’s income.
The shareholders gave the commendation at the 56th annual general meeting in Lagos. UBA posted profit after tax (PAT) of USD237 million for the 2017 financial year and recommended a total dividend of 0.3 USD cents per share, which was ratified at the AGM. Speaking at the meeting, the Chairman, Progressive Shareholders Association of Nigeria, Mr. Boniface Okezie: “I want to specially commend the Board and Management of UBA, especially the Chairman, Tony Elumelu and Group Managing Director/CEO, Kennedy Uzoka, whose leadership, has brought tremendous progress to this great institution in the past two years. We, the shareholders, are impressed with results that you have recorded so far and the achievements that the bank has recorded under your leadership, especially the sterling contributions of our subsidiaries in Africa. We are impressed with the continuous penetration of the Group’s franchise and market share gain across Africa. UBA has further demonstrated that Africa can nurture great companies and great things can be originated from Africa. UBA has showcased a high level of ingenuity in the banking space, and we are glad with the attendant value creation for shareholders and the broader stakeholders.”
Another shareholder, Mr. Timothy Adesiyan, commended the Management for being the African bank to pioneer Artificial Intelligence technology, with the launch of UBA’s Virtual Banking Robot, named “Leo”, a Chatbot which enhances lifestyle banking, as it enables customers to carry out all forms of basic banking transaction through Facebook chat. Also, speaking at the General Meeting of Shareholders of the Group, Nonah Awoh, who commended the bank for the performance, equally tasked the management to do more to ensure that all the African subsidiaries contribute at least 50 per cent to the bottom-line of the Group in the near future.
In his address to shareholders, Elumelu, said the bank recorded strong growth in both top and bottom lines in 2017.
He said: “Overall, our bank grew profit before tax by 16.1 per cent to USD318 million. More importantly, the bank remains financially strong, with BASEL II capital adequacy ratio of 20% well ahead of the 15% regulatory requirement in Nigeria and the Group’s capital adequacy ratio of 25% ranks one of the highest amongst Sub-Sahara African banking groups. More importantly, the Group remains very liquid, reinforcing the strength of our balance sheet. We recently opened for business in Mali, as we see the economy of Mali to be very viable, with strong growth prospects for us and other corporates in that market. Mali is a strategic fit for our Group and this time and the corporates and SMEs in Mali will benefit from our expertise and banking capacity in varying sectors of the economy, in addition to our value proposition to the retail customers, who can efficiently leverage our digital banking offerings to facilitate their banking transactions with ease. Hence, we see us adding a lot of value to the Malian economy and we expect positive profit contribution to our Group from this new subsidiary, going forward.  
On his part, Uzoka, the Group Managing Director/CEO said: “UBA has built a great brand that is recognised all over the world, and because of this, we have decided to be customer centric. This means our focus is on putting our customers first in all we do by making sure that we do things from the customers’ standpoint.”

MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

 Msanii Diamond akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es alaam (katikati) ni Sealouise Shayo, Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini (kulia) ni Meneja wake Sallam SK.
 Msanii Diamond na Nahreel katika mkutano wa waandishi wa habari, wengine ni maofisa wa Coca-Cola na mameneja wa msanii Diamond.
Maofisa wa Coca-Cola wakiwa katika picha ya pamoja na Diamond na Nahreel baada ya mkutano na waandishi wa habari.

Msanii nguli wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushirikiana na kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba wimbo utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 uitwao Colours.

Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha kupata fursa ya kushiriki kuimba kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla.

“Kwangu hii ni nafasi nyingine ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa kitanzania sambamba na lugha ya Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki kuimba nimetumia lugha ya taifa la Tanzania ambayo inazidi kupata umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond

Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. “Tuna imani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano haya”alisisitiza.

Prodyuza nguli wa muziki nchini na kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel ,ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa. “Ninayo furaha ya kufanya kazi na Diamond kwa mara nyingine katika tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia heshima kubwa tuliyopewa”

CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akionyesha vipeperushi vya kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitangaza kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu. 

Benki ya CRDB leo imetangaza kuanza rasmi kwa kampeni ijulikanayo kama “Furahia kandanda murua nchini Urusi” #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiaji wa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Urusi, kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo Bi. Tully Esther Mwambapa, alisema kuwa Benki ya CRDB imeanzisha kampeni kwa kushirikiana na kampuni ya Visa International ili kutoa fursa kwa wateja wake kwenda kushuhudia fainali hizo, ambazo huvutia hisia za watu wengi dunuani kote.

“Wateja wetu wenye TemboCardVisa, TemboCardVisa-Electron, TemboCard Visa-Gold, TemboCardVisa- Platinum na TemboCardVisa-Infinite, wakati wa kampeni hii watatakiwa kulipia bidhaa au huduma wanazonunua kwa kutumia TemboCardVisa zao kupitia mashine za malipo (POS) zilizopo sehemu mbalimbali kama kwenye migahawa, maduka, mahospitali, vituo vya mafuta na kwingineko, ili waweze kujishindia zawadi hii kubwa” alisema.

Bi.Mwambapa aliendelea kusema kuwa “iii mteja aweze kushinda, anatakiwa kufanya miamala mingi zaidi kila wiki na kadri mteja anavyolipia zaidi kwa kutumia TemboCardVisa yake, ndivyo anavyojiongezea nafasi kubwa zaidi ya kushinda.

Washindi wa wawili watakaokuwa wamefanya miamala mingi zaidi kila wiki watajishindia safari ya kwenda Urusi ambayo itagharamiwa kila kitu na Benki ya CRDB, ambapo jumla ya tiketi 24 zitatolewa” alisema Bi. Tully Mwambapa.

Bi.Mwambapa aliendelea kusema kuwa pamoja na washindi wawili wa kwanza kujishindia safari hiyo, Benki pia kila wiki itatangaza washindi wengine 10 kupitia vyombo mbalimbali vya habari ambao watajishindia zawadi kemkem ikiwemo luninga zitakazokuwa zimeunganishwa na kulipiwa kinga’muzi cha DSTV, jezi za timu za mataifa mbalimbali, mipira, kofia, fulana na na zawadi zingine nyingi.

TRADEMARK EAST AFRICA AND CENTRAL CORRIDOR TRANSIT TRANSPORT FACILITATION AGENCY SIGN FINANCING AGREEMENT


TradeMark East Africa (TMEA) Tanzania Country Director, John Ulanga (L) hands over a Memorandum of Association (MoU) to the Executive Secretary of Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) Captain Dieudonne Dukundane (R) during the ceremony of signing a financing agreement to provide a total of USD 1.3m (Equivalent to approximately TZS 2.86 billion) over a 3-year period (2018 to 2021) held in Dar es Salaam last week. (Photos by Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG).
 TradeMark East Africa (TMEA)  Tanzania Country Director, John Ulanga explain to journalist how the TradeMark East Africa (TMEA) and the Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency whey are working. TradeMark East Africa (TMEA) is an aid-for-trade organization that was established with the aim of growing prosperity in East Africa through increased trade. TMEA operates on a not-for-profit basis and is funded by the development agencies of the following countries: Belgium, Canada, Denmark, Finland, the Netherlands, Norway, UK, and USA. TMEA works closely with East African Community (EAC) institutions, national governments, the private sector and civil society organizations.
Executive Secretary of Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) Captain Dieudonne Dukundane (C) explaining a few things to the journalist about their publications that help traders in offering them various education.
TradeMark East Africa (TMEA) and the Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) have signed a financing agreement geared towards strengthening and enhancing the Central Corridor Transport Observatory (CCTO).

The financing will specifically improve monitoring of the Central Corridor performance in-order to support evidence-based advocacy and decision making to remove trade barriers. To that effect, TMEA will provide a total of USD 1.3m (Equivalent to approximately TZS 2.86 billion) over a 3-year period (2018 to 2021).

“TradeMark East Africa is delighted to provide this support to CCTTFA because the organization is producing reliable and timely data on the performance of the Central Corridor Transport Network. This support therefore will further strengthen that work and enable the countries served by the corridor to design interventions to further improve performance of the corridor” said John Ulanga, the Tanzania Country Director.

“CCTTFA highly appreciates this funding support from TMEA for our Central Corridor Observatory work, the funding will go a long way to support our ongoing efforts and enable us to work with various stakeholders in central corridor partner states to further improve efficiency of the corridor and hence increase the volume of trade going through the corridor for the benefit of the countries”. said Captain Dieudonne Dukundane, Executive Secretary of CCTTFA.

To accomplish the above, the CCTTFA will enhance the CCTO into a one stop center platform for availing and accessing relevant information and data related to movement of goods along the Corridor.

Specifically, this support will enable CCTTFA maintain and improve the current online information portals, develop mobile data collection tools, roll out the central corridor dashboard to other member states, develop trade costs and transport predictive models and develop tools to monitor processes and effectiveness of initiatives along the Central Corridor.

Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kulia) wakimwongoza Mwakilishi wa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji  wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (katikati) kuelekea ukumbini mara baada ya kuwasili katika hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji  wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (wa pili kulia) akisamiana na kubadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) na na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto).
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) akibadilisha mawazo na Mwakilishi wa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji  wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (wa pili kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) pamoja na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji  wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Idara ya Makampuni Benki ya Standard Chartered, James Meitaron wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini, Mh. Wang Ke (wa tatu kulia) akisalimiana na mwakilishi wa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji  wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi (kulia) mara baada ya kuwasili ukumbini wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (wa pili kulia), Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered nchini, Ami Mpungwe (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto).
Meneja Bidhaa wa Benki ya Standard Chartered, Busara Raymond (kushoto) akitoa maelezo kwa Balozi wa China nchini, Mh. Wang Ke (wa pili kulia) kuhusu mashine ya kuwekea fedha ambayo inajisoma moja kwa moja kwenye matawi ya benki yenye uwezo wa kuweka zaidi ya milioni 100 mashine hiyo yenye teknolojia ya Afrika ya Kusini inawekwa kwa mteja anayehitaji kuweke fedha salama kwenye miamala yake wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani (kulia) Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered nchini, Ami Mpungwe (wa tatu kushoto)
Mchoraji Nicodemus Zebedayo akichora baadhi ya nyuso za wageni waalikwa waliohudhuria hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya zawadi ya kumbukumbu kwa waalikwa. Kulia ni mmoja wa wageni waalikwa akitazama uchoraji wa picha hizo ukiendelea.
Baadhi ya wageni waalikwa wakitazama picha za nyuso zao kwenye bango maalum ikiwa sehemu ya zawadi ya kumbukumbu kwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji  wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyoandaliwa na benki yake ambayo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini, Mh. Wang Ke akitoa nasaha kwa wageni waalikwa wakati wa hafla wa maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya meza kuu kutoka kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered nchini, Ami Mpungwe, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani , Balozi wa China nchini, Mh. Wang Ke pamoja na Mwakilishi wa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji  wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered wakibadilishana mawazo wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Wasanii Derick Kahabwa na mpiga gitaa Hainan wakitumbuiza kwenye hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Burudani maalum ya tamaduni ya watu wa China wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifurahia burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendelea wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki Standard Chartered wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakijisevia bufee wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki Standard Chartered wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu
CHINA katika kipindi cha miaka mitatu ijayo inatarajia kuwekeza katika viwanda 200 nchini Tanzania vitakavyokuwa na uwezo wa kuajiri moja kwa moja Watanzania laki mbili.
Kwa sasa uwekezaji wa China nchini Tanzania umetoa fursa za ajira za moja kwa moja  150,000 na zisizokuwa za moja kwa moja 350,000.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage katika hafla  ya chakula cha jioni kwa wawekezaji kutoka China iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered.
Aidha Waziri Mwijage alisema amefurahishwa na kauli iliyotolewa na Benki hiyo kwamba inawekeza dola za marekani bilioni 20 sawa na fedha za kitanzania trilioni 40 katika kampeni ya China ya uwezeshaji mitaji na biashara kutoka Asia kwenda nchi nyingine za dunia.
Kampeni hiyo inayoitwa One Belt One Road inagusa nchi 65, Tanzania ikiwamo.
Aliisifu Benki hiyo kwa kuandaa hafla hiyo kwa wateja wake wa China ikiwa ni sehemu moja ya kutangaza kampeni  hiyo ya China na kuwafanya wananchi wengi kuelewa fursa zinazoambatana nazo.
Alisema kwa sasa Tanzania inapigana kuingia katika uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda na kampeni ya China inakwenda sawa na mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliokazania uwekezaji katika viwanda.
Alisema kwa sasa Serikali inaweka vyema mazingira ya uwekezaji na ikiwa na uchumi unaokua kwa kasi wa asilimia  6 hadi 7 juhudi za Benki hiyo za kuonesha fursa za uwekezaji na uendeshaji wa uchumi  zinakaribishwa na serikali ya Tanzania.
Aidha katika hotuba hiyo iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji  wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi  alisema kwamba mpango huo wa China unaozungumzia uwezeshaji wa mitaji na biashara kutoka Asia kwenda nchi nyingine ni kichocheo cha kukua kwa chumi mbalimbali duniani na kutaka watanzania kushiriki kikamilifu.
Awali Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo nchini Tanzania, Sanjay Rughani  alisema kwamba Benki ya Standard Chartered duniani inawekeza katika Belt and road Initiative kiasi cha dola bilioni 20 sawa na  shilingi trilioni 44.8 za Kitanzania kuwezesha miradi mbalimbali kwenye kampeni hiyo ya China.
Alisema mwaka jana pekee benki hiyo iliingiliana mikataba katika miradi 40 kwenye nchi mbalimbali za mradi huo.
“Standard Chartered imewekeza katika nchi 45 za kampeni ya belt and Road zenye msukumo mkubwa wa shughuli zikiwemo nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, Kusini mwa Asia na Afrika” alisema na kuongeza kuwa kazi yao kubwa ni kutoa mitaji ya kifedha ikiwamo mikopo na kuwezesha miamala mbalimbali.

Aidha alisema asilimia 50 ya mikataba hiyo na shughuli zilizofanywa kwa mwaka 2017 zilikuwa Afrika huku asilimia 25 zikienda Kusini mwa Asia na nyingine ni katika maeneo mbalimbali ya kampeni.
Alisema pamoja na kuishiriki moja kwa moja pia benki ya Standard imekuwa ikishirikiana na taasisi nyingine za fedha kusaidia wateja mbalimbali wa kwenye kampeni hiyo.
Alitaja washirika wao wengine kuwa AIIB, Silk Road Fund, China Development Bank, China Exim Bank na benki nyingine za kibiashara za China.
Alisema ikiwa na historia ya miaka 150 na kuaminika vya kutosha na wateja mbalimbali wamekuwa wakitumia utaalamu na elimu waliyonayo katika kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji katika nchi zinazohusika na kampeni ya mitaji kutoka asdia kwenda nchi nyingine.
Rughani alisema  benki  hiyo ina madawati katika nchi mbalimbali yanayoshughulikia wawekezaji kutoka China kwa lengo la kuwawezesha kutambua mazingira ya uwekezaji katika nchi husika na kuwafanya wawe na uhakika na uwekezaji wao.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke alisema kwamba taifa lake linaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kuwezesha maendeleo kwa nchi washirika katika kampeni iliyoanzishwa takribani mikaa mitatu iliyopita ambayo inakwenda hadi mwaka 2020.
Alisema amefurahishwa sana na juhudi za Benki hiyo katika kutumia fursa iliyonayo kuhamasisha uwekezaji na kuwezesha China na washirika wake wa maendeleo kuwa na uhakika na shughuli na fursa za uwekezaji kwa kuzingatia kampeni ya One Belt One Road.
Biashara ya China na mataifa hayo 65 katika kampeni hiyo, ilizidi dola za Marekani trilioni 3 kati ya mwaka 2014 hadi 2016 na kwamba uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika nchi hizo umepita dola za Kimarekani bilioni 129 kufikia mwaka 2016 kutoka dola bilioni 92 mwishoni mwa mwaka 2014.