Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (wapili kushoto) na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Water.Org, Eng. Francis Musinguzi kwa
pamoja wakionesha mikataba ya ushirikiano mara baada ya kusaini
makubaliano ya ushirikiano katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya
Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam tarehe 18 Julai 2024. Wangeni
pichani ni wanasheria wa Benki ya CRDB na Shirika la Water.Org.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (wapili kushoto) na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Water.Org, Eng. Francis Musinguzi
wakibadilishana mikataba ya ushirikiano ushirikiano katika hafla fupi
iliyofanyika makao makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam tarehe 18
Julai 2024.
========= ========
Dar
es Salaam. Tarehe 18 Julai 2024: Benki ya CRDB imesaini mkataba wa
makubaliano na shirika la Water.Org Afrika unaolenga kuboresha
upatikanaji wa maji safi na mazingira safi katika maeneo mbalimbali
nchini. Ushirikiano huu unaonyesha dhamira ya Benki ya CRDB katika
kuchangia maendeleo endelevu na ustawi wa jamii.
Akizungumza
katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki hiyo, Bruce Mwile
alisema kuwa makubaliano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Benki
ya CRDB ambayo inaelekeza katika kutoa suluhisho bunifu kwa jamii ili
kukuza ustawi wa wadau wake.
"Tunajivunia
kuona tunaendelea kuishi azma yetu ya kuchochea ustawi wa jamii kupitia
ubia wa kimkakati na wenzetu wa Water.Org. Nizishukuru timu zetu za
kitaalamu ambazo zimefanya kazi kubwa hadi kufikia hatua hii ambayo
inatoa fursa kwa jamii kunufaika na uwezeshaji katika sekta ya maji na
usafi," alisema Mkurugenzi huyo.
Mwile
amesema ushirikiano huo utawezesha miradi ya sekta ya maji pamoja na
usafi wa mazingira kwa kutumia fedha zitakazotengwa katika maeneo
mbalimbali. Miongoni ya maeneo hayo ni pamoja na utafiti na ufadhili wa
miradi ya maji na usafi wa mazingira, mikopo ya miundombinu ya maji na
usafi.
Benki
hiyo intarajia pia kutoa mikopo midogo kwa watu binafsi, wajasiriamali,
biashara, na taasisi kwa ajili ya kufunga miundombinu ya maji ya
nyumbani, vifaa vya matumizi ya maji kwa ufanisi, na ujenzi wa vyoo na
matangi ya maji safi na maji taka.
Aidha
alisema mikopo hiyo pia itaelekezwa kwa sekta ya kilimo hususani kwa
wakulima wanaotumia mifumo ya umwagiliaji yenye matumizi ya maji kwa
ufanisi. “Ushirikiano huu pia utawezesha uanzishwaji wa huduma za bima
zitakazotoa ulinzi dhidi ya majanga yanayoathiri miundombinu ya maji.”
aliongezea Mwile.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu Water.Org, Injinia Francis Musinguzi
amesema kuwa ushirikiano huu unalenga kwenye kuboresha maisha ya jamii
inayotuzunguka pamoja na hayo aliongezea kuwa utawezesha ufadhili wa
tafiti za hatifungani za maji na usafi wa mazingira, pamoja na
kuanzishwa kwa miradi endelevu ya maji na usafi.
“Ushirikiano
huu pia utawezesha ufadhili wa tafiti za ushirikiano kati ya sekta ya
umma na binafsi katika kufadhili miradi mikubwa ya usambazaji maji na
usafi, pamoja na ufadhili wa bunifu za usimamizi wa maji kwa
teknolojia,” alisema Injinia Musingizi.
Katika
eneo la elimu na uhamasishaji, Benki ya CRDB na Water.Org
watashirikiana kufadhili kampeni za elimu na uhamasishaji kuhusu umuhimu
wa usafi ili kuzuia magonjwa, kupitia taasisi ya CRDB Bank Foundation
ambayo imejikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii na kutoa mitaji
wezeshi kwa wajasiriamali wanawake na vijana.
Makaubaliano
ambayo Benki ya CRDB imeingia na Water.Org ni mwendelezo dhamira yake
ya kuchangia ufikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa
Mataifa (SDGs), hususan Lengo namba 6, 'Maji Safi na Usafi wa
Mazingira'.
No comments:
Post a Comment