HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MADAKTARI WA KICHINA WAJITAMBULISHA NA KUAGA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Kichina wanaotoa huduma katika Hospitali mbali mbali za Unguja na Pemba wakiongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa tatu kulia) katika mazungumzo yao aliwakaribisha Madakatari 21 wapya na kuwaaga 21 waliomaliza muda kutoka  Jamhuri ya Watu wa China katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Kichina unaoongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa pili kushoto) katika mazungumzo yao Rais aliwakaribisha Madakatari 21 wapya na kuwaaga 21 waliomaliza muda kutoka  Jamhuri ya Watu wa China (hawapo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,(kushoto) Kiongozi wa Madakatari waliomaliza muda Xu Zhuoqun.
 Baadhi ya Madakatari wa Kichina waliofika Ikulu Mjini Unguja kuoanana na Rais leo ambapo jumla yao ni  Aroubaini na mbili wakiwemo wapya Ishirini na moja wanaomaliza muda wao wa kazi waliofika kumuaga Rais na Ishirini na Moja walikaribishwa na Rais katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  Ujumbe wa Madaktari wa Kichina unaoongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa nne kushoto) baada ya mazungumzo na kuwaaga Madaktari hao waliomaliza muda wao wa kazi hapa Nchini, leo walipofika Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimkaribisha Kiongozi wa Madaktari wapya Ishirini na moja kutoka Jamhuri ya Watu wa China Wang QI baada ya mazunguzo na Madaktari hao waliofika Ikulu Mjini Unguja leo wakiongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (katikati) Kiongozi wa Madaktari waliomaliza muda Xu Zhuoqun.

RAIS DK.SHEIN AWAAPISHA MKUU WA JKU NA MKUU WA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimvalisha cheo cha Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Nd,Ali Abdalla Ali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa  Naibu Kamishana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Ali Abdalla Ali kuwa  Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa  Naibu Kamishana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad  kuwa   Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU )  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Baadhi ya Makamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU na Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakiwa katika hafla ya kuwapishwa wakuu wao Wapya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika Ukumbi wa wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (kulia) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Said Hassan Said na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali  baada ya kuwaapisha rasmi  Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Abdalla Ali kuwa (wa nne kushoto) na Kanal Ali Mtumweni Hamad   Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar  JKU  (wa nne kulia)  hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. (Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Viongozi wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu katika Vikosi hivyo. 

Katika hafla hiyo, Dk. Shein kabla ya kumuapisha Naibu Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Ali Abdalla Ali, alimfisha cheo cha Ukamishna na baadae kumuapisha kuwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.

Wakati huo huo, Dk. Shein, amemuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU).

Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za (SMZ), Haji Omar Kheir, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.

Wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,  Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

DK. SHEIN ATOA MSAADA KWA WANANCHI WA PEMBA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU, WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO

  MAGODORO 80 yaliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, yakiwa kwenye uwanja wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, kabla ya kugawiwa kwa waathirika wa mvua wa mkoa huo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Chakechake Salama Mbarouk Khatib, kila wilaya magodoro 40, yaliotolewa msaada na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya aathirika wa mvua wa wilaya zao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Chakechake Salama Mbarouk Khatib, kila wilaya magodoro 40, yaliotolewa msaada na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya aathirika wa mvua wa wilaya zao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, akitoa neno la shukuran, mara baada ya kukabidhiwa magodoro 40 na Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, kutoka kwa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar dk Ali Mohamed Shein kwa ajili ya waathirika wa mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

UNGA wa ngano polo 112, uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein pmoja na Mchele na Sukari idadi kama hiyo, kwa ajili ya wananchi wa Pemba, wanaoishi kwenye mazingira magumu, ambapo chakula hicho ni sadaka, inayotolewa kila mwezi wa ramadhan na rais wa Zanzibar kwa ajili ya futari, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MJUMBE wa kamati ya zaka na sadaka ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ndgu Haji Nassib Nyanya, akimkabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, mchele, sukari na unga wa ngano, chakuka chenye thamani ya shilingi milioni 40, ikiwa ni sadaka iliotolewa na Rais Zanzibar, kwa ajili ya futari ya wnananchi wanaoishi kwenye mazingira magumu kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla akizungumza kabla ya kuwakabidhi wakuu wa wilaya ya Mkoani na Chakechake, saruji paketi 150 kila wilaya, zilizotolewa na Rais wa Zanzibar, kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na mafuriko ya mvua ilionyesha hivi karibuni, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, na Mkuu wa wilaya Chakechake, Salama Mbarouk Khatib, saruji paketi 150 kila wilaya, iliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya waathirika wa mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

Rais Dk.Shein azungumza na Wauguzi na Wakunga

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar walipokuwa wakimsikiliza   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza nao leo  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar pamoja na Viongozi wengine baada ya mazungumzo yalitofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo,(Picha na Ikulu)

BRIGEDIA JENERALI FADHIL OMAR NONDO AJITAMBULISHA KWA RAIS DK.SHEIN

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo baada ya mazungumzo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar (Picha na Ikulu)

Rais wa Zanzibar Dk.Shein akutana na Balozi wa Morocco

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ikulu)

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO KUTUNZA TAARIFA NA MFUMO WA KUKUSANYIA MAPATO KIELEKTRONIKI

 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akihutubia baada ya wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) na na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akihutubia katika Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) wakati wa kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akitoka kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika la simu Tanzania TTCL Bw. Waziri Kindamba wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre)  na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Bw. Joseph Kichere wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre)  na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akionesha Ipad maalumu aliyopewa ili kumuwezesha  kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwake ni  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  akionesha Ipad maalumu aliyopewa kumuwezesha  kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. kushoto kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akionesha Ipad maalumu itayomuwezesha kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akishuhudiwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akizindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa makampuni ya mawasiliano mbalimbali nchini kwenye sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa Mabenki mbalimbali nchini sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu

RAIS WA ZANZIBAR AREJEA NCHINI AKITOKEA DJIBOUTI.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Moahammed Mahmoud mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Wakuu wa Vikosi vya SMZ mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein wa kwanza kulia akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.