HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGA TAMASHA LA UELIMISHAJI NA UPIMAJI AFYA NA KINGA DHIDI MAGONJWA YASIOAMBUKIZA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akihutubia wakati wa Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasioambukiza kwa watoto na vijana lililofanyika kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi, mgeni rasmi kwenye Tamasha hilo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Watoto wakionesha umahiri wao katika kucheza ngoma za asili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu watoto waliotoka kupata chanjo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kote nchi kuwafichua watu wanaonyanyasa na kudhalilisha watoto kijinsia ili waweze kukamatwa na kuchukua hatua za kisheria kama hatua ya kukomesha vitendo hivyo ambayo vimeanza kushamiri katika baadhi ya jamii nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kuhitimisha kampeni ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ilitoa huduma bure za vipimo na matibabu kwa watoto na vijana zaidi ya 1500 kampeni ambayo iliambatana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika viwanja vya Shule ya msingi Kinyerezi mkoani Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais amesema kuwa watenda maovu hao lazima vifichuliwe na wananchi, walezi pamoja na wazazi kwa kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa watoto wapo miongoni mwa jamii.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola kutofumbua macho vitendo hivyo bali pindi wanapopata taarifa za matukio ya udhalilishaji wa watoto wachukue hatua za haraka za kuwakamata na kuwachukulia hatua stahiki watu wanaofanya vitendo hivyo vibaya.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kote nchini waache kuwaficha watu wanaotendea vitendo hivyo vibaya bali wawapatie taarifa walimu wao na polisi ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kwa kufanya hivyo watoto watakuwa salama katika mazingira ya nyumbani na wakiwa mashuleni kwani watu wabaya wanaofanya vitendo hivyo watawajibishwa kulingana na matendo maovu waliyokuwa wanawafanyia watoto hao.

“Mtoto anaweza kufaidika na fursa sawa iwapo tu atalindwa kwa kuwezeshwa kuwa afya bora”, Amesisitiza Makamu wa Rais.

 Kuhusu kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameendelea kuua watu kwa kasi katika nchi zinazoendelea Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania.

Amesema ipo haja ya kuimarisha juhudi za kukabiliana na tatizo hilo kwa ushirikiano wa wadau wote kwani janga hilo linagharimu taifa na wananchi wake wakiwemo watu wazima, watoto na vijana.

“Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yasipodhibitiwa yatapunguza uzalishaji mali,ufanisi mahali pa kazi na hata shughuli za ulinzi na usalama nchini mwetu na hivyo pato la taifa litapungua na taifa kuwa watu maskini kutokana na magonjwa hayo”, Alifafanua Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza Serikali imeweza kupanua maeneo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa saratani nchini kwa kujenga jengo jipya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na kuongeza majengo mapya ya huduma za saratani kwenye Hospitali za Rufaa ya kanda ya Bugando mkoani Mwanza.

Amesema Serikali pia imejenga Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambayo ni taasisi ya mfano ya kutibu maradhi ya moyo ambapo kutokana na kujengwa kwa taasisi hiyo Serikali imefanikiwa kuokoa mabilioni ya fedha ambayo yangetumika kuwagharamia wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamisi Kingwangala amemhakikishia Makamu wa Raia kuwa Wizara hiyo itaendelea kuweka mipango na mikakati imara ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini.

Dkt Kingwangala ameomba wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kidini na wadau wengine kushirikiana na Wizara ya Afya katika kuongeza kasi ya kukabiliana na magonjwa hayo ili yasiendelee kuteketeza maisha ya watu nchini.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

DC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA MAAFISA WATENDAJI ,AWATAKA KUKATAA MIRADI WASIYOITAMBUA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amewataka maafisa watendaji wa mitaa,vitongoji,vijiji na kata kuwa chachu ya maendeleo kwa kushirikiana kikamilifu na madiwani wao ili kuwaletea maendeleo wananchi huku akiwataka kukataa miradi wasiyoielewa katika maeneo yao.


Matiro ameyazungumza hayo leo May 24,2017 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya maafisa watendaji wa mitaa,vitongoji,vijiji,kata na maafisa tarafa katika manispaa ya Shinyanga yaliyolenga kuwajengea uwezo katika utendaji wao yaliyofanyika katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna katika manispaa hiyo.

Matiro aliwataka maafisa watendaji kuwa makini na miradi inayoanzishwa katika maeneo yao ili kuepuka kwenye lawama na migogoro inayoepukika na kukwamisha maendeleo katika jamii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna.Kulia ni mwenyekiti wa mafunzo hayo Simon Mpaname.Wa kwanza kushoto ni Afisa Utumishi wa Manispaa ya Shinyanga Magadi Magezi akifuatiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi.


“Tunahitaji kuwa na ushirikianona kufanya kazi kwa umoja,nitasikitika sana kuona mradi unapelekwa kwenye kata yako lakini afisa mtendaji hauufahamu,ikitokea hivyo ukatae huo mradi kwani inapotokea mradi huo unaharibika atakayeulizwa ni wewe,kwa hiyo lazima ujue vyema mradi uliopo katika eneo lako ili kuepuka shida”,alieleza Matiro.

“Nilishawaambia hata wataalamu wa halmashauri zetu kuwa wanapokwenda kwenye kata au vijiji wawashirikishe maafisa watendaji kwa wao ndiyo wasimamizi wakuu wa miradi lakini mnaweza kusimamia miradi hiyo ikiwa mnaitambua na miradi ambayo hamuitambui ikataeni”,aliongeza Matiro.

Katika hatua nyingine alisema serikali haitasita kuchukua hatua kwa watendaji watakaoisababishia serikali hasara kupitia fedha mbalimbali zinazotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo.

Aidha Matiro aliwasisitiza maafisa watendaji hao kusimamia vyema suala la ukusanyaji wa mapato na kusimamia vyema suala la ulinzi na usalama katika maeneo yao.

Matiro alitumia fursa hiyo kuwakumbusha maafisa watendaji kutatua matatizo ya wananchi kwa kuhakikisha kuwa wanatenga siku maalum za kusikiliza kero za wananchi.

Naye Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi aliwataka maafisa watendaji hao kusimamia vyema utaratibu wa kusoma mapato na matumizi kwa wakati.

Mwangulumbi pia aliwaagiza maafisa watendaji kutoa ushirikiano kwa maafisa ardhi wakati wa kupima ardhi,kutunza mali za ofisi na kukusanya mapato katika maeneo yote ya biashara.
Nao washiriki wa mafunzo hayo walisema yawasaidia kiutendaji kwani wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo wajibu wao,umuhimu wa kufuata taratibu za kazi,kusimamia miradi,uandishi sahihi wa vitabu na nyaraka za serikali,masuala ya ulinzi,rushwa na tahadhari ya majanga ya moto.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kwa maafisa watendaji wa mitaa,vitongoji,vijiji na kata pamoja maafisa tarafa wa manispaa ya Shinyanga katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna leo May 24,2017-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog.

Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo ukumbini.

Maafisa mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.

Afisa Utumishi wa Manispaa ya Shinyanga Magadi Magezi akizungumza ukumbini.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akisisitiza jambo ukumbini.

Mwenyekiti wa mafunzo hayo Simon Mpaname akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

DC WA ARUMERU AHOJIWA NA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti akihojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya kuitikia wito wa kamati hiyo, Bungeni mjini Dodoma leo, kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na Matamshi aliyoyatoa mapema mwaka huu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha yaliyokuwa na madai ya kuidharau Bunge. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Mkuu wa Wilaya Arumeru Alexander Mnyeti ameitwa na Bunge kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kulidhalilisha Bunge. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema hayo leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni. Amesema Mnyeti ameitwa leo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, kinga na madaraka ya Bunge.

DC DANIEL CHONGOLO AONGOZA OPARESHENI YA KUTEKETEZA MASHAMBA YA BHANGI EKARI 5 WILAYANI LONGIDO

Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Longido ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Godfrey Daniel Chongolo imeendelea na oparesheni ya kuteketeza madawa ya kulevya katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.

Sehemu ya Bhangi ikichomwa moto,kuhakikisha haichuliwi tena kwa matumizi mengine ya ulevi.

Mkuu wa wilaya ya Longido, Godfrey Daniel Chongolo akijiandaa kuanza kuongoza oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya Bhangi akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya pamoja na DC wa wilaya ya Longido, Mh Daniel Chongol ( pichani kulia) wakiendelea na oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya bhangi katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo mkoani Arusha

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AZINDUA ZOEZI LA UTHAMINI

 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Ezekiel Odunga akizungumza na wananchi wa kata ya Farkwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la uthamini mali ili kupisha ujenzi wa bwawa la Farkwa.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma akiongozana na baadhi wa Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Wataalamu wa Halmashauri, Wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Uvuvi na umwaguliaji, Wataalamu wa Bonde la Kati na Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wamezindua zoezi la uthamini wa mali za wananchi wa vijiji viwili vya Mombose na Bubutole watakaohama kupisha mradi mkubwa wa Ujenzi wa bwawa la Farkwa mkoani hapa.

Mradi wa bwawa la Farkwa ni mradi mkubwa ambao huenda ukawa ni mkubwa katika Ujenzi wa mabwawa makubwa kuliko yote barani Afrika. Mradi huu uliasisiwa na baba wa Taifa tangu mwaka 1970 utazinufaisha Wilaya za Bahi, Chemba, Chamwino na Dodoma Manispaa na utegemea kutumia pesa za Tanzania zaidi ya Tilioni 2.

Kufuatia umuhimu wa mradi huu na uwijio wa makao makuu ya nchi mkoani Dodoma, serikali imezamilia ifikapo mei mwaka huu zoezi la Uthamini wa mali za wananchi wanaohama kupisha mradi huu mkubwa katika Vijijini vya Mombose na Bubutole vilivyopo Wilayani Chemba pamoja na vijiji vinavyopitiwa na njia Kuu ya bomba linalopeleka Maji eneo la Kilimani mjini Dodoma liwe limekamilika tayari kwa kuwalipa wananchi ili Ujenzi wa bwawa uanze.

Ujenzi wa mradi huu unategemea kuchukua miaka mitatu 2017-2021 mpaka kukamilika kwake. Hivyo wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Wataalamu wa uthamini kwa kuwa wameusubiri mradi huu kwa zaidi ya miaka 47 na leo serikali imepata fedha ya kuutekeleza.

Mhe Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Odunga wamewataka wananchi hao kujiepusha na watu wasiopenda maendeleo yao na nchi yetu kwa ujumla wa anaopita pita huko na kujifanya watetezi wa haki za wananchi. Swali hao watetezi walikuwa wapi tangu 1970 waje leo ambapo mradi unaanza kutekelezwa.? 

Aidha, amesisitiza wananchi ambao ni wamiliki halali wa maeneo husika ndio wajitokeze kwenye uthamini huo ili kuepusha udanganyifu na migogoro isiyo ya lazima wakati wa malipo yatakopoanza. Kwani kuna baadhi ya wananchi zi waaminifu na atakayefanya hivyo akibaini sheria kali dhidi yake zitachukua mkondo.

Kwa upande wa Wataalamu Mkuu huyo wa Wilaya amewataka kutumia akili, uweledi na taaluma zao katika kuhakikisha kila mwananchi wa maeneo hayo anapata haki yake stahiki kwa mujibu wa sheria za uthamini.

Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Mhe Rajabu Muheshimwa ameongea kwa kupongeza juhudi za Serikali kwa kuamua kuanza mradi huu na zaidi kusihi wananchi kutoa ushirikiano kwa Wataalamu, hali kadhalika Mhe Diwani wa Kata ya Farkwa Ndugu, Suleiman Gawa amesisitiza kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu pia Wataalamu wahakikishe wanaorodhesha mali zote za wananchi zinazotambulika kisheria ili kuepusha migongano hapo baadae.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya amewataka Viongozi wa Vijiji na vitongoji kusimamia zoezi hili kikamilifu kwani wao ndio wanaowafahamu wananchi wao pia watoto ambao wanamiliki mali lakini hawatambuliwi kisheria kutokana na umri wao.

DC: Tutashughulika na machangudoa

MKUU wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ali Hapi, ametoa onyo kwa wamiliki wa baa wanaowahifadhi watu wanaojihusisha na biashara ya ngono ‘Machangudoa’ kuwa watafutiwa leseni.
Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya Kijitonyama waliodai kuwa kuna baadhi ya baa zimekuwa zikiwahifadhi wanaouza miili, hali ambayo ni hatari kwa mazingira na makuzi ya watoto.
Hapi amesema haiwezekani serikali iwe inapambana na biashara hiyo haramu lakini kuna baadhi ya baa zinawafuga machangudoa.
"Tutashughulika na changudoa na tutashughulika na wenye baa zinazowahifadhi machangudoa, kwa sababu hili ni suala lililo kinyume cha sheria, serikali inapambana na hili tatizo halafu mwingine analikumbatia, hilo haliwezekani, tutawachukulia hatua za kisheria," amesema.
Awali, akitoa malalamiko yake kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, mkazi wa Kijitonyama alidai kuna baa zilizogeuka kero kwao.
Ameitaja baa iitwayo Kona ya Sinza imekuwa ikiwahifadhi machangudoa hivyo kuhatarisha makuzi ya watoto kwa kuwa wanaweza kuiga tabia zisizofaa.
"Hii baa iko hapo Afrika Sana, machangudoa wako pale wanajiuza hadharani, sasa kwa kweli hii ni kero kubwa kwetu, watoto wanaweza kuiga na matokeo yake tutakuwa na kizazi kibaya ," amesema mwananchi huyo.

DC Hapi aagiza Corner Bar ifungwe baada ya kudaiwa kukiuka maadili

Baada ya malalamiko kuzidi kutokana na kuwapo biashara zisizo rasmi katika baa maarufu ya Corner, sasa baa hiyo imeamriwa kufungwa.
Akiwa katika ziara ya kawaida leo (Jumamosi) mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Ofisa Biashara wa Kinondoni, Mohamed Nyasama kuifunga baa hiyo.
“Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi vikaendelea kufanyika huku tukiwa kimya…natoa agizo kesho.nendeni kaifungieni hiyo baa kwa kuwa inakiuka maadili,”amesema Hapi.

Hata hivyo Nyasama amesema walishaitoza baa hiyo faini ya Sh 300,000 kwa kosa hilo.
“Mkuu hii baa ni sugu, nimewahi hata kuipiga faini na bado imeendelea na utaratibu huo huo wa kuruhusu kina dada kujiuza.Kwa amri yako mkuu naanza taratibu za kuifungia leo, hadi kufikia kesho itakuwa tayari,” amesema.

Source: Mwananchi

DC SHINYANGA AONGOZA WANANCHI KUFANYA MAZOEZI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Februari 18,2017 amewaongoza wakazi wa Shinyanga kufanya mazoezi katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga. 


Mazoezi hayo yaliyoanza saa 12 asubuhi na kumalizika saa 2 asubuhi yamehudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Stephen Masele na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro. 
Akizungumza wakati wa mazoezi hayo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amesema wakazi wa Shinyanga wataendelea kufanya mazoezi kila siku Jumamosi ili kumuunga mkono Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan . 
“Wiki iliyopita mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alizindua mazoezi kimkoa,tumekubalina tuwe tunafanya mazoezi kila wiki siku ya Jumamosi ili kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza,nawakumbusha kuwa mazoezi ni afya hivyo wananchi naombeni muendelee kujitokeza kufanya mazoezi”,alisema Matiro. 
Hivi karibuni Makamu wa rais Samia Suluhu aliagiza amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja.
Alisema kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi ambapo aliwaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini.
Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 33 wakati wa mazoez hayo..Tazama hapa chini
Mratibu wa Mazoezi hayo,Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ili azungumze na washiriki wa mazoezi hayo katika viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa mazoezi leo katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na washiriki wa mazoezi hayo
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akitoa neno kwa washiriki wa mazoezi hayo ambapo alisema mazoezi ni afya na yanajenga upendo na kufahamiana kwa washiriki wa mazoezi
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Stephen Masele akizungumza na washiriki wa mazoezi hayo ambapo aliwahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kufanya mazoezi 
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Stephen Masele akizungumza uwanjani


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifanya mazoezi
Mazoezi yanaendelea
Wananchi wakifanya mazoezi
Mazoezi yanaendelea
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Stephen Masele(wa pili kulia) akifanya mazoezi
Mazoezi yanaendelea
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro(wa kwanza kulia) akifanya mazoezi
Mazoezi yanaendelea
Washiriki wa mazoezi wakisalimiana baada ya mazoezi
Picha ya pamoja ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na baadhi ya washiriki wa mazoezi hayo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog