Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB Dk Aloyce Nzuki wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania walioipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masuala ya Utalii
wakiwa wameshika vyeti vyao,kutoka kushoto ni Wilfred Moshi, Respicius
Baitwa wa pili kutoka kulia na Juma K. Nugaz aka Antonio Nugaz wa tatu
kutoka kushoto wengine ni Geofrey Meena Meneja Masoko wa TTB na Devotha
Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa pili kutoka kushoto.
Bodi
ya Utalii Tanzania TTB leo imetoa vyeti kwa watanzania watatu
walioipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masuala ya Utalii.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Dk Aloyce Nzuki Akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa tukio la kuwatunikia vyeti watanzania
watatu walioipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masuala ya Utalii,amesema
watanzania hao waliweza kupeperusha bendera ya Tanzania vizuri hasa
katika masuala ya utalii, kwa hapa Tanzania na nchi za nje.
Watanzania
hawa wameweza kufanya mambo makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa sana
yamechangia kwenye sekta ya utalii.Watanzania ambao wamepata tuzo hizo
leo ni pamoja na
- Respicias H. Baitwa
- Wilfred Moshi
- Juma K. Nugaz
1.
Respicius BaitwaNi mtanzania wa kwanza ambaye ameweka rekodi ya Afrika
kwa mwafrika wa kwanza anatarajia kupanda vilele saba virefu katika
mabara yalioko duniani.
Bw.
Baitwa mpaka sasa ameshapanda vilele 4. Ameshapanda kilele cha kwanza
Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 100, amepanda Elbrus kilele kirefu
katika nchi za ulaya, Aconcagua, Argentina na Kosciusko Australia
2. Wilfred Moshi
Wilfred
Moshi amekuwa mtanzania wa kwanza kupanda kilele kirefu kuliko vyote
duniani kilele cha mlima Everest. Wilifred Mosha alipanda mlima Everest
mwezi may 2012 na amekua mwafrika wa 3 kupanda na kufika kilele cha
mlima Everest, na kupandisha bendera ya Tanzania kwa kufanya hivyo
Wilifred Mosha ameweza kutangaza jina la Tanzania na kwenye mahojiano
mbalimbali na vyombo vya habari duniani ameweza kutangaza vivutio vya
utalii wa Tanzania kwa ujumla wake.
3. Juma K. Nugaz (Antonio Nugaz)
Juma
Nugaz mtayarishaji wa kipindi cha utalii cha Kambi Popote kinachorushwa
na clouds TV amekuwa mtangazaji bora katika kuhakikisha utalii wa ndani
kwa mwaka 2012 tuzo iliytolewa na chama cha waandishi wa habari
Tanzania.
Mr.
Juma Nugaz amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utalii wa ndani
kupitia kipindi cha kambi popote na amekuwa akitembelea bila kuchoka
vivutio vya utalii na mwaka jana mwezi wa Disemba aliweza kurekodi
kipindi maalum wakati wa zoezi la kupanda mlima kwa baadhi ya watanzania
katika sherehe za kuazimisha miaka hamsimi (50) wa Tanzania bara ya
Uhuru.Tunampongeza sana.
Bodi ya utalii Tanzania inawapongeza watanzania hawa kwa kufanya juhudi
kubwa ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii wa Tanzania na tutaendea
kushirikiana nao kutangaza vivutio vyetu zaidi.
Pamoja
na kuwazawadia cheti hiki vilevile tunawazawadia safari ya kitalii
kwenda mbuga za wanyama za Selous kwa siku nne na familia zao.



No comments:
Post a Comment