HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » BREAKING NEWS: RC NJOMBE AIBIWA USIKU WA SENSA

Mkuu wa Njombe Aser Msangi

Watu wasiofahamika wameingia nyumbani kwa mkuu wa mkoa wa
Njombe [RC] Kaptain Mstaafu Asseri Msangi usiku wa kuamkia
agosti 26 siku ya sensa ya watu na makazi inayofanyika nchini kote
na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
moja.

Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com nyumbani kwake leo asubuhi Kaptaini Msangi alisema tukio hilo lilitokea usiku wa manane wakati
amelala, na alivitaja vitu vilivyoibiwa kuwa ni pamoja na kidadavuo
mpakato [laptop] yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu pamoja
na simu tatu za vijana wake zenye thamani ya shilingi ya laki nne na
nusu.

Hata hivyo Kaptaini Msangi alisema tukio hilo limemsikitisha sana
hasa ikizingatiwa kwamba nyumba yake inalindwa na askari wa jeshi
la polisi wenye bunduki zenye risasi za kutosha.
"Nimeishi miaka mingi kwenye nyumba bila ulinzi wowote nilipo
kuwa mkuu wa wilaya [DC] sijawahi kuibiwa lakini leo hii mkuu wa
mkoa nina walinzi lakini nimeibiwa, mpaka hapa naona haina haja ya
kuwa na walinzi"alisema Msangi.

Aidha Msangi alisema anawatilia shaka askari polisi waliokuwa zamu
huku kuwa wanahusika na tukio hilo.
Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa wakati mwingine walinzi hao
huwa wanatoroka lindo na kwenda kunywa pombe.
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia
askari wawili wa jeshi hilo waliokuwa lindo kwa mkuu wa mkoa
usiku huo wa tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Akizungumza na gazeti hili kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Njombe Fulgency Ngonyani aliwataja askari hao kuwa ni pamoja na
askari mwenye namba G. 5414 PC Ombeni na askari mwenye
namba G. 5455 PC Mohamed ambao wakati tukio hilo likitokea ndio
waliokuwa zamu ya kulinda kwa mkuu huyo wa mkoa.

"Tunawashikilia askari hawa kwa kuwa ndio walikuwa lindo, lakini
hata hivyo tumefanya uchunguzi wa awali hatujaona sehemu yoyote
iliyobomolewa yawezekana watu walifanya tukio hilo la wizi
walitumia funguo bandia" alisema Kamanda Ngonyani.

Akizungumzia hataua ya askari wa jeshi hilo kuwa na tabia ya
kuacha lindo na kwenda kunywa pombe, Kamanda Ngonyani alisema
hana taarifa hizo lakini aliahidi kulifanyia kazi, ambapo amemwagiza
mkuu wa upepelelezi kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo.


CHANZO: http://francisgodwin.blogspot.com

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: