Katikati ni Mkurugenzi
mtendaji wa bank ABC Boniphace Nyoni na kushoto kwake ni Mkurugenzi mkuu wa
kitengo cha fedha Mwalim Zuberi na kulia kwake ni kocha wa Timu ya Jamhuri Ameri
Chuwa.
Kocha wa timu ya Mtibwa Sugar Mecky wakati akiongea
na waandishi wa habari.
Nusu fainali zitapigwa Uwanja wa Taifa kesho Jumatano, ambako Simbaa itavaana na Azam huku Mtibwa sugar ikipepetana na Jamhuri. Mchezo wa kwanza utaanza saa nane mchana wataanza Mtibwa sugar na Jamhuri ya Zanzibar na mchezo wa pili ni kati ya Simba Vs Azam utakao anza saa kumi.
MTIBWA, Simba, Azam FC na Jamhuri ya Pemba zimefanikiwa kupenya hatua ya nusu fainali ya michuano ya BancABC SUP8R inayondelea katika vituo vinne hapa nchini.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Banc ABC, ilikuwa
ikirindima katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar na sasa
imefikia hatua ya nusu fainali.
August 12 mwaka huu kwenye dimba la Chamazi, Mbagala
jijini Dar es Salaam, ilishuhudiwa kwa mara ya pili nyuki wakikatiza uwanjani
hapo, Jamhuri iliichapa Mtende kwa mabao 4-0.
Mabao ya washindi yalifungwa na Sadik Rajab dakika
ya 28 na 45, Selemani Nuhu dakika ya 82 huku Suleiman Ally akikandamiza la nne
dakika ya 90.
Kwenye dimba la Kirumba Mwanza, makinda wa Simba
waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zimamoto yote yakitiwa kimiani na
Edward Christopher, wakati huko Moshi kwenye Uwanja wa Ushirika, Azam FC
iliifunga Polisi Morogoro kwa mabao 2-1.
Bingwa katika michuano hiyo atajitwalia kombe na
kitita cha sh milioni 40, wa pili milioni 20 huku timu zitakazoishia nusu
fainali kila moja itapata sh mil 15 na zitakazosalia zitajipoza kwa sh milioni 5
kila moja.

No comments:
Post a Comment