Katikati
ni Rashid Matumla akipima uzito wake (kilo 76) mbele ya waandishi wa
habari (hawapo pichani). Kushoto ni promota wa pambano hilo, Siraji
Kaike na kulia ni daktari, Michael Abraham na Maneno Oswald.
Katikati ni bondia Maneno Oswald akipanda kwenye mizani kupima uzito wake (kilo 56)
Kushoto ni Maneno Oswald, promota wa pambano hilo, Kaike Siraji na Rashid Matumla wakiwa katika picha ya pamoja hotelini hapo.
Mabondia wa kitambo Bongo, Rashid
Matumla na Maneno Oswarld, leo walikuwa katika Hoteli ya The Atriums kwa
ajili ya kupima uzito kujiandaa kwa pambano kali litakalochezwa siku ya
Iddi Mosi katika Ukumbi wa Dar Live jijini, Dar.
Akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari, promota wa pambano hilo, Kaike Silaji, kila bondia yupo katika afya nzuri na wapo tayari kwa ajili ya pambano hilo siku ya Idd Mosi.
“Niwahakikishie wapenzi wa mchezo wa ngumi kufika kwa wingi siku hiyo kwani mabondia wetu wamejipanga vilivyo kuhakikisha kila mmoja anajiwekea heshima ya kuwa mshindi. “Kutakuwepo na mapambano ya utangulizi ya vijana matata katika mchezo wa Boxa kabla ya Maneno na Matumla hawajapanda ulingoni,” alisema Kaike.

STORI/PICHA: ERICK EVARIST & GEORGE KAYALA/ GPL.

No comments:
Post a Comment