Askari
wa jeshi la polisi pamoja na askari wa Tanapa wahifadhi ya Katavi
wakiwa na mtuhumiwa Jonathani Laftari (mwenye tishet nyekundu) Mkazi wa
Kijiji cha Uluila Wilaya Mlele Mkoa wa Katavi walie mkamata na bunduki
ya kivita aina ya SMG yenye namba M22-13350 pamoja na risasi 37 ndani ya
hifadhi ya mbuga ya katavi.
Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Jonathani Charles Naftari (26)
mkazi wa kijiji cha Uruila baada ya kukamatwa na bunduki ya kivita na
risasi 37 ndani ya hifadhi ya Katavi.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa
habari kuwa mtuhumiwa alikamatwa hapo jana majira ya saa 8:00 mchana
katika eneo la Kalumbi ndani ya hifadhi ya Katavi akiwa na Bunduki
Sub-Machine Gun (SMG)yenye namba M22 – 13350 pamoja na risasi 37 zikiwa
ndani ya magazine yake na risasi nyingine saba zilikuwa ndani ya mfuko
wa serikali.
Mtuhumiwa
alikamatwa siku hiyo kufuatia msako mkali ambao ulifanywa na askari wa
jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya
kataviKidavashari alieleza kuwa mtuhumwa ambaye alikuwa na wenzake
watatu walipozungukwa na askari wa polisi na Tanapa na kutakiwa
kujisalimisha walikataa kutii amri hiyo na ndipo walipoanza kuwafyatulia
askari risasi hovyo kuwalenga askari
Ndipo
askari walipojibu mapigo ya risasi na hatimaye majangiri hao walianza
kutimua mbio na askari kwa ustadi mkubwa walifanikiwa kumkamata
Jonathani na silaha hiyo ya kivita.Baada ya mtuhumiwa kukamatwa
alipekuliwa na kukutwa na risasi saba ndani ya mfuko wa saluari pamoja
ana panga na kisu ambacho kilikuwa na damu.
Kamanda
Kidavashari alisema mtuhumiwa alipofikishwa katika kituo cha polisi
alidai kuwa silaha hiyo ilikuwa ni mali yake na yeye na wenzake
waliingia ndani ya hifadhi kwa lengo la kuwinda wanyama.Kidavashari
alieleza polisi kwa kushirikiana na Askari wa Tanapa wanaendelea na
msako kuwatafuta watuhumiwa watatu waliotoroka kwenye tukio hilo.
Pindi upelelezi wa tukio hili utakapokamiliaka mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabiri



No comments:
Post a Comment