Kwa
takribani miezi 9 sasa tangu nimeungana na wenzangu waishio Kigamboni
nimejikuta katika wakati mgumu hususan, wakati natumia Kivuko jambo
lililonipa msukumo wa kukaa chini na kuandika mada hii. Kwa mtazamo
wangu, nadhani hakuna mawasiliano kati ya Afisa wa Mamlaka ya Bandari
(TPA) anayeongoza Meli zinazoingia na kutoka Bandarini na Afisa wa
TEMESA (Mamlaka yenye dhamana na Vivuko) anayehusika kuruhusu vivuko.
Inawezekana
nisiwe sahihi, lakini nataka kutahadharisha kuwa haya ni mawazo yangu
binafsi. Katika kipindi chote ambacho nimeanza kujihusisha na shughuli
za kuhamia Kigamboni nimekutana na kero ambazo nilidhani katika hali ya
kawaida kuna Afisa anapaswa kusimamia pale Kivukoni. Cha kushangaza ni
kuwa sioni na sidhani kama wenzetu wameona hili. Pamoja na hilo naomba
kueleza mambo yafuatayo:-
1. MUDA WA KUINGIZA NA KUTOA MELI BANDARINI:
Ndugu
zangu ni jambo la kushangaza mno kukuta eti wakati wananchi ama
wanawahi kazini asubuhi au wanarudi majumbani jioni baada ya pirika za
ujenzi wa Taifa ndipo Afisa Muoongoza Meli anapojaribu kuruhusu Meli
kubwa kutumia njia. AJABU KWELI! Kwa wale wasiojua, Meli hizi ni kudwa
mno na hulazimika kupita taratibu sana kuepusha misukosuko au tafrani
kwenye Vivuko kwani vinaweza kuanguka. Wachache wenu ambao wamewahi
kukutana na dhoruba za namna hii wakati Boat za kwenda Zanzibar
zinapopita watakuwa ni mashahidi wazuri.
Boti ya TPA Ikizuia Pantone ili meli iweze kupita huku Panton imepatia abiria. Hivi hapo ikitokea itirafu kwenye Panton nani hatakayewajibika kwa usimamizi huu unaoonekana hapo kwenye picha.
![]() |
Meli inapita huku abiria wa Pantoni wamesubiri karibu saa nzima, tujifunze kwa mengi kwani hapa ni hatari sana kwa abilia wa Panton. |
![]() |
Pata picha ya Idadi ya watu waliozuiliwa na meli: Wakitoka kwenye Pantoni.Kiukweli tuweke utaratibu wa mawasiliano katika Panton kabla ya kuondoka kwani tunaweka maisha ya watu rehani |
1. MATUMIZI YA VYOO:
TEMESA
wamekuwa busy na kukusanya pesa lakini cha ajabu utaratibu wa vyoo ni
mbovu kupindukia. Fikiria wale wanaotumia magari madogo kwa mfano; Kila
siku wanalipia Tsh. 3,000/= lakini mtu huyo akihitaji kujisaidia lazima
akalipe Tsh. 200/= tena inakuwa kama ni adhabu hadi kupata mahali ambapo
kuna vyoo ambavyo vinanuka kwa kukithiri na uchafu. HAIINGI AKILINI
HATA KIDOGO.
2. PARKING YA MABASI/DALADALA:
Utaratibu
ni mbovi, abiria na magari yanatuamia njia moja halafu mlangoni mnakuta
daladala zinasubiri abiria, sasa subiri uone kasheshe yake!
USHAURI WANGU KWA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA:
1. Mamlaka
zinazohusika kuandaa utaratibu ambao utazuia Meli kubwa kupita wakati
watu wanawahi au wanatoka vibaruani kwa wingi. Meli hizi hutumia zaidi
ya saa 1 kupita hali ambayo husababisha usumbufu mkuwa kwa wananchi.
2. Uandaliwe
utaratibu wa kusafisha vyoo, kujenga vyoo ambavyo ni rafiki kwa abiria
wa miguu na wanaotumia magari binafsi. Aidha, uwezekano wa wanaolipa
gharama za magari kutumia vyoo bure uangaliwe upya. Hawa watu wanalipa
pesa nyingi wakati huduma ni duni.
3. Vile
vile mamlaka husika isimamie na kutenganisha abiria na magari kutumia
lango moja la kutokea kuepuka na usumbufu na hatari zinazoweza
kujitokeza. Hali huwa mbaya sana wakati wa kutoka haswa upande huu wa
Dar es Salaam.
MWISHO:
Naamini
ushauri wangu utasaidia Mamlaka zinazohusika kuboresha hali hii.
Watanzania na wateja wenu haturidhishwi, wapo wengi wanapenda kuyasema
haya lakini naamini wanabanwa na muda wa kuweza kuandika kama ambavyo
nimejaribu hapa.
Imetolewa na:
Elias Pasco Mahwago Kayandabila
No comments:
Post a Comment