Wananchi wa manispaa ya Iringa wakishuhudia ajali hiyo ya michezo ya pikipiki
Huku
kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda akiwaonya
madereva kuzingatia sheria za usalama barabara kwa siku hii ya leo
wakati wa sikukuu ya Id El Fitri ,hali imekuwa tofauti katika
manispaa ya Iringa baada ya kijana mmoja aliyekuwa katika maonyesho ya
pikipiki kupata ajali eneo la stendi kuu ya mkoa wa Iringa.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 8 mchana baada ya kijana huyo mwendesha pikipiki kushindwa kuimudu pikipiki yake hiyo na kumponyoka na kwenda kuwagonga watu wawili waliokuwa wakipata kinywaji katika duka moja eneo hilo la stendi kuu.

Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema kuwa, kijana huyo ambaye alikuwa katika
msafara wa waendesha piki piki zaidi ya watatu ambao walikuwa
wakizunguka mitaani na kuonyesha vionjo kwa wananchi kabla ya kwenda
uwanja wa Samora ambako walipanga kufanya onyesho hilo alijikuta
akitupwa chini na piki piki hiyo baada ya kutaka kusimama juu ya
stelingi ya pikipiki hiyo huku ikiwa katika mwendo mkali.
Hata hivyo katika ajali hiyo kijana huyo ambaye jina lake bado kufahamika amejeruhiwa pamoja na watu wengine wawili waliokuwa wakishuhudia mchezo huo .
Hata hivyo katika ajali hiyo kijana huyo ambaye jina lake bado kufahamika amejeruhiwa pamoja na watu wengine wawili waliokuwa wakishuhudia mchezo huo .
Picha kwa hisani ya http://francisgodwin.blogspot.com

No comments:
Post a Comment