Taarifa Kwa Umma


                      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                    WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

                          TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa Bodi mbali mbali zilozoko chini ya Wizara. Kuanzia sasa Wajumbe wa Bodi hizo watapatikana kwa njia ya ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.
Kwa sasa kuna Bodi nane (8) ambazo muda wake umeisha au unakaribia kuisha.Bodi hizo ni za za Taasisis/Mashirika yafuatayo;-
I. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
II. Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
III. Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
IV. Makumbusho ya Taifa
V. Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA)
VI. Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi
VII. Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
VIII. Bodi ya Leseni za Utalii (TTLB)
Watanzania wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Bodi hizo wanatakiwa kupeleka maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Maelezo zaidi ya namna ya kupeka maombi yataweka kwenye magazeti na tovuti ya Wizara, www.mnrt.go.tz 

BOFYA HAPA KWA MAELEZO ZAIDI

No comments

Powered by Blogger.