SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
WIZARA YA HABARI UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO
Tel: 0255 24 2237325/0255 24 223 7313 Idara ya Habari Maelezo Fax: 0255 24 2237314 P.O. Box 2754
Zanzibar E-mail: habarimaelezo@yahoo.co.uk, maelezozanzibar@zanlink.com, maelezozanzibar@hotmail.com, maelezozanzibar@gmail.com
09/08/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Idara
ya Habari (MAELEZO) tunawakumbusha tena waandishi wa habari juu ya
ulazima wa kuwa na kitambulisho cha kufanyia kazi ya uandishi wa habari
Zanzibar kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo(Press Card) kwa mujibu
wa sheria Zanzibar.
Aidha,
waandishi wa habari kutoka nje ya Zanzibar hawataruhusiwa kufanyakazi
ya uandishi wa habari mpaka pale amepata ruhusa ya Idara ya Habari
Maelezo kwa mujibu wa sheria ya usajili magazeti N0 5 ya mwaka 1988 ya
Zanzibar.
Kutokana
na hali ilivyojitokeza hivi sasa duniani, tunashauri vyanzo vya habari
ikiwemo viongozi wa Serikali wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri, Naibu
Waziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wasemaji
katika Taasisi mbalimbali kutotoa taarifa zozote kwa vyombo vya habari
kwa mwandishi ambaye hana Press Card iliyotolewa na Idara ya Habari
Maelezo Zanzibar.
Hivyo,
kuanzia tarehe 1/09/2012 waandishi wa habari wote wakiwa kazini ni
muhimu kuonyesha kitambulisho kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo.
Aidha,,
tunasisitiza kwamba kwa mujibu wa sheria ya usajili wa magazeti sheria
N0 5 ya mwaka 1988,kifungu cha 13 kinasisitiza kwamba mtu yeyote
atakayechapisha Kitabu, Magazeti, Vipeperushi, Vijarida,Ramani na Chati
lazima awasilishe nakala tatu si zaidi ya siku 14 baada ya kuchapishwa
kwa Mrajis Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Kutofanya
hivyo ni kwenda kinyume cha sheria ya Usajili Magazeti na Vitabu N0 5
ya mwaka 1988 hatua za kisheria zitachukuwa kwa atakayekiuka.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI (MAELEZO) ZANZIBAR
09/08/2012




No comments:
Post a Comment