TASWIRA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

 Waziri wa Fedha , Dkt. William Mgimwa, akiingia katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo tayari kwa maandalizi ya kusoma hotuba  ya wizara  yake ya Mapato na Matumizi  ya Fedha  ya mwaka wa fedha 2012/2013.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati aliyevaa suti nyeusi)akizungumza na baadhi ya Masheikh 69  wa  Jimbo la Iramba Magharibi wakati akizungumza nao kuhusu  zoezi la Sensa na akiwasisitiza juu ya kuwaelimisha waumini  wao juu ya umuhimu wa sensa kwa maendeleo ya taifa . Masheikh   hao walihudhuria kikao cha Bunge leo,  mjini Dodoma kwa mwaliko wa Mbunge wao, Mwigulu Mchemba.
 Mbunge wa Viti Maalum CCM, Martha Mlata, akizungumza na baadhi ya Masheikh 69  wa  Jimbo la Iramba Magharibi, waliohudhuria kikao cha Bunge mjini Dodoma leo kwa mwaliko wa Mbunge wao Mwigulu Mchemba. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati aliyevaa suti nyeusi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Masheikh 69  wa  Jimbo la Iramba Magharibi . Masheikh   hao wamehudhuria kikao cha Bunge leo,  mjini Dodoma kwa mwaliko wa Mbunge wao, Mwigulu Mchemba. Picha Zote na Magreth Kinabo -MAELEZO

No comments

Powered by Blogger.