Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika matembezi ya hisani ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania,
yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Matembezi hayo yalianzia
katika Viwanja vya Karimjee jijini na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders
Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Moahammed Gharib Bilal,akimkabidhi cheti, Mhandisi Grace Beo, kutoka Kampuni ya
Temesa ICT Engineer, akiwa ni mmoja kati ya waliochangia na kushiriki vyema
katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa
Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Makamu alikabidhi
vyeti hivyo baada ya kuhitimisha rasmi matembezi hayo ya hisani yaliyoanzia
katika Viwanja vya Karimjee na kumalizikia kwenye Viwanja vya Leaders Club
Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja
ya kumbukumbu na Wahandisi (Local Engineers) baada ya kuhitimisha matembezi
hayo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Daar es Salaam leo,
Oktoba 7, 2012.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR






No comments:
Post a Comment