![]() |
| Frederick Sumaye |
* Asema hayupo CCM kwa ajili ya madalaka
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Ikiwa ni siku mbili baada ya
gazeti la Mwananchi kuandika katika ukurasa wa kwanza habari iliyoambana
na picha ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Mwenyekiti wa
Chadema Freeman Mbowe, 'likiuza' kwamba Sumaye ateta na Chadema kuhusu
hatima yake kisiasa, leo Waziri Mkuu huyo mstaafu amesema hawezi kuhama
CCM.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema, ndoto za wanaodhani kwamba
atahama CCM kwenda chama kingine, ni sawa na fisi anayevizia mkono wa
mtu akidhani utakatika lakini asiambulie kitu.
"Napenda kueleza wazi kwamba,
sina nia wala ndoto ya kuhama CCM kwenda Chama chochote, mimi sipo CCM
kwa sababu ya cheo", alisema Sumaye.
Akizungumzia kushindwa kwake ujumbe wa NEC katika uchaguzi wa Hanang, Sumaye amedai rushwa imesababisha kuanguka kwake.
Katika uchaguzi huo, ambao ni
miongozi mwa chaguzi za CCM zinazoendelea nchini kote katika nafasi
mbalimbali, Mary Nagu aliibuka mshindi.




No comments:
Post a Comment