Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Job Masima akizungumza
na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima Ofisini kwake
leo alipomtembelea na wajumbe kutoka JWTZ Makao Makuu waliofika Mkoani
Rukwa kwa ajili ya kujionea shughuli zinazoendelea kufanywa na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo ni kuzoa shehena ya mahindi kutoka
Mkoani Rukwa kwenda Mkoa jirani wa Katavi ambapo yatasafirishwa kwa reli
kwenda Mikoa ya Kaskazini. Jumla ya tani 20,000 zinategemewa
kusafirishwa na jeshi hilo ambapo mpaka sasa zimeshazolewa tani 11,000.
Mahindi hayo yamenunuliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Chakula.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza na ugeni
huo Ofisini kwake. Akizungumza katika kikao hicho Alhaj Chima
alilishukuru jeshi hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya kwani mpaka sasa
hakuna malalamiko yeyote yaliyojitokeza.
Baadhi
ya maofisa wa jeshi hilo waliongozana na Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi
Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Rukwa Samson Mashalla.






No comments:
Post a Comment