KONGAMANO LA WANAWAKE KUHUSU KATIBA MPYA

WANAWAKE kutoka mikoa yote nchini  wamepata fursa ya kushiriki Kongamano la kwanza la Kitaifa la wanawake kujadili masuala muhimu ya haki za wanwake wanazotaka ziingie kwenye Katiba mpya.

Kongamano hilo liloandaliwa na Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), linafanyika kwa siku tatu kuanzia  22-24 Oktoba 2012 jijini Dar es salaam, ambap[o watajadili kwa kina na kuchambua mapungufu ya katiba inayotumika hivi sasa na kuwekeana maazimio ya  masuala yatakayotakiwa kuingizwa kwenye mahudhui ya Katiba mpya inayotarajiwa kuanza kutumika ifikapo 2014.

Mkurugenzi Mtendaji wa WFT Mary Rusimbi akichangia mada

Washiriki wa Kongamano la masuala ya Haki za Wanawake  na Katiba  Tanzania lililoandaliwa na Mfuko wa wanawake Tanzania (WFT).
Pamoja na mambo mengine,  mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo ni Umuhimu wa katiba katika maendeleo ya wanawake, mapungufu ya Kijinsia Katika Katiba iliyopo, haki za msingi za mwanamke za kuzingatia Katika katiba mpya, masuala muhimu ya kuzingatia katika haki za wanawake na kuwekeana mikakati  ya kutumia vizuri  fursa ya mchakato  wa uuandwaji wa katiba mpya.

No comments

Powered by Blogger.