Askofu
Damian Kyaluzi wa Jimbo katoliki la Sumbawanga akiendesha ibaada ya
mazishi ya kumuombea marehemu Padre Augustino Kanyengere (75) hapo jana
katika Kanisa kuu la Jimbo la Sumbawanga. Padre Kanyengere alifariki
Oktoba 17 mwaka huu katika hospitali la Kristu Mfalme Mjini Sumbawanga
kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu na kuzikwa hapo jana katika
makaburi ya Katandala. Padre
huyo ndiye aliyekuwa padre wa kwanza wa Kanisa hilo kupata Upadre kwa
kutokea seminari ya Kaengesa inayomilikiwa na kanisa katoliki Jimbo la
Sumbawanga iliyoanzishwa mwaka 1956.
(Picha na Walter Mguluchuma - Sumbawanga)



No comments:
Post a Comment