MWANAFUNZI
Agnes Vedasto (17) amezuiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidacho cha nne
Sekondari ya Bukoba, kutokana na kudaiwa kuwa na mimba inayokaribia
miezi tisa
Agnes mwenye namba ya mtihani S.0304/0003 alizuiwa na
Ofisa Elimu Taaluma, Christina Shadrack na Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu,
Wandele Pamba wote wa Manispaa ya Bukoba waliofika shuleni hapo kwa
lengo la kusambaza vifaa.
Inadaiwa kuwa baada ya maofisa elimu hao
kufika shuleni kabla ya wanafunzi kuingia darasani kuanza kufanya
mtihani, waliulizwa na Mkuu wa shule, Deus Gasper kama mwanafunzi huyo
aliyefika jana asubuhi kwa lengo la kufanya mtihani, anaweza kuruhusiwa
kutimiza.
Baada ya kuzuiwa kuingia chumba cha mtihani, mwanafuanzi
huyo alilazimika kurejea nyumbani eneo la Hamugembe, Manispaa ya
Bukoba.
Mkuu wa Sekondari ya Bukoba, Gasper alisema kwa miezi
mitatu mwanafunzi huyo alikuwa haonekani shuleni na uongozi wa shule
ulitambua ni mjamzito, mzazi wake aliitwa na kukiri kuwa mwanae ana
mimba.
Gasper alisema wakati anatambuliwa jina lake tayari
lilikuwa limeshapelekwa Baraza la Mitihani na liliporudi alitaarifiwa na
wanafunzi wenzake , akaamua kufika kwa lengo la kufanya mtihini wa
kuhitimu kidato cha nne akiwa amevaa sare na vifaa vyote vya shule.
Ofisa
Elimu Manispaa ya Bukoba, Simon Mwombeki alisema kwa mujibu wa sheria
ya elimu namba 25, ni kosa mwanafunzi kupata ujauzito akiwa shule, kuoa
wala kuolewa, hivyo mwanafunzi huyo tayari amekosa sifa.
“Mama
yake mzazi (hakumtaja jina) jana alifika ofisini kwangu na kuniomba
mtoto wake aruhusiwe kufanya mtihani, lakini nilishindwa jinsi ya
nimsaidie,” alisema Mwombeki.
Mwombeki alisema kwa mujibu wa
maelezo yaliyotolewa na mama mzazi, mtoto wake anatarajiwa kujifungua
kati ya Oktoba 25 na 26, mwaka huu.
Mapema mwezi uliopita
mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kabirizi, wilayani Muleba, Happiness
Mzalendo (18) alijifungua mtoto wa kiume baada ya kuumwa uchungu akiwa
katika chumba cha mtihani.
Mwanafunzi huyo alilamizika kuomba
msaada kwa msimamizi wa mtihani ambaye alimtoa nje ya chumba na
kujifungulia chini ya mgomba ulioko katika shamba la shule.
CHANZO: MWANANCHI
|
Mwanafunzi Azuiwa Kufanya Mtihani Kutokana na Ujauzito
Tag:



No comments:
Post a Comment