Alisema kamati
hiyo ndogo ya Haki, Kinga, Madaraka ya Bunge ambayo iliongozwa Ngwilizi
ilifanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma hizo na kugundua kuwa hazikuwa
na ushahidi.
Alisema kamati hiyo iliundwa kutokana na michango mbalimbali iliyotolewa na baadhi ya wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Julai 27, hadi 28, mwaka huu bungeni.
Alisema tuhuma hizo pia ziliibuliwa kwa maandishi na Maswi ambaye alimwandikia barua Katibu wa Bunge.
Spika alisema katika barua yake, Maswi alisema baadhi ya wabunge wa iliyokuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini walikuwa wanakwenda ofisini kwake kuomba rushwa ili watetee wizara hiyo inapowalisha taarifa mbalimbali kwenye kamati.
Tuhuma nyingine zilikuwa baadhi ya wabunge wa kamati hiyo kuwa na mgongano wa kimasilahi katika kutekeleza majukumu yao ya kibunge ya kusimamia wizara hiyo kwa vile wanafanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Nyingine zilikuwa baadhi ya wabunge
kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kupokea fedha kutoka katika
kampuni za mafuta kwa lengo la kuzitetea kupinga uamuzi wa Maswi wa
kutoa zabuni ya ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL
na Puma.
Mbali ya Katibu Mkuu huyo kutoa tuhuma hizo, nyingine za kujihusisha na rushwa zilitolewa na wabunge mbalimbali zikielekezwa kwa wabunge wa kamati hiyo.
Makinda alisema kutokana na uzito wa tuhuma hizo aliamua kuunda kamati ya kuchunguza jambo hilo sambamba na kuivunja Kamati ya Nishati na Madini.

Wabunge ambao walituhumiwa na Maswi ni Mbunge
wa Viti Maalumu (CCM), Sarah Msafiri ambaye alidaiwa kumwomba Sh50
milioni ili azigawe kwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini kwa lengo
la kuitetea.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleman Zedi
alituhumiwa na Maswi kutaka awalipe wajumbe wa kamati yake Sh2 milioni
kila mmoja ili awatulize wasiendelee kumshambulia kutokana na utendaji
wake waliokuwa wakiulalamikia.
Pia Katibu Mkuu Maswi aliwatuhumu Wabunge wa
Viti Maalumu (CCM), Munde Tambwe na Sarah Msafiri na Mbunge wa
Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kwamba walimwambia kwamba lazima
aachie nafasi kwa kuwajibika kutokana na utendaji wake usioridhisha.
Wabunge ambao walitoa tuhuma kwa wabunge
wenzao wakati wakichangia na ambao walihojiwa na Kamati ya Ngwilizi ni
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ali Kesi;, John Mnyika
(Ubungo-Chadema), Joseph Selasini (Rombo-Chadema), Kangi Lugola
(Mwibara-CCM) na Mbunge wa Singida Kaskazini (Chadema), Tundu Lissu
ambaye aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuwatuhumu wabunge wa
kamati hiyo kujihusisha na rushwa.
Akitoa uamuzi wake, Spika alisema baada ya
kuhojiwa na Kamati ya Ngwilizi, Maswi alishindwa kutoa ushahidi
kuthibitisha tuhuma zake kwa wabunge hao.
Alisema hata wabunge wote waliotoa tuhuma kwa wabunge wa kamati hiyo, walishindwa kuthibitisha tuhuma hizo huku wengine wakisema habari za kusikia.
Alisema kutokana na hali hiyo anawasafisha wabunge waliotuhumiwa.

Baadaye Spika Makinda alisema pamoja na
kuwasafisha wajumbe hao, ameivunja moja kwa moja Kamati ya Nishati na
Madini na kwamba ataunda mpya katika Bunge lijalo.
Alisema kuwa itakuwa vigumu kwa wabunge hao kuendelea kufanya kazi na watendaji wa wizara hiyo na kwamba wabunge hao amewapangia katika kamati nyingine.
Waliotuhumiwa wanena
Akizungumzia hatua hiyo ya Spika, Zedi aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, alisema anashukuru kuwa ukweli umedhihirika. Alisema ingawa alikuwa akijua kuwa tuhuma hizo zilikuwa za uongo, aliamua kuichia kamati ifanye kazi yake na sasa umma umepata ukweli.
Hata hivyo, alisema hana kinyongo na wabunge wenzake waliomtuhumu kujihusisha na rushwa na kwamba amekubaliana na ushauri wa Spika wa kuwasamehe.

Kwa upande wake, Msafiri alisema anashukuru
kwamba Watanzania wameujua ukweli kuhusu tuhuma alizokuwa amepewa.
Alisema kuwa tuhuma dhidi yake ambazo alikuwa ametuhumiwa na Maswi ni za
uongo.
Hata hivyo, Mnyika kwa upande wake alisema hakubaliani na uamuzi wa Spika kuhusu jambo hilo na kusema kwamba atakata rufaa.
“Sijakubaliana na uamuzi wa leo wa Spika
kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge na hatima ya Kamati ya Nishati
na Madini. Nitakata rufaa. Ripoti yote ya Ngwilizi inapaswa iwekwe
hadharani.”
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment