HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Hoteli yatuhumiwa kuhujumu umeme wa Tanesco

Hoteli ya Lidila ya jijini Dar es Salaam imetuhumiwa kulihujumu Shirika la Umeme (Tanesco) baada ya kubainika kuwa ‘imechakachua’ mita ya LUKU na kuliibia shirika hilo umeme.

Ilielezwa kuwa wakati mita inasomeka 00 kumaanisha kuwa hakuna nishati hiyo hotelini hapo umeme uliendelea kutumika hadi Tanesco ilipobaini hujuma hizo.

Mkaguzi wa Miundombinu wa Tanesco, Christian Simon, aliwaambia wanahabari jana baada ya kubaini kile alichokiita wizi unaofanywa na mteja huyo, kuwa shirika limekata umeme unaoingia hotelini hapo.

Simon alisema licha ya hoteli hiyo kuwa na matumizi makubwa ya umeme wameshangazwa kuona mita ya LUKU ikisomeka 00 huku wakiendelea kutumia nishati hiyo.
Alifafanua kuwa mita ya hoteli hiyo ‘ imechakachuliwa’ kwa kutengenisha nyanya halali zinazopaswa kuingiza umeme ndani yake na taarifa zake kurekodiwa , badala yake wamevuta umeme wa wizi ambao unatumika bila kulipewa.

"Kwa kweli wanatuumiza kwa sababu wanaisababishia Tanesco hasara kubwa kutokana na umeme mwingi wanaotumia bila ya kuulipia,"alisema Simon

Alisema wamechukua vifaa vya umeme ambavyo vilikuwa vinatumika ndani ya hoteli hiyo, ambapo wanakwenda kuvipima na kuwaandikia gharama ya deni wanalotakiwa kulipa tangu walipofanya wizi huo.

"Kwa sasa hoteli hii haiwezi kuwa na umeme, mpaka pale watakapolipa deni lao na watawafungiwa mita nyingine," alisema Simon

Aliongeza kuwa wateja wa wanasababisha hasara kwa taifa kutokana na kutumia umeme mwingi bila ya kulipa huku wateja wa viwango vya chini wamekuwa wakilipa gharama zao.

Wakati huo huo,Ofisa Usalama wa Tanesco, mkoa wa Kinondoni Kaskazini, Shami Dunia amewataka wakazi wa jijini kutoa taarifa za wezi wa umeme ili wachukuliwe hatua.

Dunia alisema wakifanya hivyo watakuwa wamelisaidia shirika kubaini wahujumu wanaoinyima Tanesco mapato kutokana na kutumia nishati hiyo bure.
CHANZO: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: