Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimia baadhi ya wana-CCM,
wakati akiingia kwenye ukumbi wa Kizota, kuendesha Mkutano Mkuu wa CCM
unaomalizika leo
Msinisahau katika Ufalme wenu: Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete akisalimia baadhi ya wana-CCM, wakati akiingia kwenye ukumbi wa
Kizota, kuendesha Mkutano Mkuu wa CCM unaomalizika leo. Kikwete
anapigiwa kura leo ili kuweza kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.
Msanii Vicky Kamata akiimba wimbo maalum kunogesha Mkutano Mkuu wa CCM katika ukumbi wa Kizota, Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu, wakishiriki kucheza
wimbo maalum ulimbwa na Vicky Kamata kabla ya kuanza mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu, wakishiriki kucheza
wimbo maalum ulimbwa na Vicky Kamata kabla ya kuanza mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal
(kulia), Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya na Rais Mstaafu wa Zanzibar,
Dk. Salim Ahmed Salim, wakifuatilia matukio kwenye mkutano huo,
ukumbini.
Wake wa viongozi ,Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Fatma
Karume, Mama Kawawa, Shadya Karume, Mwanamwema Shein na Tunu Pinda
wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe na waalikwa wakimiminika kuingia kwenye viwanja vya Kizota, Dodoma wakati wa mkutano mkuu leo
BIASHARA: Wajumbe na waalikwa wakinunua bidhaa zinazouzwa na
wajasiriamali nje ya ukumbi wa Kizota, Dodoma wakati wa mkutano huo.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Janeth Mbene akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Lina nje ya ukumbi wa Kizota.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Janeth Mbene akizungumza na Kamanda Asas wa UVCCM, mkoa wa Iringa, nje ya ukumbi wa Kizota.
Kamanda Asas wa UVCCM mkoa wa Iringa akitazama nakala ya UHURU
alipotembelea banda la kampuni ya Uhuru Publications Ltd,
wanaochapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, kwenye
viwanja vya Kizota.
Banda maalum la Mamalishe ndani ya viwanja vya Kizota
Mtangazaji wa TBC Swedy Mwinyi, akiwa 'live' wakati wa mkutano mkuu wa
CCM, kwenye ukumbi wa Kizota, Dodoma, Kulia ni Swedy Mwinyi na Salum
Othman wa Shirika la Utangazaji Zanzibar.
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment