Baadhi
ya wanafunzi wanaosafiri kwa treni kutoka katikati ya Jiji la Dar es
Salaam kuelekea Ubungo wakiwa wamepanga mabegi yao kwenye mstari huku
wao wakiwa wamepumzika pembeni wakisubiri usafiri huo. Kwa utaratibu wa
kawaida wa usafiri huo abiria hutakiwa kupanga foleni ili inapowasili
kila abiria aingie kadri ya ulivyowahi kwenye foleni hiyo.

Na Mwandishi wa Thehabari.com
BAADHI
ya Wanafunzi jijini Dar es Salaam ambao hutumia treni ya abiria
inayofanya safari zake Ubungo na Katikati ya Jiji la Dar es Salaam
(Stesheni) wamebudi staili mpya ya kuepuka kupanga mstari mrefu huku
wakisimama muda mrefu kusubiri usafiri huo.
Wanafunzio
hao wanapofika mapema kituoni hupanga mabegi yao kwa mstari na wao
kupumzika pembeni hadi treni inapofika ndipo huinuka katika maeneo
mbalimbali waliokaa na kuingia kwenye mstari kwa kufuata begi la mtu.
Begi moja kwenye mstari humwakilisha mwanafunzi mmoja.
Thehabari
imeshuhudia utaratibu huu waliobuni wanafunzi kuepuka wao kusimama muda
mrefu wakiisubiri treni kuwasili kituoni. Kikawaida abiria wanaosafiri
kwa treni hiyo wakiwemo wanafunzi husimama kwa foleni kwa muda mrefu
wakisubiri usafiri huo, huku kukiwa hakuna viti vya kutosha kupumzikia
wasafiri wanaposubiri usafiri huo. Habari/Picha Imeletwa na Joachimu
Mushi wa The Habari
No comments:
Post a Comment