HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Mahafali ya 5 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)

Mlau wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Bertha Koda akiongoza wanataaluma katika Mahafali ya tano ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika Jumamosi 10, Novemba 2012. Jumla ya wahitimu 886 walihitimu ambapo 712 walitunukiwa Shahada ya kwanza ya Elimu ya Jamii na Ualimu, 39 Shahada ya kwanza ya Elimu katika Elimu ya Jamii, 33 Shahada ya kwanza ya Elimu katika Sayansi na 102 Shahada ya kwanza ya Sayansi na Ualimu.
Viongizi wakuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa tayari kwa ya Mahafali ya tano ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Balozi Fulgence Kazaura akiwatunukia shahada wahitimu katika Mahafali ya tano ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika Jumamosi 10, Novemba 2012.
wahititimu wakiwa katika Mahafali ya tano ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika Jumamosi 10, Novemba 2012.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam Abdul Njaidi (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanataaluma vijana wa chuo hicho.
 
CHANZO: MICHUZI BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: