HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAMA MZAZI WA ANETH ALIYEKATWA MKONO ATOA SHUKRANI KWA WATANZANIA WOTE WALIOFANIKISHA MTOTO WAKE KUTIBIWA

MAMA MZAZI WA ANETH ASERA MKANDARA

ANETH SASA ANAEDELEA VIZURI

MAMA ANETH AKIONGEA NA RASHIDI MKWINDA WA GAZETI LA MAJIRA HOSPITALINI HAPO

WAKAZI WA MBEYA WANAOENDA KUMWONA MTOTO ANETH HOSPITALINI

MAMA wa mtoto Aneth Johanes aliyefanyiwa unyama na hatimaye kukatwa mkono Asera Mkandara  ametoa shukurani kwa wananchi wa Mbeya na majirani waliosaidia kutoa taarifa na hatimaye kuokoa maisha ya mwanaye aliyekuwa akiishi kwa mateso.
Bi. Mkandara alizungumza hayo alipotembelewa na wanahabari waliofika wodi namba 8 kumjulia hali mtoto Aneth na kusema kuwa alipewa taarifa za kutokea kwa matatizo ya mwanaye lakini hakufafanuliwa ni tatizo gani alilopata.
Anasema kuwa amewasili Jijini Mbeya akitokea kwao Muleba Bukoba na kumkuta mwanaye Aneth ambaye ni mtoto wake wa pili baada ya mwanaye wa kwanza mwenye umri wa miaka 7 anayelelewa na bibi yake mjini Bukoba.
Anasema kuwa hata hivyo yeye hana shughuli maalumu zinazomuendeshea maisha yake isipokuwa biashara ndogo ndogo hivyo kuchukuliwa kwa mtoto wake na kaka yake aliyemtambulisha kwa jina moja la Mkandara ilikuwa ni sehemu ya msaada kwake.
Mama huyo anafafanua kuwa anashukuru kukuta mwanaye ni mzima na anawashukuru madaktari waliompa msaada kwani inawezekana huduma za matibabu zingechelewa angeweza kupata madhara makubwa.
Anasema kuwa kwa sasa anasaidiwa na ndugu na majirani na baadhi ya watu wanaomiminika hospitalini hapo kutoa msaada.
YEYOTE MWENYE MAPENZI MEMA ANAWEZA KUTOA MSAADA KUPITIA NAMBA YA SIMU YA MKONONI YA MAMA HUYO  0756-293784

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: