
Marehemu John Steven enzi za uhai wake
TASNIA
ya filamu nchini Tanzania, jana imefikwa na msiba mwingine Mkubwa wa
Msanii wa Filamu, John Stephano Maganga aliyefariki katika Hospitali ya
Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa Wasanii zinasema kuwa Mipango
ya mazishi inafanyika Nyumbani kwao Mwananyama A jirani na Kopakabana
Bar jijini Dar es Salaam.
Marehemu
John anaetarajiwa kuzikwa siku ya jumanne Makaburi ya Kinondoni Dar es
Salaam, alianza kujiingiza katika sanaa ya uigizaji mwaka 2001 chini
Thea na Deo Shija na ilipofika mwaka 2008 alianza kuigiza filamu na hadi
mauti yanamfika alikuwa njiani kutoa Filamu yake.
Aidha
Wasanii wote wanataarifiwa kufika katika Kikao Maalum Nyumbani kwa John
Stephan oleo Saa tisa alasiri kwaajili ya kupanga mikakati, ya mazishi.



No comments:
Post a Comment