Mtu mmoja
ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kufuatiaa vurugu zilizotokea leo majira ya
saa tano asubuhi katika eneo la barabara
ya Pamba karibu na soko kuu la jijini Mwanza katika vurugu baina ya
wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga na askari wa Halmashauri ya jiji
la Mwanza.
Mtu huyo
ambaye jina lake kamili halikupatikana badala yake ametambuliwa kwa jina moja
tu la Greda.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa leo mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi askari wa
halmashauri ya jiji wakiwa katika maeneo yao ya kazi eneo la barabara ya Pamba kwenye
stendi ya zamani ya mabasi ya Tanganyika karibu na soko kuu la jiji la Mwanza,
wakiwa katika operesheni zao za kawaida za kusafisha jiji walikamata bidhaa
zilizokuwa zimepangwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria wakiwa kwenye
eneo hilo mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mmachinga alimrukia mgambo wa jiji
shingoni na kumtolea silaha ya jadi aina ya sime kwa nia ya kumdhuru.
Baada ya
tukio hilo wamachinga waliokuwa eneo la tukio walianza kuwarushia mgambo hao wa
jiji mawe ndipo wale mgambo wa jiji katika kujihami wakaanza kurusha risasi
hewani kuwatawanya wamachinga hao
waliokuwa wakiongezeka kadri kuanza kwa seleka hilo, kwa bahati mbaya
moja kati ya risasi hizo zikampiga mpiga debe mmoja upande wa kushoto na kufariki
papo hapo.
Machinga
mwingine amejeruhiwa kwenye mkono wa kushoto katika kiwiko, naye dereva wa
magari ya biashara za kusafirisha mizigo
wa gari aina ya Kenta, magari ambayo hupaki katika eneo hilo amejeruhiwa upande
wa kushoto kichwani na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando kwa matibabu.



No comments:
Post a Comment