HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Mwenyekiti UWT Dar ala yamini


Mwenyekiti  wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Janet Masaburi
 
VIONGOZI wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wametakiwa kutekeleza ahadi  walizotoa kwa wanachama wao wakati  wakiomba kura.
Vilevile wagombea walioshindwa katika uchaguzi wa chama hicho kushirikiana na waliopata fursa ya kuwaongoza kuhakikisha chama kinarudisha imani kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Massaburi alisema viongozi waliochaguliwa wanatakiwa kuondokana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na kukifanya chama kupoteza dira.
“Kutokana na hali ya kisiasa hivi sasa, kiuchumi, kijamii na mabadiliko makubwa na misukosuko ya maisha ni vyema tukabadili staili ya utendaji,” alisema Massaburi na kuongeza:
“Muda mwingi unatakiwa kuutumia katika kutekeleza yale uliyoyaahidi wakati ukiomba kuwaongoza, kufanya hivyo tutarudisha imani ya waliotuchagua kwa kuwatumikia kwa ufanisi.”
Alisema utendaji wa wakati wa chama kimoja umekwisha na sasa kuna upinzani, hivyo wanatakiwa kuwa makini ili kuijenga CCM.
“Tufanye kazi na tuondokanane na rushwa, kwani hii yote inatokana na sisi kutokuwajibika ipasavyo hivyo kila mmoja akifanya kazi hakutakuwa na anayetaka rushwa,” alisema.
Pia, Mwenyekiti huyo aliwataka watendaji wa Dar es Salaam kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi, ikiwamo kuwapo na tathmini ya utendaji kila baada ya miezi mitatu.
“Nawaahidi miezi mitatu ya utendaji uliotukuka na kama haitakuwa hivyo katika mkutano wa kujitathmini, mkiona upungufu niondoeni,” alisema Massaburi huku akishangiliwa na wanachama.
Alisema uchaguzi wa chama hicho umemalizika na kilichobaki hivi sasa ni kuunganisha nguvu kwa pamoja kuhakikisha kinakubalika kwa wananchi na kuwezesha kuendelea kushika dola mwaka 2015.“Tuondoe tofauti zetu za uchaguzi na kilichopo mbele yetu ni kuhakikisha tunajitihidi kuwatumikia wananchi, ili kuhakikisha chama kinaendelea kuwapo madarakani,” alisema Massaburi.

CHANZO: MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: