HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » Ecobank yasherehekea miaka 40 kwa kampeni ya “Gutuka na Ecobank”



Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi Ecobank Tanzania, Innocent Urio (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni maalum ya “Gutuka na Ecobank”  inayolenga kuhamasisha Watanzania kuthamini utamaduni wa kuweka akiba.
Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo na Wakati (SME) Ecobank Tanzania, Juma Hamisi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni maalum ya “Gutuka na Ecobank” ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya huduma zake barani Afrika na miaka 15 tangu kuanza kwa huduma zake hapa nchini Tanzania.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu (kulia) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya “Gutuka na Ecobank” ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya huduma zake barani Afrika na miaka 15 tangu kuanza kwa huduma zake hapa nchini Tanzania.
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Maxwell Machange "Mzee Shayo" (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna alivyojipanga kuifikisha kampeni kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa wa kampeni maalum ya “Gutuka na Ecobank”
Mkutano ukiendelea 

Ecobank Tanzania imezindua kampeni maalum ya “Gutuka na Ecobank” ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya huduma zake barani Afrika na miaka 15 tangu kuanza kwa huduma zake hapa nchini Tanzania.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika Septemba 10, 2025 na itadumu kwa miezi mitatu, ambapo wateja watakaoweka akiba kupitia akaunti ya Supa Seva watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki za miguu mitatu (Gutas) na pesa taslimu  hadi shilingi milioni moja. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Innocent Urio amesema kampeni hiyo inalenga kuhamasisha watanzania kuthamini utamaduni wa kuweka akiba.

“Kupitia kampeni hii, wateja wetu watajipatia zawadi, lakini muhimu zaidi ni kujifunza thamani ya akiba kwa maisha yao ya kifedha,” alisema Urio.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo na Wakati (SME), Juma Hamisi, alisisitiza kuwa wafanyabiasha sasa wana nafasi ya kunufaika na kampeni ya Gutuka na Ecobank ambapo mteja atakayefungua akaunti ya Supa Seva inampa mteja riba hadi asilimia 5 kwa robo mwaka bila makato ya mwezi, fursa ya kutoa pesa bure mara moja kila mwezi na huduma ya Lipa Namba bure kwa wateja wa SME na kadri mteja anavyoweka akiba zaidi, ndivyo anavyozidisha nafasi ya kushinda zawadi kubwa.

“Gutuka na Ecobank ni zawadi kwa wateja wetu kutokana na uaminifu wao katika safari ya miaka 40 barani Afrika na miaka 15 nchini Tanzania. Ni hatua ya kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa maisha bora kifedha,” alisema Hamisi.

«
Next
This is the most recent post.
»
Previous
Older Post

No comments: