Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali
na kumpa pole Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga ambaye
amelazwa katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kufuatia majeraha ya usoni na kifuani yaliyotokana na
kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika
Kiwanja cha Mwanakwerekwe mjini Unguja juzi. Rais ambaye amerejea
Jumanne Novemba 6, 2012 akitokea katika ziara ya kikazi ya takriban
juma moja katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida,
amemtakia Sheikh Soraga nafuu ya haraka.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment