Msanii/Muigizaji/Mchekeshaji Hussein Ramadhani Mtioeti (27) maarufu SHARO MILIONEAenzi za Uhai wake
Mwili wa Sharo Milionea kama unavyoonekana baada ya ajali mbaya ,meno yake yaling'oka baada ya ajali hiyo

Hili ni moja kati ya magari ya msanii Sharo Milionea (japo hili silo alilokuwa nalo wakati akipata ajali

Hili ni moja kati ya magari ya msanii Sharo Milionea (japo hili silo alilokuwa nalo wakati akipata ajali
Msanii/Muigizaji/Mchekeshaji Hussein Ramadhani Mtioeti (27) maarufu SHARO MILIONEA amefariki dunia katika ajali ya gari jijini Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe, amethibitisha kutokea kwa ajali na kusema kuwa marehemu amefikwa na umauti baada ya gari lake aina ya Toyota Haria lenye namba za usajili T478DVR kuacha njia na kupinduka.
Hili
ni pigo jingine kwa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania, hasa ukizingatia
kuwa juma lililopita alifariki msanii Mlopelo na wakati Sharo Milionea
anafariki tayari tasnia hiyo ya bongo Move ipo katika Msiba mwingine
mzito wa Mcheza Filamu John Steven anaetarajiwa kuzikwa kesho.
Kamanda
Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku wa
Novemba 26, 2012 katika kijiji cha Maguzoni Soga Wilaya ya Muheza Mkoani
Tanga.
Akisimulia
zaidi RPC Massawe anasema kuwa marehemu alikuwa akiendesha gari hilo na
alikuwa peke yake bila abiria mwingine na ajali kumfika akiwa katika
kijiji hicho kilichopo kati ya segera na Muheza.
“Marehemu
ndie alikuwa akiendesha gari lile, na lililopopinduika yeye alirushwa
nje lkupitia kiooo cha mbele na umauti kumfika hapo hapo” alisema
Kamanda Massawe.
Aidha Kamanda Massawe amesema msanii huyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam na alikuwa akienda nyumbani kwao Muheza.
Inakumbukwa
kuwa Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa staili yake ya
utembeaji na uongeaji alipata al;inusurika katika ajali nyinge mapema
mwaka huu baada ya basi alilokuwa akisafiria la Taqwa kutoka nchi jirani
ya Burundi kupata ajali Mikese mjini Morogoro Januari 5 mwaka huu
akirejea Dar es Salaam.
Father
Kidevu Blog inatoa salamu za Pole kwa Familia, wasanii wa Filamu,
Vichekesho na muziki nchini kwa Msiba huo mzito hasa ukizingatia kuwa
bado wapo katika Msiba wa Mcheza filamu John Stephen anaetarai kuzikwa
kesho Makaburi ya Kinondoni.





No comments:
Post a Comment