Nguruwe
Utafiti wa wanasayansi kutoka Canada unaashiria kuwa aina hatari zaidi
ya virusi vya Ebola inaweza kusambazwa hewani kati ya aina mbili ya
viumbe.
Matokeo ya utafiti huo, yanasema kuwa nguruwe waliokuwa wameambukizwa
aina ya Ebola kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waliweza
kuipitisha kwa nyani, bila ya kugusana.
Watafiti
hao wanadhani maambukizi ya aina hiyo yanachangia kusambaa kwa ugonjwa
huo hatari barani Afrika, na kwamba nguruwe huenda wanabeba virusi
hivyo.
Lakini wanaamini ugonjwa huo unaweza tu kusambazwa katika eneo dogo, na hauwezi kusambaa haraka kama homa.
Nchini Uganda, mkurupuko mpya wa Ebola umewauawa watu wawili karibu na mji mkuu, Kampala.
Virusi vya ugonjwa huop wa Ebola, husababisha maafa kwa bvinadamu na viumbe vingine mbali na binadamu.
Matokeo ya uchunguzi huo yamechapishwa kwenye jarida ya kimatibabu.
Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO,
maambukizi miongoni mwa binadamu husambazwa kwa watu kukaribiana,
kupitia damu, unyevu mwilini na maji maji yanayotokana na wanyama
wengine kama vile, sokwe na Swara.
Popo vile vile amekisiwa kuwa chanzo cha maambukizi hayo ya viruso vya ebola.
Lakini baada ya utafiti kufanya, imebainika kuwa nguruwe wanaofugwa nyumbani au wale wa mwituni wanaweza kuwa vyanzo vya virusi hivyo ambavyo ni hatari zaidi.
Lakini baada ya utafiti kufanya, imebainika kuwa nguruwe wanaofugwa nyumbani au wale wa mwituni wanaweza kuwa vyanzo vya virusi hivyo ambavyo ni hatari zaidi.
CHANZO: BBC SWAHILI



No comments:
Post a Comment