Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh . Hawa Ghasia (kulia) akiteta jambo na
mtaalamu wa masuala ya biashara kutoka Baraza la Biashara la Taifa
(TNBC) Wille Magehema katika mkutano maalumu wa ushirikiano kwa manufaa
ya wote (smart partnership dialogue) uliohusisha wakuu wa mikoa, wakuu
wa wilaya na makatibu tawala wa mikoa.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia (kulia)
akibadilishana mawazo na mtaalamu wa masuala ya biashara kutoka Baraza
la Biashara la Taifa (TNBC) Wille Magehema katika mkutano maalumu wa
ushirikiano kwa manufaa ya wote (smart partnership dialogue) uliohusisha
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa mikoa.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Bishara la Taifa (TNBC), Bw. Samson
Chemponda (kulia) akimsikiliza kwa makini Inspekta Jeneral wa Polisi
(IGP), Said Mwema muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa mkutano
maalumu wa ushirikiano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership Dialogue)
uliohusisha wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa mikoa,
katikati ni mtaalamu wa masuala ya biashara kutoka baraza la biasha la
Taifa (TNBC), Mr. Wille Magehema.
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda, amewataka viongozi wa serikali nchini
kuchukulia kwa umakini suala la Ushirikiano wa manufaa kwa wote
(smartpartership dialogue) kuwa moja ya chachu kubwa ya kuleta maendeleo
katika maeneo yao na Taifa kwa ujumla.
Kauli
hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa
mkutano maalumu wa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa
mikoa juu ya ushiriki wao katika majadiliano ya pamoja ya kuhusu
ushirikiano kwa manufaa ya wote.
“Mikutano
ya ‘smart partnership Dialogue’, ni tofauti na mikutano mingine, hili
ni jukwaa la majadiliano kati ya serikali na jumuiya mbalimbali za
wananchi kuhusu jambo lolote lenye manuafaa kwao, na ambalo kwa namna
moja ama nyingine litaleta maendeleo yao kijamii na kiuchumi,”
alisisitiza Mh. Pinda.
Alisema
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa ujulikanao kama “
Global 2013 Smart partnership Dialogue” na hii ni kutokana na ahadi ya
Rais Jakaya Kikwete aliyotoa wakati alipohudhuria mkutano kama huo
Petrojaya nchini Malaysia mwezi Juni mwaka 2011, mkutano ulioitwa “
Langkawi smart partnership dialogue”.
Aliongeza
kuwa lengo la majadiliano haya ni kupata maoni na mawazo kutoka kwa
watu wa kawaida kuanzia ngazi za chini mpaka juu, dhana hii inatambua
kwamba kila mtu anao mchango wake kwenye jumuiya anayoishi ili kuleta
mabadiliko katika jamii.
“Katika
hili ndugu zangu, viongozi wa ngazi za juu serikalini hukaa pamoja kama
watu wa ngazi sawa na jumuiya za wananchi, zikiwemo za vijana, wasomi,
wafanyakazi, wafanyabiashara, waandishi wa habari, wanasanaa, wanasiasa,
madhehebu ya dini na kwa ujumla wake jumuiya hizi hujulikana kama smart
partnership links” alisisitiza Waziri Mkuu.
Alisema
serikali kwa sasa ina mkakati mzuri wa kutambua mchango wa wabunifu na
wagunduzi katika kuendeleza sayansi na teknolojia, huku akisisitiza kuwa
jukwaa hili la kimataifa liwe sehemu kupanua ushirikiano wa kimataifa
katika nyanja ya teknolojia na ubunifu.
“Kuna
wagunduzi wanaopatikana kule, hivyo ni lazima kuwe na mikakati ya
kuwabaini na kuwaendeleza ili kazi zao zaisaidie kuendeleza uchumi wa
nchi yetu na kujiletea maendeleo miongoni mwetu” aliongeza Waziri Mkuu.
Kwa
upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC)
Bw. Samson Chemponda, alisema majadiliano hayo yanatoa fursa hasa kwa
mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya katika kuweka mikakati yao ya
kibiashara katika maeneo yao hasa kwa kushirikisha wadau wa eneo husika
katika ushiriki wao.
“Sisi
tukiwa ni wahusika wakuu katika hili tutahakikisha kuwa mpango huu
unafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika nchi hii, hivyo ni jukumu letu
kuhakikisha kuwa wananchi katika kada zote wanatambua na kuelewa dhana
hii kwa ukubwa na upana wake,” alisema Chemponda.
Alisisitiza
kuwa wao kama baraza wanalojukumu kuhakikisha kuwa ushirikiano wa
manufaa kwa wote unaeleweka kwa kutoa elimu kwa wadau wote ili kuleta
manufaa kwa jamii nzima.
Elimu
ndo msingi wa kila kitu, tutahakikisha tunatoa elimu kuhusu dhana hii
katika ngazi zote za uongozi na sehemu mbali mbali hapa nchini ili kila
mtu aweze kushiriki katika nafasi yake kama mwananchi na kutoa mawazo
yake,” alisisitiza Bw. Chemponda.



No comments:
Post a Comment